DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,149
Msanii Mkongwe Rashidi Abdallah Mohamed Makwiro maarufu kama Chidi Benzi ameruhusiwa kurejea uraiani na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya wakishirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa walioshiriki kumpeleka katika Nyumba ya Matibabu kwa walioathirika na Madawa ya Kulevya (Sober House) ambapo mpaka sasa amekaa kwa miezi 10 pekee.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Chidi Benzi leo Auguts 22, baada ya kutoka amesema kuwa anafahamu kuwa amepita kwenye matatizo kwa kutumia Madawa ya Kulevya kutoka Mtaani lakini sasahivi yuko saw ana anarejea mtaani kwaajili ya kuendelea na kazi zake.
Chidi ameongeza kuwa anaomba ushirikiano kutoka kwa jamii kumpokea pamoja na kuzishukuru Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) pamoja na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA),
Aidha, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo amesema Chidi Benzi aliingia kwenye Madawa ya Kulevya, lakini serikali ilichukua hatua ya kumchukua yeye na vijana wengine kuwapatia tiba.
“Mpaka sasa watu waliotibiwa na serikali bure kutokana na kuathiriwa na dawa za kulevya wanafika zaidi ya milioni moja, akiwemo kijana mwenzetu Chidi Benzi ambaye tunamtoa kama mfano wa vijana waliopata tiba na serikali” Kamishna Lymo.