Kata tiketi za ndege Tanzania kupitia WhatsApp sasa

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Wakati Teknolojia inazidi kushika Kasi ulimwenguni Sasa kampuni ya Precision Air imeleta njia Rahisi ya kukata tiketi, Sasa utakua na uwezo wa kukata tiketi za safari ya ndege kupitia mtandao wa WhatsApp.

View attachment 2703035

Mfumo huu umepewa jina la Swala umezinduliwa tarehe 26 Julai mwaka 2023 na naibu Waziri wa ujenzi na uchukuzi Mr Godfrey Kasekenya.

Mkurugenzi wa Precision Air Mr Patrick Mwanri amesema mtu yeyote atakayekata tiketi ya safari za ndege za Precision Air kupitia mfumo wa Swala hatokutana na Ugumu wowote.

Hatua zote unafanya mwenyewe kupitia simu yako na kupata tiketi yako ndani ya Muda mfupi , hiyo ndiyo itakua tiketi yako ambayo utaweza kuonyesha mwenyewe wakati unataka kusafiri.

View attachment 2703036

Mwanri ameongezea kwa kusema hii ndo Huduma ya kwanza kwa upande wa Afrika Mashariki pamoja na Tanzania kwa ujumla kwani mchakato wa huu ulianza mwaka 2019 ila kutokana na changamoto ya uviko ulichelewa kuanza ila sasa rasmi.

Mfumo huu unakupa uwezo wa kulipia kwenye simu sio lazima utafute wakala , ikiwa hauna pesa kwenye simu unapewa namba ya booking Ili uweze kujihudumia amesema Mwanri.

ATR-72-500_Precision_Air_Services_(PRF)_F-WWEW_-_MSN_923_-_Named_Kilimandjaro_-_Will_be_5H-PWG...jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom