Mapenzi ya dhati na matamu zaidi ni faragha, haya ya kujionyesha mitandaoni na kwenye public ni unafiki mtupu na ni chanzo kikuu cha kutengana

Mapenzi ya dhati na matamu zaidi ni faragha, haya ya kujionyesha mitandaoni na kwenye public ni unafiki mtupu na ni chanzo kikuu cha kutengana

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
44,008
Reaction score
36,133
Kwanza kabisa ni kwamba mapenzi ya mitandaoni na kujionyesha kwenye public hua hayadumu kwasababu hua ni unafiki mtupu. Ila yale ya faragha hudumu zaidi kwasababu hua ni ya dhati, ya kweli na tena hujaa furaha ya kweli, msamaha wa kweli, ustahimilivu na subra.

Mapenzi ya mitandaoni na kwenye public huchochea na kuatract laana za watu na maombi mabaya mabaya ya wanaokerwa na aina hiyo ya mapenzi na matokeo yake one mistake one goal. Hayanaga msamaha wa kweli, hayanaga kuvumiliana na wala hayanaga subra. Huvunjika kwa haraka sana tena kwa kosa moja dogo sana miongoni mwa wahusika. Kwasababu wahusika wa aina hii ya mapenzi au ndoa za kinafiki hua na kazi kubwa tatu, moja ni kumfurahisha mwenzi wake, pili kufurahisha watu wa mitandaoni, na tatu kuifurahisha jamii inayo kuzunguka.

Sote ni mashahidi juu ya namna ambavyo wanao anika mahusiano au ndoa zao mitandaoni wanavyovurugana na kusambaratika upesi na kirahisi sana. Unaweza kuweka mifano mingi mwenyewe kadiri uwezavyo. Mapenzi ya mitandaoni daima hulenga kuwafurahisha au kuwakera watu wa mitandaoni, na hivyo unafiki hua ndio msingi mkuu wa aina hiyo ya mapenzi.

Lakini wale waliokataa kutumia mitandao ya kijamii kuonyesha maisha ya mapenzi au ndoa zao, daima wamekua wakiinjoy zaidi wao wenyewe wakiwa ndani ya nyumba zao, bila kulenga kuwafurahisha au kuwakera watu wa mitandaoni au publics kwa ujumla.

Je,
ungependelea kua na maisha gani kwenye mahusianao au ndoa yako ili uinjoy zaidi?
ni yale ya kuinjoy kwa kujionyesha mitandaoni na wasiohusika nayo au yale ya faragha ya kuinyoy wewe na mwenzi wako pekee? :BASED:

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom