Mauaji yaliyojaa utata

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
15,818
2,000
NYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA
Sehemu ya Ishirini na Mbili.
Benjamin hakutaka kutoka kule alipokuwa, alikuwa kimya, japokuwa katika bomba lile kulikuwa na joto kali na uchafu mwingi hasa moshi hakutaka kutoka, alibaki humohumo akiendelea kusubiri mpaka maofisa wale wa FBI waondoke ndiyo atoke ndani ya bomba lile.
Alimsikia rafiki yake, Harry alivyokuwa akiwaambia maofisa hao kwamba yeye hakuwepo, alikuwa amekwishaondoka na hakujua mahali alipokuwa. Maofisa wale walimtafuta, muda wote mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kule alipokuwa lakini hakutaka kutoka.
Walimtafuta bila mafanikio yoyote na kuamua kuondoka ndani ya nyumba hiyo. Hapo ndipo Benjamin alipoona ni muda muafaka kutoka ndani ya bomba lile, alianza kuangalia huku na kule, hakuwa akijiamini hata kidogo.
Hakukuwa a mtu nyumbani hapo, alikuwa peke yake, senhemu hiyo haikuonekana kuwa salama tena, kama maofisa wa FBI walikuja na kuondoka, aliamini kwamba wangerudi tena mahali hapo, alichokifanya ni kuanza kutoka.
Alitembea kwa mwendo wa tahadhali, alihofia kukamatwa, alitembea huku kichwani akiwa na kofia yake, hakuwa na usafiri, ingekuwa rahisi sana kama angefanikiwa kupata usafiri, magari yalikuwepo lakini hilo halikuwezekana.
Akachukua simu yake na kuanza kumpigia mpenzi wake, Vanessa, alitaka kuonana naye na kupanga ni kwa namna gani angeweza kuwa naye na mwisho wa siku kuondoka nchini hapo na kuelekea Urusi ambapo hakukuwa mbali sana.
Simu ikaanza kuita, alikuwa mvumilivu, wakati akipiga simu hiyo, alihakikisha anakuwa katika sehemu ambayo itakuwa vigumu kuonekana, alijibanza sehemu na watu wote waliokuwa wakipita pale alipokuwa, hakukuwa na aliyemgundua.
“Upo wapi?” aliuliza Benjamin mara baada ya simu kupokelewa.
“Nipo nyumbani!”
“Kuna usalama huko?” aliuliza.
“Nadhani. Hakuna mtu, nipo peke yangu!”
“Na FBI je?”
“Hawapo!”
“Hebu chungulia dirishani, angalia kwa umakini, kweli hawapo?” aliuliza Benjamin na Vanessa kufanya hivyo.
“Hakuna mtu!”
“Sawa! Nakuja!”
Japokuwa aliambiwa na msichana wake kwamba hakukuwa na maofisa wa FBI pale nyumbani alipokuwa lakini alishindwa kabisa kujiamini, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda na kuona kwamba kama angekwenda huko ilikuwa ni lazima kukamatwa.
Wakati anafikiria hayo, upande mwingine wa moyo wake ukamwambia kwamba hakukuwa na tatizo lolote lile, kama alitaka kwenda huko, aende na kila kitu kingekuwa vizuri.
Kutoka hapo alipokuwa mpaka alipokuwa akiishi Vanessa, katika nyumba ambayo aliamua kuipanga kwa muda haikuwa mbali sana, hakuchukua muda mrefu akawa amefika katika mtaa huo.
“Ni lazima tuondoke na kuelekea nchini Urusi, hapa Marekani si salama tena,” alijisemea Benjamin.
****
Wakati Benjamin akiwasiliana na Vanessa, vijana wa Bwana Seppy walikuwa wakifahamu kila kitu na walikuwa wakifuatilia neno moja baada ya jingine. Bado Benjamin alionekana kuwa mtu muhimu sana, walijua kwamba kama wasingefanikiwa kumpata mtu huyo na kumuua basi bosi wao angekuwa kwenye wakati mgumu sana.
Mawasiliano yale wakamuonyeshea Bwana Seppy ambaye alionekana kuwa na mawazo mno ya kukataliwa na msichana Stacie, alichoagiza ni kwamba Benjamin na mpenzi wake, Vivian watafutwe na kuuawa haraka iwezekanavyo.
“Hakuta tatizo mkuu! Tunawafuata hukohuko,” alisema Dracula na kisha kuwakusanya watu wake kuelekea kule ambapo Benjamin alitakiwa kuonana na mpenzi wake, Vanessa.
****
Benjamin alianza kupiga hatua za taratibu kuifuata nyumba aliyokuwemo Vanessa, hakujiamini kabisa na alijua fika kwamba inawezekana kuna sehemuu maofisa wa FBI walikuwa wamejificha.
Aliangalia huku na kule, hakuona mtu, hakujua kama maofisa hao walikuwa kwenye gari ambalo mbele hakukuwa na mtu, walikuwa kwa nyuma huku wakimfuatilia katika televisheni walizokuwa nazo na hata mazungumzo yake na Vanessa waliyasikia kwani tayari walikuwa wakimfuatilia msichana huyo tangu siku ile walipomruhusu kutoka katika kituo cha polisi.
“What should we do?” (Tufanye nini?) aliuliza jamaa mmoja.
“There is no time, let’s roll,” (Hakuna muda, twendeni)
Hicho ndicho walichokifanya, hawakutaka kusubiri mahali hapo, wakateremka huku wakiwa na bunduki zao mikononi. Wakati Benjamin akiendelea kupiga hatua kuelekea katika nyumba ile, ghafla akaliona gari likija kule alipokuwa, alionekana kuogopa, hakujua gari hilo lilikuwa la kina nani, alichokifanya ni kuanza kukimbia kuelekea katika nyumba ile.
Hao waliofika hawakuwa maofisa wa FBI, walikuwa ni vijana kutoka kwa Bwana Seppy, walifika hapo na kuhisi kwamba walikuwa peke yao, kitendo cha Benjamin kukimbia kuelekea ndani, wakaanza kumkimbiza huku wakiwa na bunduki.
Benjamin akaingia ndani, nao wakamfuata na kuingia ndani. Msichana Vanessa ambaye alikuwa ndani ya nyumba hiyo, akaanza kupiga kelele, watu wale hawakutaka kujali, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumkamata Benjamin na kisha kumkamata na Vanessa ambaye muda wote alikuwa akiomba msamaha tu kwamba aachwe.
“Mlidhani mtatusumbua miaka yote, kwisha habari yenu,” alisema Dracula huku akiachia tabasamu pana, uso wake ulionyesha jinsi gani alikuwa na furaha.
Wakawachukua na kuanza kutoka nje. Hawakujua kama maofisa wa FBI walikuwa hapo nje, kitendo cha kutoka tu, milio ya risasi ikaanza kusikika, walichokifanya ni kujificha pembezoni mwa nyumba hiyo.
“Who are they?” (Ni wakina nani?) aliuliza jamaa mmoja.
“I don’t know.” (Sifahamu)
“They are cops,” (Ni polisi) alisema Dracula.
“Who call them?” (Nani aliwapigia simu?)
“I don’t know,” (Sijui) alijibu Dracula.
Hakukuwa na muda wa kuulizana maswali mengi zaidi, kama walivyokuwa wakirushiwa risasi nao wakaanza kujibu mapigo. Yalikuwa ni mapigano makubwa, maganda ya risasi yalikuwa yakidondoka chini tu.
Sehemu hiyo ikabadilika na kuwa uwanja wa vita. Vijana wa Bwana Seppy walikuwa na silaha nzito hivyo kuionekana kuwa na kazi nyepesi kabisa. Kwanza walianza kulishambulia gari la maofisa wale bila tatizo lolote lile.
Kwa maofisa wale ilikuwa ni kazi ngumu kuwarushia risasi kwani watu hao walikuwa na Benjamin mtu ambaye walimtaka kwa udi na uvumba. Wasiwasi wao ndiyo uliosababisha kushambuliwa sana.
Benjamin ambaye alikuwa amekaa nyuma alipoona mashambulizi yanazidi na wote wamemsahau na kuwa bize na maofisa wale, akarudi ndani haraka sana, hakutaka kumshtua Vanessa kwani mahali alipokuwa ilikuwa vigumu sana.
Mmoja wa vijana wale alimuona Benjamin akikimbia lakini hawakuwa na muda wa kumkimbiza kwani bado mashambulizi kutoka kwa maofisa wa FBI yalikuwa yakiendelea kama kawaida.
“He is running....he is running...” (Anakimbia....anakimbia...) alisema jamaa huyo lakini hakuna aliyajali, wote walikuwa bize na mapambano.
****
Kulikuwa na watu wawili tu waliokuwa wakikizuzua kichwa cha Bwana Seppy kila siku, mtu wa kwanza kabisa alikuwa Benjamin na wa pili alikuwa msichana Stacie ambaye kwa kipindi kifupi tu aliuteka moyo wake na kuuendesha alivyotaka.
Hakutulia, kila wakati alionekana kuwa mtu mwenye mawazo mengi, alichanganyikiwa na wakati mwingine alihisi kama angeweza kupoteza maisha kutokana na jinsi alivyokuwa na mawazo lukuki kichwani mwake.
Kwa wakati huo alikuwa akisubiri habari njema kutoka kwa vijana wake aliowatuma kumteka Benjamin na kuja kumuua kwa mkono wake. Tangu vijana hao walipoondoka mpaka muda huo, hakuwa amepata taarifa yoyote ile kitu kilichomshangaza sana.
Dracula, mmoja wa vijana wake alikuwa mtu makini sana, kila alipomtuma, alikuwa mleta taarifa mzuri sana, hata kabla hajauliza kilichokuwa kimeendelea, tayari alimpa taarifa lakini siku hiyo, hali ilionekana kuwa tofauti kabisa, kila alipompigia simu Dracula, ilipatikana, ila haikupokelewa kitu kilichomtia wasiwasi mkubwa.
“Kuna nini? Mbona hapokei simu?” alijiuliza huku akikosa jibu kabisa.
Aliendelea kusubiri zaidi kwani kila alipopiga simu majibu yalikuwa yaleyale kwamba simu haikupokelewa.
Baada ya saa moja ndipo akaona kulikuwa na simu iliyoingia katika simu yake, moja kwa moja akayapeleka macho yake katika simu ile, namba aliyokutana nayo ilikuwa ni ya Dracula, harakaharaka akaipokea.
“Mmefikia wapi?” lilikuwa Swali lake la kwanza kabisa hata kabla ya salamu.”Ametukimbia...”
“Amewakimbia, yaani kirahisi tu?”
“Hapana mkuu! Tulikutana na tatizo, kulikuwa na maofisa wa FBI nao walikuja kumchukua, tukawa tunarushiana risasi, tumepoteza mwenzetu mmoja ila FBI wote wapo chini,” alisema Dracula.
“Kwa hiyo Benjamin mmemkosa?”
“Tulimpata, tulikuwa naye ila mapigano yalivyoanza, akapata nafasi ya kukimbia, ila tunaye mpenzi wake hapa,” alisema Benjamin.
“Nani? Vivian?”
“Ndiyo!”
“Mleteni huyohuyo.”
Hakutaka kusikiliza mazungumzo zaidi, alichokifanya ni kukata simu huku akiwa kwenye hasira kali, moyo wake ulikasirika, kitendo cha vijana wake kumpata Benjamin na kisha kuwatoroka kwake kilionekana kuwa kama uzembe mkubwa hata kama walikuwa wamezungukwa na maadui.
Kwa sababu Vivian alipatikana, kwake hakukuwa na tatizo, msichana huyo alikuwa muhimu kwani aliamini kama angekuwa naye basi ilikuwa ni lazima Benjamin ajipeleke kwani bila kufanya hivyo aliahidi kumuua Vivia ili kumtia hofu kijana huyo.
Wala haukupita muda mrefu, Vivian alikuwa mbele ya Bwana Seppy, kwanza akamwangalia msichana huyo, hakumpenda kwa sababu mpenzi wake alimsumbua sana. Akamwamuru Dracula amuweke kwenye kochi na yeye kuanza kuzungumza naye.
“Ben yupo wapi?” aliuliza mzee huyo.
“Sijui chochote kile,” alijibu Vivian huku akionekana kuwa na kiburi fulani.
“Unanificha?”
“Hapana! Waulize vijana wako, mimi sijui chochote kile,” alisema Vivian kwa ujasiri mkubwa.
