ndetichia
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 27,769
- 6,585
Nimepita hapa maeneo ya ilala karibu na club ya wazee, kuna mauaji yametokea kwa watu wawili kupigwa risasi na muuaji nae kajiua,pia wawil wamejeruhiwa. Taarifa zaid ntawajuza.
Kwa mujibu wa shuhuda wa Clouds FM.
Mauaji hayo yamefanyika maeneo ya Ilala, kataja maeneo kwa jina lake maarufu (bahati mbaya sikudaka vizuri). Inadaiwa kuna gari ilikua inatoka ndani ya geti kutoka ikiwa na dereva mwanaume, abiria mwanamke mbele, na abiria wengine wawili wakiwa seat ya nyuma.
Pembeni hapo kulikua na jamaa kasimama. Inadaiwa alishushwa hapo dakika chache toka katika tax, walipotokeza abiria hao kupitia gari yao alitoa silaha yake na kupiga risasi gari akilenga zaidi abiria wa mbele pande zote kisha na nyuma. Baada ya kumaliza hapo muuaji huyo naye alijipiga risasi na kufariki hapo hapo.
Dereva na abiria wake wa mbele wamefariki dunia, huku abiria wa nyuma mmoja mama mtu mzima kajeruhiwa na risasi mgongoni na dada mwingine kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni.
hakuna kitu kibaya kama kula jasho la mtu au kumuibia muke yake ndio huwa inaishia hivyo..