zulushaka
JF-Expert Member
- Feb 5, 2017
- 372
- 298
Hv vitu nikivinunua online naenda kuvipata wapi mf km hyo cdONYO KUBWA SANA
Usithubutu kumfanyia hivi mwanamke au mwanaume unayempenda sana, kwa kuwa unaweza kufa kwa presha, kama anakupenda, anakusikiliza, haina haja ya kumchunguza. Kwani unapomchunguza uwe tayari kukabiliana nayo yale utakayoyaona.
Kuna mambo mengi sana kupita kiasi, usimchunguze MTU ambaye hajakufanyia vitu vyovyote.
Kuna SIM CARD READER hii kitu ni mwisho wa matatizo yote, unainunua online na inakuja na CD yake ya software, unainstall hiyo CD kwenye laptop yako, hiyo card reader ipo kama flash disc, kuna sehemu ya kupachika laini ya SIMU, unapachika then unaichomeka kwenye laptop kupitia USB kama flash, ni balaa itasoma vitu vya tokea laini ilipoanza kutengenezwa, vilivyofutwa na vilivyopo.
Niliwahi kumfanyia hivi aliyekuwa mke wangu ambaye sasa tumeshaachana, aliniona sifai haswa maana kila nilipomueleza mimi si mtu wa nchi hii hakuwa akiamini, alikuwa ni mtu wa kuficha ficha simu yake, ukigusa tu simu yake ugomvi mkubwa sana na tayari niliona siwezi kuwa naye tena, nikaifanya hiyo kazi niliyoyaona humo ni siri yangu, lakini haikuwa tens ndoa mpaka leo.
Pia polisi walinikasirikia sana wakaniambia nimedukua nyaraka za siri sana, ilibidi nimlipe mwanamke fidia kesi isifike mbele kwani ingeweza kuwa na matatizo kwangu, SIM CARD READER ilileta meseji zake zote ambazo alikuwa akizifuta anapomaliza tu kuwasiliana na mabwana zake.