Bwana Seppy hakutaka kuuliza swali jingine, alichokifanya ni kuamuru msichana huyo achukuliwe na kupelekwa katika chumba kimoja kilichokuwa ndani ya nyumba hiyo, chumba hicho kilikuwa na giza kubwa huku kukiwa na buibui wengi.
Kilikuwa chumba chenye mateso makali, watu wengi waliojifanya jeuri, walichukuliwa na kuingizwa ndani ya chumba hicho na kuachwa kwa siku kadhaa.
“Nisikilize Dracula,” alisema Bwana Seppy.
“Ndiyo mkuu!”
“Unamfahamu Stacie?”
“Huyu mrembo wa dunia tuliyekwenda kumuona siku ile?”
“Ndiyo!”
“Amefanyaje?”
“Ninaitaka roho yake!”
“Kwa nini?”
“Dracula! Tangu lini umeniuliza sababu? Nimekwambia ninaitaka roho yake, unaniuliza kwa nini! Unataka nikujibu nini?” aliuliza Bwana Seppy huku akionekana kuwa na hasira kubwa.
“Samahani mkuu! Tumuue kama kawaida au kivingine?”
“Kama kawaida!”
“Sawa.”
Huo ndiyo ulikuwa uamuzi aliokuwa ameufikia, hakutaka tena kuwa na huruma, alimpenda msichana Stacie, alimwambia lakini mwisho wa siku msichana huyo akamletea mapozi na kumkataa.
Hilo lilimkasirisha na ndiyo ilikuwa sababu ya kupanga mauaji, hakutaka kuumizwa moyoni mwake, kitendo cha kukataliwa kilimfanya kuwa na chuki kali dhidi ya Stacie, alijijua kwamba alikuwa na fedha nyingi hivyo kuwa na uhuru wa kuwa na msichana yeyote yule, sasa kwa nini msichana huyo amkatae?
Vijana wake wakaondoka mahali hapo, ilikuwa ni lazima kummaliza msichana Stacie kama walivyowamaliza watu wengine ambao walimkwaza Bwana Seppy ambaye alikuwa na utajiri mkubwa mno kipindi hicho.
Kabla ya yote, kitu cha kwanza kabisa ni kuanza kutafuta msichana huyo alikuwa sehemu gani.
Je, nini kitaendelea
 
dont trust any 1

JF-Expert Member
Jun 30, 2015
236
250

Kama isiishe vile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SAW_111

JF-Expert Member
Aug 18, 2017
211

Ubarikiwe sana kila inavyozidi kwenda mbele utamu unazidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
15,818
2,000
NYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA
Sehemu ya Ishirini na Tatu
Maisha yalibadilika kabisa, kilichokuwa mbele ya Stacie kilikuwa ni kutengeneza pesa tu. Mikataba iliendelea kumiminika, aliisaini tena kwa kiasi kikubwa cha fedha. Alijiona kuwa tajiri mkubwa hapo baadaye, watu walizidi kumpapatikia kwa sababu alikuwa msichana mrembo, mwenye mvuto wa ajabu ambapo kila mwanaume alitamani sana kuwa naye.
Hakuwa mwepesi, alitaka kutengeneza pesa kwanza kabla ya kuamua kuwa na mwanaume fulani. Mtu ambaye alikuwa akimfikiria kipindi hicho alikuwa mwanaume mmoja tu, huyu aliitwa Alan, mwanaume aliyewahi kuwa naye utotoni.
Siku zikaendelea kukatika, akasahau kama alitakiwa kurudi nchini Australia, kama walivyokuwa mastaa wengine, naye akatokomea nchini Marekani kwani ndipo kulipokuwa na ishu nyingi za pesa, kurudi nchini kwake isingewezekana tena.
Baada ya miezi kadhaa, akaitwa kwa ajili ya kuwa balozi wa watoto katika shirika la Umoja wa Mataifa kupitia UNICEF. Kazi kubwa ilikuwa ni kuzunguka duniani kote, kukutana na wanawake na watoto waliokuwa na matatizo kiafya na kuzungumza nao huku kiasi kikubwa cha dawa kikiwa kimeandaliwa.
Kichwa chake hakikumfikiria Bwana Seppy, hakujua ni maumivu makali kiasi gani aliyomuachia mzee huyo, aliendelea na maisha yake kama kawaida huku kila alipokwenda, watu walimheshimu mno.
