Maumivu ya mapenzi ni zaidi ya msiba

Maumivu ya mapenzi ni zaidi ya msiba

kwanza mwanaume huwa haliiukiona halii amepungukiwa sifa za uanaume, ulisema ulimjali kulioko ndugu zako na wadogo zako hii inaonyesha una upendo wa kweli kwa ndugu zako ingawa upendo wa ndugu na mpenzi wako haviwezi kulingana kwani kila mmoja ana nafasi yake mwisho ukipata msiba huyo mtu amepotea moja kwa moja hawezi kurudi lakini ukiachana na mpenzi wako ni maumivu ya muda hivyo huwezi kufananisha kupoteza mpenzi na msiba ingawa hujaeleza umri wako nalo linaweza kuwa tatizo
 
Pole sana, mapenzi yanaumiza sana na hasa umpnde MTU aside kupenda na unajua kabisa hakupnd ila unajpndekeza, inauma sana aseee.
 
Hahaha. Eti nikiachwa. Mimi nimeshaacha na kuachwa mara kibao lakini sijawahi umia roho wala mwili ndo maana nashangaa wanaosema maumivu ya mapenzi. Hata niliyenaye akifa ndo nitaumia lakini akiniacha hata leo wala sitajisikia vibaya. Ndo maana nikasema labda naumwa sijijui maana I don't feel what others claim to feel.
Then you have never experience what love is..and how is it feel when you love someone I doubt so..
 
Upo sahihi sana mkuu...ILA hata huyo wa malengo mimi nilishaumizwa naye na nikakoma na kuamua kutompenda tena kwa 100%

Kwanza yuko wapi binti wa kumpenda kwa 100% sikuhizi?

USIJE KOSEA UKAMWAMINI MWANAMKE.
Kazi kweli kweli !
 
Watalaamu wa mambo ya mahusiano wanasema hivi: Mpenzi akikukose kosa ambalo inabidi muachane nae kwa huo huo muda usimwache, usifanye hivo utaumia zaidi. 1. utaumia kwa kosa alokutendea 2. utaumia kwa kumkosa 4rever. so inabidi uvumilie ukiendelea kuwa nae huku ukiwa unaigiza igiza tuu kumpenda ili maumivu yapungue coz hata km amekukosea sana angalau ukiwa unamuona maumivu hupungua. ukishakaa sawa piga chini hamna maumivu nakuhakikishia hilo
Na ukiwa humwoni kabisa?
 
nilipoteza best friend yangu mwaka jana,hamna maumivu kama yale mpaka leo kuna sehemu au k2 nikikumbuka hua namkumbuka yeye..usifananishe maumivu ya kufiwa na mapenz..ukifiwa hupat replacement.

Nimefiwa na uncle wangu mwaka jana zaidi ya uncle halafu alikuwa kaniita kwake tukaongea sana siku hiyo mpaka saa nane usiku kesho yake anakufa halafu mpuuzi anafananisha kifo na upuuzi wa mapenz pumbavu kabisa
 
Habarini za asubuhi wana MMU,

Ni yapata mwezi mmoja na wiki mbili umepita sasa, tangu niachane na Girlfriend niliyetokea kumpenda saaana nakiri kuwa nilikuwa namuhudumia na kumjali kuliko hata wadogo zangu na familia yangu kiujumla lakini mwisho wa siku alinifanyia kitu cha ajabu saana, mwanaume nililia saana, sikuweza kula wala kuoga kilichonisaidia nilikuwa OFF hivo ile wiki yote ambayo nlikuwa siendi kazini niliiona kama mwaka kwangu nashkuru Mungu hicho kipindi kilipita vizuri na hatimaye niliingia ulimwengu mwingine wa usingle life.

Wadau, usiombe ukutwe na hili janga binafsi nimeprove kuwa maumivu ya msiba yanapita kwa muda mfupi lakini maumivu ya mapenzi hudumu kwa muda mrefu, hasa pale unapo kumbuka yale yote ambayo mliyafanya pamoja.

Pia nawashukuru sana wale wote walionitia moyo katika kile kipindi kigumu ambacho nilikuwa napita, ingawa sijatengamaa bado maana yote yalonitokea nilikuja kuomba ushauri hapa jamvini.

Niwaombe wale wote ambao mnatarajia kuingia katika mahusiano, kuweni sana makini yawapasa muwe na tahadhari kubwa sana, usiingie na miguu yote kama mimi nilivyofanya, maana siku hizi maigizo ni makubwa kuliko upendo yaani kupitia maigizo yake, unaweza thibitisha kuwa unapendwa lakini mwisho wa siku unashangaa gia imebadilishwa angani.Pia mshirikisheni sana Mungu kwa wote ambao mpo tayari kwenye mahusiano ili awaepushie mbali na shari.

Niwaombe wote ambao mmepitia maumivu ya mapenzi kwa namna moja ama nyingine, tujuzane hapa na pia ukielezea ni kwa namna gani uliweza kuvuka salama ili iwe msaada kwa wengine pia.

Nawasilisha hoja, ahsanteni sana
Pole sana, ila unaonekana haujafiwa na mzazi wako hata Mmoja.
 
Nimefiwa na uncle wangu mwaka jana zaidi ya uncle halafu alikuwa kaniita kwake tukaongea sana siku hiyo mpaka saa nane usiku kesho yake anakufa halafu mpuuzi anafananisha kifo na upuuzi wa mapenz pumbavu kabisa

Pole sana, ila unaonekana haujafiwa na mzazi wako hata Mmoja.
Wakuu embu acheni hizi mambo, kama hazijawakuta mna lolote mnaweza kuongea.

Mzazi au mtu wako wa karibu anaweza kukutoka ukaumia sana lakini ukija kukum buka ni safari inayomhusu kila mtu unajifariji huenda mtakuja onana.

Hii kitu acha watu wajiue si ya kubeza, ni kuomba usiwe cast tu.
 
Naomba usini Quote kwa huu upumbavu wako, nina msiba wa kufiwa na wazazi wangu kwa siku moja na maumivu ya hayo mapenzi nayajua vizuri lakini hata siku moja sijaona kama yanaingia pale hata nusu, kumbuka mapenzi kuna replacement japo inauma lakini kamwe maumivu yake huwezi fananisha na msiba tena wa wapendwa wako, labda kama unataka kuchangamsha kijiwe tu.
 
Jaman mm nawaambia kama hujatendwa furahi kusimuliwa ukikutwa!!!!!!!
Mimi sijawahi kutendwa enzi sijaoa nilikua msanii hivyo binti akijifanya kunitenda namwangalia .sikuwahi kuwa na mapenzi ya dhati mpaka nilipompata shemeji yako.huyu kwakweli nampenda nakiri nikimkosa nitayumba kidogo lakini nitakaa sawa.
 
Naomba usini Quote kwa huu upumbavu wako, nina msiba wa kufiwa na wazazi wangu kwa siku moja na maumivu ya hayo mapenzi nayajua vizuri lakini hata siku moja sijaona kama yanaingia pale hata nusu, kumbuka mapenzi kuna replacement japo inauma lakini kamwe maumivu yake huwezi fananisha na msiba tena wa wapendwa wako, labda kama unataka kuchangamsha kijiwe tu.
Pole kwa kufiwa.

Nakijua nilichikiandika, sijaandika kwa bahati mbaya.wakati wako ukifika utanielewa. Ingawa sio lazima kufika, unaweza usionje pia.

Asante.
 
Upo sahihi sana mkuu...ILA hata huyo wa malengo mimi nilishaumizwa naye na nikakoma na kuamua kutompenda tena kwa 100%

Kwanza yuko wapi binti wa kumpenda kwa 100% sikuhizi?

USIJE KOSEA UKAMWAMINI MWANAMKE.
Chanzo ni sisi wanaume.
 
watu mnapenda vibaya sijui kwa nini...ukitakausiuie penda kiasi...au kuwa na wawili watatuakikuzingua huyu unahaia kwingine....mhh....ila mimi sipendi kihivo wala si invest mahelaaaa kama hatujawa pamoja...kuwa na kiasi
 
Na ukiwa humwoni kabisa?
Endelea kuwasiliana nae kwa ukaribu zaidi kuliko kawaida. maana utapokuwa unaisikia sauti yake angalau itapoza machungu na maumivu. ukishaona unaanza kuwa sawa piga chini
 
Back
Top Bottom