Maumivu ya mapenzi ni zaidi ya msiba

BILGERT

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
6,534
11,010
Habarini za asubuhi wana MMU,

Ni yapata mwezi mmoja na wiki mbili umepita sasa, tangu niachane na Girlfriend niliyetokea kumpenda saaana nakiri kuwa nilikuwa namuhudumia na kumjali kuliko hata wadogo zangu na familia yangu kiujumla lakini mwisho wa siku alinifanyia kitu cha ajabu saana, mwanaume nililia saana, sikuweza kula wala kuoga kilichonisaidia nilikuwa OFF hivo ile wiki yote ambayo nlikuwa siendi kazini niliiona kama mwaka kwangu nashkuru Mungu hicho kipindi kilipita vizuri na hatimaye niliingia ulimwengu mwingine wa usingle life.

Wadau, usiombe ukutwe na hili janga binafsi nimeprove kuwa maumivu ya msiba yanapita kwa muda mfupi lakini maumivu ya mapenzi hudumu kwa muda mrefu, hasa pale unapo kumbuka yale yote ambayo mliyafanya pamoja.

Pia nawashukuru sana wale wote walionitia moyo katika kile kipindi kigumu ambacho nilikuwa napita, ingawa sijatengamaa bado maana yote yalonitokea nilikuja kuomba ushauri hapa jamvini.

Niwaombe wale wote ambao mnatarajia kuingia katika mahusiano, kuweni sana makini yawapasa muwe na tahadhari kubwa sana, usiingie na miguu yote kama mimi nilivyofanya, maana siku hizi maigizo ni makubwa kuliko upendo yaani kupitia maigizo yake, unaweza thibitisha kuwa unapendwa lakini mwisho wa siku unashangaa gia imebadilishwa angani.Pia mshirikisheni sana Mungu kwa wote ambao mpo tayari kwenye mahusiano ili awaepushie mbali na shari.

Niwaombe wote ambao mmepitia maumivu ya mapenzi kwa namna moja ama nyingine, tujuzane hapa na pia ukielezea ni kwa namna gani uliweza kuvuka salama ili iwe msaada kwa wengine pia.

Nawasilisha hoja, ahsanteni sana
 
Mimi nililia sana tena sana kitandani hadi nkapitiwa usingizi ilinisaidia kupunguza uchungu na hasira nilozokuwanazo.....nilipoamka nikaoga vizuriii nikaupara mwenyewe nikajitoa out na rafiki angu kipenzi .... Baada ya hapo mmmh kama sio mimi nikawa busy sana na kanisani mpaka Leo nakwambia nashine tu .....
 
Mimi nililia sana tena sana kitandani hadi nkapitiwa usingizi ilinisaidia kupunguza uchungu na hasira nilozokuwanazo.....nilipoamka nikaoga vizuriii nikaupara mwenyewe nikajitoa out na rafiki angu kipenzi .... Baada ya hapo mmmh kama sio mimi nikawa busy sana na kanisani mpaka Leo nakwambia nashine tu .....


Aiseee,nashkuru kwa kunishirikisha kisa chako mkuu.yaani maumivu ya mapenzi ni UN DIFINED
 
Mimi nililia sana tena sana kitandani hadi nkapitiwa usingizi ilinisaidia kupunguza uchungu na hasira nilozokuwanazo.....nilipoamka nikaoga vizuriii nikaupara mwenyewe nikajitoa out na rafiki angu kipenzi .... Baada ya hapo mmmh kama sio mimi nikawa busy sana na kanisani mpaka Leo nakwambia nashine tu .....

Wewe ni wa kike au kiume?
 
Habarini za asubuhi wana MMU.Ni yapata mwezi mmoja na wiki mbili umepita sasa,tangu niachane na Girlfriend niliyetokea kumpenda saaana...nakiri kuwa nilikuwa namuhudumia na kumjali kuliko hata wadogo zangu na familia yangu kiujumla.lkn mwisho wa siku alinifanyia kitu cha ajabu saana,mwanaume nililia saana,ckuweza kula wala kuoga.kilicho nisaidia nilikuwa OFF..hvo ile wiki yote ambayo nlikuwa siend kazini niliiona kama mwaka kwangu.nashkuru Mungu hicho kipnd kilipita vizur na hatimaye niliingia ulimwengu mwingine wa usingle life.

Wadau,usiombe ukutwe na hili janga.Binafsi nmeprove kuwa Maumivu ya msiba yanapita kwa muda mfupi lakini maumivu ya mapenzi hudumu kwa muda mrefu,hasa pale unapo kumbuka yale yote ambayo mliyafanya pamoja.

Pia nawashukuru sana wale wote walionitia moyo ktk kile kipind kigumu ambacho nilikuwa napita,ingawa sijatengamaa bado.maana yote yalonitokea nilikuja kuomba ushauri hapa jamvini.

Niwaombe wale wote ambao mnatarajia kuingia katika mahusiano,kuweni saana makini.yawapasa muwe na tahadhar kubwa saana,,usiingie na miguu yote kama mm nilivofanya,maana siku hizi maigizo ni makubwa kuliko upendo.yaani kupitia maigizo yake,unaweza thibitisha kuwa unapendwa lkn mwsho wa siku unashangaa gia imebadilishwa angani.Pia mshirikisheni sana Mungu kwa wote ambao mpo tayar kwenye mahusiano ili awaepushie mbali na shari.

Niwaombe wote ambao mmepitia maumivu ya mapenz kwa namna moja ama nyingine,tujuzane hapa.na pia ukielezea ni kwa namna gani uliweza kuvuka salama.ili iwe msaada kwa wengne pia.



Nawasilisha hoja...Ahsanteni saaaana
Ukajitoa mtoto wa watu, ukafikiri ni waifu. Kumbe kuna wenzio walikuwa wanakula kiulaini wakaamua kuchukua kabisaaaa.
Funzo , next time when you fall in live, dont spend too much money kwaajili yake, inaonyesha maumivu yako yamezidi si kwa upendo tu bali pia ni kwa gharama ulizoingia juu yake
 
Kwa jinsi ulivyoandika nilitaka nikushukie kama ungekuwa dume, lakini nikaona ni vyema nikauliza kwanza kuliko kusadiki na kuishia kukosea.
Kwann unishukie akati kila Mtu kuna njia yake ya kumpunguzia maumivuu jamani..kuna nini baya na nilichoandika?
 
Mmh pole usitue bag na rambo vyote utakufa ooh watch out next time,ukiwa ndoani tua vyote
 
Back
Top Bottom