Maumivu ya mapenzi ni zaidi ya msiba

Maumivu ya mapenzi ni zaidi ya msiba

Bilgert hiyo setuation kila mwaname takriban inampitikia katika maisha yk., mimi mara 3 saivi nishazoea be strong, alafu kizuri zaidi nilichokigundua demu akikuacha kwa ukatili kama ivyo baada ya mda hurud mwenyewe apo unamkaanga upendavyo.

Ahsante saana mkuu londoni...binafsi najiona nmekomaa sasa.na nina uhakika sitokuja umia tena ktk suala la Mapenzi
 
Mpenzi wako akifa roho haiumi kama akikusaliti.kuna aina nyingi za usaliti ila usikutane na usaliti dharau huu ni balaa bora yule anaekusaliti huku bado anakujali na kukuonysha mapenz
 
Habarini za asubuhi wana MMU,

Ni yapata mwezi mmoja na wiki mbili umepita sasa, tangu niachane na Girlfriend niliyetokea kumpenda saaana nakiri kuwa nilikuwa namuhudumia na kumjali kuliko hata wadogo zangu na familia yangu kiujumla lakini mwisho wa siku alinifanyia kitu cha ajabu saana, mwanaume nililia saana, sikuweza kula wala kuoga kilichonisaidia nilikuwa OFF hivo ile wiki yote ambayo nlikuwa siendi kazini niliiona kama mwaka kwangu nashkuru Mungu hicho kipindi kilipita vizuri na hatimaye niliingia ulimwengu mwingine wa usingle life.

Wadau, usiombe ukutwe na hili janga binafsi nimeprove kuwa maumivu ya msiba yanapita kwa muda mfupi lakini maumivu ya mapenzi hudumu kwa muda mrefu, hasa pale unapo kumbuka yale yote ambayo mliyafanya pamoja.

Pia nawashukuru sana wale wote walionitia moyo katika kile kipindi kigumu ambacho nilikuwa napita, ingawa sijatengamaa bado maana yote yalonitokea nilikuja kuomba ushauri hapa jamvini.

Niwaombe wale wote ambao mnatarajia kuingia katika mahusiano, kuweni sana makini yawapasa muwe na tahadhari kubwa sana, usiingie na miguu yote kama mimi nilivyofanya, maana siku hizi maigizo ni makubwa kuliko upendo yaani kupitia maigizo yake, unaweza thibitisha kuwa unapendwa lakini mwisho wa siku unashangaa gia imebadilishwa angani.Pia mshirikisheni sana Mungu kwa wote ambao mpo tayari kwenye mahusiano ili awaepushie mbali na shari.

Niwaombe wote ambao mmepitia maumivu ya mapenzi kwa namna moja ama nyingine, tujuzane hapa na pia ukielezea ni kwa namna gani uliweza kuvuka salama ili iwe msaada kwa wengine pia.

Nawasilisha hoja, ahsanteni sana
1. Msamehe aliyekukosea huku ukiamini kuwa kila jambo hupangwa na Mungu.
2. usiweke jambo/tukio hilo akilini kila wakati na epuka tabia ya kuwa mpweke muda mwingi.
3. Tfuta jambo lakufanya ambalo ni positive ili liweze kuku-keep bussy, inaweza kuwa kazi au mazoezi.
4.Toa kila mabacho unajua alikilwta au kukiweka yeye ambacho unajua kila ukikiona unamkumbuka na kuumia.
5. Futa namba ykae, meseji zake, picha zake na chati zake kutoka kwenye simu yako.
6. M-block kwenye page zako na profile zako za nsocial network.
7. Tafuta kipozeo kitakachokusadia kupumua na kuziba pengo lake, ikiwezekana awe bomba zaidi ya yeye.
8. Usijarbu kuziba pengo lake kwa Pombe, haitokusaidia zaidi ya kukuongeze machungu pale pombe zitakapokwisha.
 
Ahsante sana kwa ushaur wako mkuu....ubarikiwe saana
 
Jamani sijui mimi naumwa au la. Nimewahi kupiga chini na kupigwa chini mara kadhaa lakini sijawahi hata kuumia. Hayo maumivu yanakuwaje mdau? Kama tumbo lililovurugika, kama jino au yakoje? Unajisikiaje isee?
 
Kuachwa ni maumivu jamani..hayapimiki nimejifunza kutokumuamini mtu anayeitwa mwanaume zaidi ya baba yangu mzazi kila siku nauambia moyo koma kazi yako kusukuma damu acha kiherehere
Yakoje hayo dada? Ni kama maumivu ya jino, tumbo lililovurugika. What is it really?
 
mapenzi ni mapenzi habari ya msiba ni ingine asikuambie mtu kabisa inauma inauma tena saaaaaana jamani msiba Mmmmh
 
Back
Top Bottom