“Kuna simu nilipigiwa,” alisema meneja wake, Robert.
“Na nani?”
“Mkurugenzi wa Google.”
“Amesemaje?”
“Anataka kuingia mkataba na wewe kwa ajili ya kufanya matangazo zaidi juu ya programu mpya wanayotarajia kuiweka katika simu zote zinazotumia android,” alijibu.
“Mmh! Wamesema wanaweza kutoa kama kiasi gani?”
“Sijajua ila si chini ya dola milioni hamsini,” alijibu meneja huyo, kiasi hicho kilikuwa ni zaidi ya shilingi bilioni mia moja.
“Sawa! Tukitoka huku, tutaonana nao tuwasikie, ila nina furaha sana,” alisema Stacie huku akiachia tabasamu pana.
Wakati huo walikuwa safarini kuelekea nchini Japan, alikuwa ameingia mkataba na kampuni ya kutengeneza matairi ya Yokohama, alitakiwa kwenda huko haraka iwezekanavyo, hakutaka kuchelewa kwani kiasi alichowekewa kilikuwa kikubwa mno, hivyo akafanya hivyo.
Ndani ya ndege, muda wote alikuwa mtu mwenye mawazo tele, hakuamini kama kile kilichokuwa kikiendelea kiliendelea katika maisha yake. Hawakuchukua muda mrefu ndege ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tokyo.
Hapo, kulikuwa na maofisa wa Yokohama ambao walitumwa kumpokea msichana huyo mrembo. Walipotoka tu nje ya uwanja huo, kundi kubwa la waandishi wa habari wakaanza kuwasogelea na kuwapiga picha.
Walifanya kile walichokuwa wameitiwa na baada ya siku mbili, safari ya kurudi nchini Marekani ikaanza. Kichwani mwake alikuwa akifikiria mkataba aliotaka kuingia nao na Kampuni ya Google. Wakati mwingine aliiona ndege hiyo ikichelewa kutua, alitamani kufika nchini Marekani na hatimaye asaini mkataba uliokuwa mbele yake.
Walichukua saa kumi na sita mpaka kufika nchini Marekani ambapo ndege ikatua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JFK uliokuwa jijini New York.
“Wamesema wapo jijini Las Vegas,” alisema Robert.
“Las Vegas?”
“Ndiyo!”
“Tunatakiwa kupumzika. Mpigie simu Alejandro na umwambie ajiandae, kesho tunakwenda huko,” alisema Stacie na Robert kufanya hivyo.
Usiku wa siku hiyo hakulala vizuri, kila alipogeuka, alizifikiria fedha ambazo aliahidiwa kupewa kama tu angesaini mkataba wa kuitangaza kampuni hiyo.
Asubuhi ilipofika, akaamka, tayari tiketi zilishakatwa na hivyo kuonana na Alejandro kisha kuanza safari ya kuelekea huko Nevada katika Jiji la Las Vegas.
Baada ya saa mbili, ndege ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa McCarran. Kitendo cha kufika katika jiji hilo tu kikampa uhakika wa kuondoka na mamilioni ya dola.
Walipofika nje, wakapanda ndani ya gari maalumu waliloandaliwa na kisha kuelekea katika Hoteli ya Vikings Hill. Wakapelekwa katika vyumba walivyotakiwa kulala. Siku hiyo akalala hotelini pasipo kujua kama kulikuwa na watu walitumwa kwa ajili ya kuichukua roho yake tu.
****
Kujua Stacie alikuwa wapi kipindi hicho halikuwa jambo kubwa, wakapata taarifa kwamba msichana huyo alikuwa safarini akielekea nchini Japan kwa ajili ya kufanya matangazo ya biashara na kuwekeana mkataba na Kampuni ya Yokohama iliyokuwa ikitengeneza matairi ya magari na ndege.
Hawakutaka kuelekea nchini humo kufanya mauaji, kwa kuwa kipindi hicho ilikuwa ni lazima afike nchini Marekani kwa ajili ya shughuli zake, walihakikisha wanamsubiri ili siku akiingia, kama kawaida wafanye kile walichoambiwa.
Walijiandaa kwa kila kilichokuwa kikiendelea, waliwaweka watu tayari kwa ajili ya kufuatilia ishu nzima ya Stacie na baada ya kuondoka nchini Japan siku mbili baadaye, walipewa taarifa nzima kwamba msichana huyo alitakiwa kwenda Las Vegas kwa kuwa Kampuni ya Google walitaka kufanya naye biashara kwa kusaini mkataba mnono ambao ungewatangaza.
“Alisema atafikia kwenye hoteli gani?’ aliuliza Dracula.
“Bado sijajua, ila nikijua tu, nitawapeni taarifa,” alisema mtoa taarifa.
Huo haukuwa mwisho, waliendelea kuzipokea taarifa hiyo na taarifa ya mwisho kabisa kuwafikia ilisema kwamba msichana huyo angefikia katika Hoteli ya Vikings Hill.
“Ni lazima twende huko kabla yake,” alisema Dracula.
“Hakuna tatizo.”
Baada ya saa mbili, Dracula na wenzake wawili walikuwa ndani ya ndege wakielekea jijini Las Vegas. Ilikuwa ni lazima kufanikisha kile walichoambiwa kwani bila kufanya hivyo, walijua kwamba kungekuwa na tatizo kubwa kwani Bwana Seppy hakutaka washindwe kwenye jambo lolote lile.
Walipofika, wakateremka kwenye ndege na moja kwa moja kuelekea nje ambapo wakakodi taksi iliyowapeleka mpaka katika hoteli hiyo ya kifahari ambapo ndani yake kulikuwa na Cassino iliyokuwa na michezo mingi ya kamari.
Hawakuacha kuwasiliana na kijana aliyekuwa akiwapa maelekezo, aliwaambia kwamba tayari msichana huyo aliingia jijini New York na hivyo kesho asubuhi angeanza safari ya kwenda Las Vegas ambapo tayari aliweka oda ya vyumba ndani ya hoteli hiyo.
“Tutafanikiwa, nilihisi kwamba tungekuwa na ugumu, ila inaonekana kuwa kazi nyepesi sana,” alisema Dracula.
“Kwa hiyo tumuue kama wale wengine?”
“Ndiyo! Hayo ni maelekezo niliyopewa na mzee.”
“Basi hakuna tatizo.
Walichokifanya ni kwenda kutembea, walizunguka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kula raha tu, walikuwa na fedha hivyo kila kitu walichokifanya kiligharimu fedha kitu ambacho wala hawakuwa na tatizo nacho kwani kama fedha, walikuwa nazo za kutosha tu.
Muda mwingi walikuwa wakiifikiria kazi hiyo, walitakiwa kupanga mipango kabambe, walijua kwamba kulikuwa na kamera ndani ya hoteli hiyo ila walitakiwa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha hawakamatwi na mtu yeyote yule.
Walizunguka kwa zaidi ya saa moja na nusu ndipo wakarudi hotelini ambapo baada ya kula, wakalala huku wakiisubiri siku inayofuatia kwa hamu kubwa.
Asubuhi ilipofika, wakaelekea katika mgahawa uliokuwa chini na kupata kifungua kinywa. Huko ndipo waliposikia taarifa za ujio wa msichana Stacie kwamba angefikia katika hoteli hiyo siku hiyo.
Watu kutoka sehemu mbalimbali walianza kufika ndani ya hoteli hiyo, kila mmoja alitaka kumuona msichana huyo, wengi walimuona katika sehemu mbalimbali, hasa kwenye televisheni na majarida, siku hiyo walitaka kumuona ana kwa ana.
“Kuna kitu jamani,” alisema kijana mmoja.
“Kitu gani.”
“Nina wazo. Nadhani tukitumia njia kama tuliyowaua watu huko nyuma tutashindwa kwani watu wanajua hivyo tunaweza kukamatwa,” alisema kijana huyo.
“Wewe unataka tufanye nini?”
“Ni lazima tumlevye huyu msichana.”
“Kivipi?”
“Kwa kutumia madawa ya usingizi. Tutumieni hata Phenometriphone, sumu yenye nguvu ambayo ikimpata mtu kwenye ngozi yake, ndani ya dakika arobaini, atalewa na kulala kwa usingizi mzito,” alisema kijana huyo.
“Baada ya hapo?” aliuliza Dracula.
“Ndipo tutamuua kwa kuingia chumbani kwake bila kipingamizi,” alisema kijana huyo.
Wazo alilolitoa liliungwa mkono na kila mtu, hakukuwa na mtu aliyekataa, kumlevya msichana huyo kabla ya kumuua lilionekana kuwa jambo jema ambalo kama wangelifanya, lingewapa urahisi, na wasingeweza kugundulika kwa urahisi.
Kitu walichokifanya ni kuanza kutafuta sumu hiyo. Waliuona ugumu uliokuwepo mbele yao, isingekuwa kazi nyepesi kuuziwa dawa hiyo pasipo kuwa na kibali kutoka kwa daktari ila kwa kuwa walikuwa na fedha, waliamini kwamba kila kitu kingekuwa chepesi.
Wakaondoka na kwenda kwenye duka la dawa, Dracula ndiye aliyekuwa mteja wa kununua sumu hiyo, alipofika kwenye duka moja la dawa, muuzaji alikataa kumuuzia, alichokifanya ni kutoa noti za dola, akaweka mezani dola elfu moja, harakaharaka akapewa sumu aliyoitaka na glavu.
“Ila usinichome,” alisema muuzaji huyo.
“Usijali.”
Dracula akaondoka na kurudi hotelini, huko akaonana na marafiki zake na kuwaambia kile kilichoendelea ambapo alikuwa na sumu hiyo iliyokuwa kwenye kikopo kidogo.
Aliwaambia kwamba walitakiwa kuwa na gravu, alikuja nazo hivyo kujiandaa huku yeye ndiye aliyetakiwa kumpaka msichana Stacie sumu ile.
“Tujadiliane, tutampaka vipi?” aliuliza Dracula.
“Kazi nyepesi sana, niachie mimi. Kitu cha msingi, yule kijana anayepokea mabegi watu wanaokuja hotelini, ile nafasi tunatakiwa kuwa nayo sisi,” alisema kijana aliyetoa wazo, kijana mwenye akili nyingi, huyu aliitwa Stephen, ila alipendwa kuitwa Steph.
Walichokifanya ni kusubiri, waliposikia kwamba msichana huyu alikuwa kwenye ndege, wakawasiliana na kijana aliyekuwa akihusika kupokea wageni na kumwambia kwamba walitaka kuzungumza naye, kijana yule pasipo kujua hatari iliyokuwepo, akawafuata chumbani, hukohuko wakamfunga kamba miguuni na mikononi huku wakimuwekea plasta kubwa mdomoni.
Steph akachukua mavazi ya kijana yule na kuyavaa kisha kutoka ndani ya chumba hicho. Kwa kuwa hoteli ilikuwa kubwa, tena ikiwa na wafanyakazi wengi ilikuwa kazi ngumu sana kugundua kwamba kijana huyo hakuwa mmoja wa wafanyakazi.
Tayari mkono wake wa kulia aliupaka sumu ile na aliyekuwa akimsubiri alikuwa Stacie tu. Baada ya dakika ishirini, kelele za watu zikaanza kusikika kuonyesha kwamba msichana huyo alikuwa akikaribia kuingia mahali hapo.
Harakaharaka Steph akapiga hatua, gari liliposimama, akaufungua mlango, watu wakawa wanampiga picha Stacie, alipoteremka tu, akampa mkono, wakasalimia tena kwa kushika kiuhakika kana kwamba walikuwa wakifahamiana, baada ya hapo, akachukua mabegi yake huku tayari akiwa amekwishampaka sumu ile Stacie.
“Tayari! Kwisha habari yake,” alisema Steph huku akiwa ameshika mabegi ya Stacie aliyekuwa akiwasalimiana na mashabiki zake, alipofika mapokezi, mizigo akaitelekeza, akapandisha juu mpaka katika chumba walichokuwepo wenzake na yeye kuingia.
“Imekuwaje?” aliuliza Dracula.
“Kila kitu tayari,” alijibu Steph huku akitoa tabasamu pana.
Je, nini kitaendelea?
 
Inazidi kuwa tamu madame

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Norshad

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
4,543
2,000
Huu upuuzi sasa unatoka kusoma sehemu ya nne unakutana na sehemu ya kumi na mbili mtutag na sisi aargh
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Similar Discussions

Top Bottom