Maudhui ya nyimbo za Taifa HUISHI. Nimeangalia wa Ukraine

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,349
4,807
Baadhi ya maneno yaliyopo katika wimbo wa taifa wa Ukraine.
" we will lay down soul and body for our freedom "
"We will never let anyone be master in our land"
"We will stand in a fierce bloody battle,...".

Nimeangalia wimbo wa Russia nao maudhui yake yanafanana na tabia zake.

Nimeangalia wa Israel na wenyewe sishangazwi na yanayoendelea. Wanasema " Then our hope, the two thousand year old hope will not be lost, to be a free people in our land. The land of Zion and Jerusalem "

Nimeangalia wa Marekani na Uingereza napo sijashangaa ni kwanini wapo vile na ni kwanini wameendelea sana, na ni kwanini huwa wanataka kutawala hadi nje ya mipaka yao/Dunia.

Nikarudi wimbo wetu wa Taifa/Tanzania. Kwa kweli sijashangazwa na tabia ya nchi yetu kama Taifa. Maudhui ya wimbo wetu yapo KIROHO ZAIDI/MAOMBI na hakika ndicho tunachokipata, nchi imebarikiwa hasa rasilimali za Ardhi nzuri, Misitu, wanyama, milima ya kipekee, mbuga za utalii, Bahari, maziwa, mito na vijito, mvua ya kutosha, hali ya hewa ya kila aina nk.

Tuliomba kudumisha umoja na hakika Mungu alitusikiliza, tukaomba amani na hakika tumepewa.
Binafsi nafikiri tulitakiwa kufanya zaidi ya hapo, inavyoonekana wimbo wetu mwanzo mwisho ni Maombi NA NDIO MAANA TUMEKUWA TUKISUBIRIA NEEMA YA MUNGU KATIKA KILA JAMBO. Tulitakiwa kutaja fahari zetu, Ushujaa wetu, miiko yetu, upendo, uzalendo , utayari wetu, tunu zetu na malengo yetu KISHA TUNAMUWEKA MUNGU MBELE.

JAMANI ANGALIENI NYIMBO ZA MATAIFA MBALIMBALI MTAGUNDUA KITU
 
Baadhi ya maneno yaliyopo katika wimbo wa taifa wa Ukraine.
" we will lay down soul and body for our freedom "
"We will never let anyone be master in our land"
"We will stand in a fierce bloody battle,...".

Nimeangalia wimbo wa Russia nao maudhui yake yanafanana na tabia zake.

Nimeangalia wa Israel na wenyewe sishangazwi na yanayoendelea. Wanasema " Then our hope, the two thousand year old hope will not be lost, to be a free people in our land. The land of Zion and Jerusalem "

Nimeangalia wa Marekani na Uingereza napo sijashangaa ni kwanini wapo vile na ni kwanini wameendelea sana, na ni kwanini huwa wanataka kutawala hadi nje ya mipaka yao/Dunia.

Nikarudi wimbo wetu wa Taifa/Tanzania. Kwa kweli sijashangazwa na tabia ya nchi yetu kama Taifa. Maudhui ya wimbo wetu yapo KIROHO ZAIDI/MAOMBI na hakika ndicho tunachokipata, nchi imebarikiwa hasa rasilimali za Ardhi nzuri, Misitu, wanyama, milima ya kipekee, mbuga za utalii, Bahari, maziwa, mito na vijito, mvua ya kutosha, hali ya hewa ya kila aina nk.
Tuliomba kudumisha umoja na hakika Mungu alitusikiliza, tukaomba amani na hakika tumepewa.
Binafsi nafikiri tulitakiwa kufanya zaidi ya hapo, inavyoonekana wimbo wetu mwanzo mwisho ni Maombi NA NDIO MAANA TUMEKUWA TUKISUBIRIA NEEMA YA MUNGU KATIKA KILA JAMBO. Tulitakiwa kutaja fahari zetu, Ushujaa wetu, miiko yetu, upendo, uzalendo , utayari wetu, tunu zetu na malengo yetu KISHA TUNAMUWEKA MUNGU MBELE .
JAMANI ANGALIENI NYIMBO ZA MATAIFA MBALIMBALI MTAGUNDUA KITU
Una point kubwa sana
 
Una point kubwa sana
Na kwa point hiyo ndio maana tunasalia kama kisiwa cha amani na kimbilio la wasaka amani wote duniani. Trust me watalii wakija Tz sio kwamba wanaangalia wanyama tu na vivutio vingine vya taifa, wanasaka peace of mind.

Tanzania sio sehemu ya bata kwa wageni hawa ila ni sehemu pekee duniani ambayo wanaweza saka amani ya moyo na wakaipata.

Ukitaka kuamini hilo jaribu kukutana na watalii wawili watatu na wadadisi kuhusu hilo.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
 
Haya ni mawazo finyu kutokana na kukosa exposure. Zipo nchi nyingi tu duniani zenye amani kuishinda Tanzania.
Halafu kwa utalii Africa hatupo hata Top five.
 
Nakumbuka kuna siku S.F wa UK wakiwa wamehitimu wale SAS niliona kidogo pass out yao. Wakati wa National anthem kuna commando machozi yanatoka unagundua commitment ya washikaji imejaa kwa kiasi gani.

Sisi bado neno uzalendo hatujawahi jua lina lenga nini hasa. Hasa kwa hawa wanasiasa..
 
Haya ni mawazo finyu kutokana na kukosa exposure. Zipo nchi nyingi tu duniani zenye amani kuishinda Tanzania.
Halafu kwa utalii Africa hatupo hata Top five.
Exposure? Ungejua aiseee usingetumia neno hilo kwenye comment yako.
 
Na kwa point hiyo ndio maana tunasalia kama kisiwa cha amani na kimbilio la wasaka amani wote duniani. Trust me watalii wakija Tz sio kwamba wanaangalia wanyama tu na vivutio vingine vya taifa, wanasaka peace of mind.

Tanzania sio sehemu ya bata kwa wageni hawa ila ni sehemu pekee duniani ambayo wanaweza saka amani ya moyo na wakaipata.

Ukitaka kuamini hilo jaribu kukutana na watalii wawili watatu na wadadisi kuhusu hilo.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Mbona Tanzania haipo sasa kwenye top five ya nchi zinazipokea watalii wengi Africa,tunazidiwa na Kenya ambako kuna mavurugu hatri

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom