skfull
JF-Expert Member
- Dec 24, 2013
- 2,944
- 2,376
Kweli seppy ni jam hadi Kero,,, shukurani zangu zimfikie mtunzi na mwandishi wa story hii
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kapande kadogo lakini katam kweliNYEMO CHILONGANI
MAUAJI YALIYOJAA UTATA
Sehemu ya Ishirini na Nne.
Kwa kumwangalia, Stacie alionekana kuwa na furaha tele, hakuamini kama kulikuwa na watu waliokuwa wakimpenda kama ilivyokuwa, kila alipowaangalia, moyo wake ulikuwa na furaha tele.
Ni kweli alipendwa lakini watu waliojitokeza hotelini siku hiyo walikuwa wengi, ilimshangaza, alichokifanya baada ya kusaini vitabu vya mashabiki hao ni kuondoka na kuelekea ndani ya hoteli hiyo ambapo tayari kilikwishaandaliwa.
Alipokaa kitandani na kuanza kuvua nguo zake, akaanza kujisikia hali ya tofauti, mwili ulichoka na macho yake yakawa mazito, alishindwa kujua nini kiliendelea kwani dakika chache zilizopita wakati akiingia ndani ya hoteli hiyo, alijisikia vizuri kabisa, hakuwa na uchovu wowote ule.
Akapuuzia, akaendelea kuvua nguo zake lakini ghafla akajikuta akilala kitandani, usingizi mzito ukampitia, hakujua ni kitu gani kiliendelea baada ya hapo.
Dracula na vijana wake waliokuwa ndani ya kile chumba, harakaharaka wakatoka na kuelekea chumbani kule, walijua kwamba mpaka muda huo msichana Stacie alikuwa amelala kutokana na kuzidiwa sumu ile aliyopakwa.
Mlango haukuwa umefungwa, ulikuwa wazi walichokifanya ni kuufungua na kuingia ndani. Walimuona msichana huyo akiwa kitandani, hakuwa akijitambua, alizidiwa na sumu aliyokuwa amewekewa, hawakutaka kuchelewa, walichokifanya ni kuanza kumnyonga hapohapo kitandani, tena kwa kumziba pua na mdomo.
Wala hawakupata ushindani wowote ule, walifanikiwa kufanya walichotaka kukifanya kwa asilimia mia moja, baada ya kuhakikisha mapigo ya moyo yamesimama, wakachukua dawa za kulevya na bomba la sindano kisha kumchoma kwenye mkono wake na kuziweka alama za vidole vya Benjamin kwa kutumia plastini yenye unyevuunyevu kama kawaida, baada ya hapo wakaacha fedha walizotakiwa kuziacha na kisha kuondoka mahali hapo huku wakiwa wamefanikiwa.
Taarifa zilisikika usiku uleule baada ya mhudumu kufika ndani ya chumba hicho kwa ajili ya kumhudumia msichana huyo. Alipofika, akaanza kuugonga mlango ili afunguliwe lakini hakukuwa na sauti yoyote iliyosikika kutoka ndani, ukimya mkubwa ulikuwa umetawala.
Alichokifanya mhudumu huyo ni kwenda mapokezini ambapo huko akahitaji dada wa hapo apige simu katika chumba hicho ili azungumze na Stacie na kumwambia kwamba walitaka kumhudumia kwa kumpelekea chakula.
Simu ya ndani ya chumba alichokuwa Stacie ikaanza kuita, iliita na kuita lakini haikupokelewa kitu kilichoonekana kuwashangaza sana. Hawakutaka kukubali, wakampigia simu meneja wake, haraka sana, simu ikapokelewa.
“Upo na Stacie?” aliuliza dada wa mapokezi baada ya salamu.
“Hapana! Yupo chumbani kwake, kwa nini unauliza hivyo?” aliuliza Robert.
“Tunampigia simu, hapokei, unaweza kumpigia kwani tunahitaji kumuhudumia,” alisema msichana huyo.
“Hakuna tatizo, namfuata hukohuko chumbani,” alisema Robert na kukata simu.
Akatoka chumbani humo na kwenda chumbani kwa Stacie kwa lengo la kuzungumza naye kwamba wahudumu walitaka kumhudumia, alipoufikia mlango, akagonga hodi, kama ilivyokuwa kwa wahudumu, naye ilitokea vilevile, hakukuwa na sauti yoyote iliyosikika kutoka ndani.
“Stacie, fungua mlango,” alisema Robert lakini hakukuwa na majibu yoyote yale.
Alichokifanya ni kuufungua mlango na kuingia ndani, taa zilikuwa zikiwaka, alipigwa na mshtuko mkubwa baada ya kuangalia kitandani na macho yake kutua kwa msichana Stacie aliyekuwa amefariki kitandani pale.
Robert akachanganyikiwa, hakutaka kubaki chumbani humo, harakaharaka akatoka na kumpigia simu mbunifu wa mavazi, Alejandro na kumwambia kile kilichokuwa kimetokea.
“Unasemaje?” aliuliza Alejandro huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Ndiyo hivyo! Ngoja nikatoe taarifa...”
Robert alionekana kuchanganyikiwa, akatoka hapo na kwenda mapokezini huku akikimbia, hakuamini kile kilichokuwa kimetokea, kwake, ilionekana kama ndoto fulani hivi ambapo baada ya muda angeamka na kujikuta akiwa kitandani.
Alipofika mapokezi, kila mtu akabaki akimwangalia, hawakujua sababu iliyomfanya kutoka chumbani kwake na kuja mahali hapo huku akionekana kuwa kwenye presha kubwa.
“Kuna nini?”
“Ninataka kuongea na uongozi,” alisema Robert, watu waliokuwa pembeni, nao wakamsogelea, walitaka kujua kuna nini.
“Kuna nini kaka?”
Hapo ndipo Robert alipoanza kuhadithia kile alichokutana nacho chumbani kwa Stacie, hawakuamini, walichokifanya wahudumu hao ni kwenda huko chumbani kuhakikisha.
Kile walichoambiwa ndicho walichokutana nacho, msichana Stacie alikuwa kitandani, hakuwa akipumua, alikufa kwa kunyongwa lakini kwa jinsi ilivyoonekana, alionekana kama mtu aliyekuwa akijidunga madawa ya kulevya.
“Alikuwa akijidunga!” alisema mhudumu mmoja.
“Nashangaa! Sikuwahi kumuona akitumia madawa ya kulevya, si hivyo tu, hata kusikia tetesi sehemu yoyote ile,” alisema Robert.
“Sasa imekuwaje leo atumie madawa ya kulevya?”
“Hata mimi nashangaa.”
Kwa kuwa hawakuwa na maneno yoyote yale, walichokifanya ni kumpigia simu meneja wa hoteli hiyo ambaye alifika na kushuhudia kile kilichokuwa kimetokea, hawakumpigia huyo tu, bali waliwapigia simu polisi ambao kwa haraka sana wakafika mahali hapo.
Kile walichokiona hakikuwa kigeni katika macho yao, katika kipindi hicho, watu waliokufa hotelini walikufa kwa staili hiyohiyo na muuaji alikuwa mmoja tu, huyo alikuwa Benjamin.
Polisi hawakutaka mwili huo uguswe, bado walitakiwa kuuchunguza na kugundua kifo chake kilisababishwa na nini. Kitendo cha wahudumu kugundua kwamba msichana Stacie alikuwa amekufa chumbani humo, taarifa hizo wakaanza kuzisambaza katika mitandao ya kijamii.
Kila mtu aliyezipata, alishtuka, hawakuamini kile walichokiona kwamba msichana huyo alikuwa amekufa ndani ya chumba cha hoteli. Hawakutaka kujiuliza sana, wakajua kwamba muuaji alikuwa yuleyule aliyekuwa akitafutwa kila kona, Benjamin ambaye mpaka katika kipindi hicho hakukuwa na mtu aliyejua mahali alipokuwa.
“Ila kwa nini anaua jamaniiii?” aliuliza msichana mmoja huku akiwa ameishika simu yake, kile alichokiona, hakukiamini hata kidogo.
“Mimi mwenyewe nashangaa...halafu yeye anaua masupastaa wanaochipukia, kwa nini lakini?” alisema msichana mwingine.
Ndivyo ilivyokuwa. Taarifa zile ziliendelea kusambaa kila kona, watu walilia kwani hakukuwa na msichana ambaye waliamini kwamba angefanikiwa na kuwa na mashabiki wengi kama Stacie kutokana na mvuto aliokuwa nao.
Baada ya siku mbili mwili kuchunguzwa, taarifa zikasikika kwamba muuaji alikuwa yuleyule, mtu hatari aliyeogopwa, Benjamin ambapo kwa kipindi hicho, FBI waliamua kumtafuta kwa nguvu kubwa kwani pasipo kufanya hivyo, angeendelea kuua.
****
“David! Umefikia wapi?” aliuliza Benjamin kwenye simu.
“Kila kitu tayari, ushahidi upo wa kutosha, nikutumie kwenye barua pepe?’ aliuliza David.
“Sawa. Nitumie, hata kama kuna sauti nitumie pia,” alisema Benjamin.
“Hakuna tatizo. Ila unajua kwamba keshokutwa pia kuna mauaji yatafanyika?” aliuliza David.
“Hapana! Imekuwaje tena?”
“Huyu jamaa anataka kumuua mrembo wa dunia.”
“Unasemaje?”
“Ninavyoongea tayari kashatuma watu kwenda Las Vegas kwa ajili ya kufanikisha mpango huo,” alisema David.
“Kwa hiyo atatumia alama zangu za vidole?”
“Nadhani!”
Benjamin akabaki kimya kwa muda, hakutaka kuendelea na mazungumzo hayo, hapohapo akakata simu. Alikuwa kwenye mawazo mengi, hapo alipokuwa, haikuwa sehemu sahihi ya yeye kuwepo kwani alihisi kwamba muda wowote ule angekamatwa.
Alipanga kuondoka Boston na kuelekea New York, alitulia katika viti vya abiria katika kituo cha treni cha Smallville, alitaka kukimbilia huko kwani hapo Boston hakukuonekana kuwa salama katika maisha yake.
Japokuwa kulikuwa na watu wengi kituoni hapo lakini hakukuwa hata na mmoja aliyekuwa amemgundua. Aliendelea kubaki hapo mpaka treni ilipofika, haraka haraka akasimama na kwenda kuingia ndani, akatafuta kiti na kutulia.
Treni haikusimama sana kituoni hapo ikaanza safari ya kuelekea jijini New York.Humo ndani ya treni, hakutaka kumwangalia mtu yeyote yule, alikuwa kimya huku muda wote akiwa anaangalia chini na huku kofia ikiwa kichwani mwake.
Wakati akiwa katika hali hiyo, ghafla akashtukia kuona wanaume wawili waliokuwa wamevalia suti wamesimama mbele yake, harakaharaka akayainua macho yake na kuwaangalia watu hao, hawakuzungumza kitu, walibaki wakimwangalia, walipomuona kama mtu aliyechanganyikiwa, wakatoa beji zao zilizoonyesha kwamba walikuwa maofisa wa FBI.
“Upo chini ya ulinzi Benjamin. Hatutaki ulete fujo, tulia hivyohivyo,” alisema ofisa mmoja. Benjamin akatii. Wanaume hao wakakaa pembeni yake, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia.
****
FBI walikuwa na kazi kubwa mbele yao, hawakujua ni kwa jinsi gani wangeweza kumpata Benjamin ambaye alionekana kuwa mtu hatari sana, mtu ambaye hakutaka kuachwa akitanua mitaani hata mara moja.
Mauaji mengi yalitokea, yaliitetemesha Marekani na duniani kote kwa kuwa hao waliouawa walikuwa watu maarufu sana, watu waliofanikiwa kuiteka mioyo ya watu wengi duniani.
Walikesha usiku na mchana, walitegesha kamera sehemu nyingi hasa katika Jiji la Boston ambapo huko ndipo waliamini Benjamin alikuwepo katika kipindi hicho.
Watu waliopewa kazi ya kumfuatilia usiku na mchana hawakutakiwa kulala hata mara moja, walipewa agizo kwamba walitakiwa kuhakikisha kamera zinafanya kazi kila saa na kila kitu kitakachokuwa kikiendelea kiwe kinarekodiwa.
Hilo halikuwa tatizo, watu wa IT kutoka katika shirika hilo la kijasusi wakawa wanafanya kazi zao kama vile walivyoagizwa. Siku ziliendelea kukatika mpaka walipofanikiwa kumuona mtu aliyefanana na Benjamin akiingia katika Kituo cha Treni cha SmallVile.
Kitu cha kwanza walichokifanya ni kuivuta picha yake kwa karibu, hakuwa akionekana vizuri lakini kingine walichokifanya ni kuichukua picha yake nyingine ambayo alikuwa akionekana usoni na kisha kuilinganisha na picha ile.
Kila kitu kilifanana, kompyuta ikaandika neno 100 Match yaani ikimaanisha kwamba kila kitu kilikuwa sawa kati ya ile picha ya kichwa na picha ie ambayo ilipigwa katika kituo cha treni.
Walichokifanya ni kuwasiliana na maofisa wa FBI na kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea, harakaharaka wakawaagiza watu kuelekea huko huku wakiwatumia picha jinsi alivyovaa ili asiweze kuwapotea.
Hilo halikuwa na tatizo, wakaondoka kuelekea huko. Walikuwa maofisa wawili waliokuwa na bunduki, kama kawaida yao walivalia suti nyeusi. Walikwenda mpaka walipofika katika kituo hicho cha treni.
Haikuwa kwenda na kumuona bali walitakiwa kumtafuta na kuona alikuwa wapi, hivyo ndivyo walivyofanya, wakajifanya kuwa bize, waligawana kila mtu kuwa kivyake, kwa bahati nzuri wakati treni imefika, wakafanikiwa kumuona akisimama harakaharaka kuifuata treni, akaingia ndani na safari kuanza.
****
Muda wote msichana Vivian alikuwa akilia tu, hakuamini kama mwisho wa siku angekamatwa na kuingizwa ndani ya chumba hicho kilichokuwa na giza totoro. Alipiga kelele kuhitaji msaada wa kutolewa ndani ya chumba hicho lakini hakukuwa na mtu aliyejali, hata mtu wa kuufungua mlango huo hakutokea kabisa, bado chumba kilikuwa kimefungwa.
Saa zilisogea, alipoona amepiga sana kelele pasipo kupata msaada wowote ule akaamua kubaki kimya na kuona ni kitu gani ambacho kingeendelea. Baada ya kukaa ndani ya chumba hicho kwa saa kadhaa, mlango ukafungiliwa, mwanaume mmoja aliyekuwa na tochi akaingia na kummulika tochi usoni, mkononi alikuwa ameshika sahani iliyokuwa na chakula, alichokifanya ni kumrushia pale alipokuwa.
“Please let me out of here,” (Naomba unitoe hapa, tafadhali) alisema Vivian huku akilia.
“We can’t let you out of here, you have ten minutes to eat your damn food,” (hatuwezi kukutoa hapa, una dakika kumi za kula chakula chako) alisema mwanaume yule kisha kuufunga mlango.
Vivian akaanza kutambaa pale sakafuni, aliona wakati sahani ikisukumwa kule alipokuwa hivyo alitambaa kwa hisia kwamba sahani ilikuwa sehemu fulani. Hiyo ilimfanya kuwa rahisi sana kuipata sahani hiyo ambapo akaichukua na kuanza kula.
Alikuwa kwa kuwa alikuwa na njaa lakini hakuona radha yoyote ya chakula hicho, alitumia dakika saba tu kula, alipomaliza, akajisogeza pembeni na kuanza kulia tena.
Hakuona kama angeweza kutoka ndani ya chumba hicho, watu waliokuwa wamemkamata, hawakumtaka yeye, wao walimtaka Benjamin ambapo hakujua kama kulikuwa na kosa lolote alilolifanya mpenzi wake mpaka watu hao kumtafuta na kutaka kumuua kwa gharama zozote zile.
Alitamani kuwapigia simu watu wake wa karibu na kuwapa taarifa lakini alishindwa kufanya hivyo kwani kipindi alichokuwa ametekwa, hakuwa na simu yoyote ile, alifikishwa humo ndani akiwa mikono mitupu.
Alichokifanya ni kumuomba Mungu kwani hakukuwa na njia nyingine ambayo ingemuwezesha kutoka ndani ya chumba hicho kwani hao watu waliomkamata, walionekana kutokuwa na masihara hata kidogo.
Je, nini kitaendelea?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kazi nzuri sana madameNYEMO CHILONGANI

NYEMO CHILONGANIMadame S huyu nyemo hajatukumbuka tu sisi wasomaji wake jamani