Mauaji ya watu 3 Ilala - Dar

Mauaji ya watu 3 Ilala - Dar



Ilala4.jpg





Ilala1.jpg





Ilala2.jpg



ilala3.jpg


Mapema leo asubuhi milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatu wakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa limetokana na wivu wa kimapenzi.


Dereva mmoja wa tax kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza, alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu, ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye alikuwa ni muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu nyingine.

Kwa mujibu wake dereva huyo aliendelea kusimulia, alimpeleka jamaa mpaka aneo la tukio hilo kwenye nyumba iliyopo pembeni mwa Hotel mpya iitwayo MM.

Mara baada ya kufika hapo, jamaa alitoa sh. 5,000 na kumkabidhi dereva ila cha kushangaza ni kitendo cha jamaa huyo kutoa bastola wakati akiwa anaelekea kwenye geti la nyumba, aliendelea kusimulia dereva huyo.

Wakati jamaa anaelekea getini mlango ulifunguliwa na gari aina ya Toyota Surf ilitoka ikiwa na watu wanne ndani, mwanaume mmoja ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari mama mmoja na wadada wawili.

Jamaa akiwa na bastola alianza kuwashambulia watu waliokuwa ndani ya gari hilo na kumpiga risasi dereva na mdada mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Carol, hii ni kwa mujibu wa dereva huyo na mara baada ya kuona hivyo hivyo ikabidi akimbie.

Vyanzo vingine vinaeleza kuwa katika tukio hilo jamaa pia limpiga risasi ya mgongoni mama wa mwanamke aliyemuua na pia alimpiga msichana mwingine risasi ya mguu.

Mtuhumiwa na dereva aliyekuwa akiendesha gari walifariki palepale huku msichana mmoja akielezwa kufariki akiwa njiani kuelekea hospitali.

Bado haijafahamika moja kwa moja chanzo cha mauwaji hayo licha ya watu wengi ambao nilipata bahati ya kuongea nao wakilihusisha tukio hilo na mambo ya kimapenzi.
 
Duh, poleni sana ndugu na jamaaa, ila kwa maeleo yako inamaana hao kwenye picha ni wengine tena sio akina dada uliowaeleza hapo?
 
Hataree! Mi hisia zangu zinanifananishia na UFOOSARO
 
mbona wapo wawili nje wakati walikuwa ndani ya gari?
 
Huyo ni dereva mwanaume, na muuaji.

Katika hao wadada mmoja ndo kafariki, na wawili wamejeruhiwa.
 
Huyu jamaa alikuwa na shabaha kweli sio kama Mushi, maana amemuua msichana, mume aliyemuibia na yeye mwenyewe tena zote za kichwa.
Anaitwa Gabriery Munisi!
 
jamani msisikie hii habari nimeishuhudia kwaq macho imetisha sana nilijua ni yale ya westgate.

mimi mnataka kujua sababu ni nini hasa
 
Sijaelewa vizuri bado. Nitakuja nisome tena kwa nukta ngoja niende kwa kapuya. Pasco ametueleza yule binti ana matatizo ya akili kitu ambacho kinanifanya na muheshimiwa niwe na hisiya naye, naye ni yule yule
 
Huyo ni dereva mwanaume, na muuaji.

Katika hao wadada mmoja ndo kafariki, na wawili wamejeruhiwa.
muuaji ni huyo kaka mwenye shati jeupe la strips na yy sijui alipata wapi ujasiri alijipiga risasi ya chini ya kidevu

aisee yaani alikuwa amedhamiria kabisa kuua
 
A lady who have built his banking career for 9 good years...anakuja kuuawa kinyama kiasi hiki???RIP my co-worker and friend......RIP Alpha Alfred
mkuu hebu tufumbue vizuri, ameuawa na kaka yake au na mchumba wake?
 
muuaji ni huyo kaka mwenye shati jeupe la strips na yy sijui alipata wapi ujasiri alijipiga risasi ya chini ya kidevu

aisee yaani alikuwa amedhamiria kabisa kuua
Jamaa -------- sana huyu, sasa kwa nini amemuua dereva asiye na hatia
 
mkuu hebu tufumbue vizuri, ameuawa na kaka yake au na mchumba wake?

ameuawa na shemeji yake(mchumba wa dada yake)...huyo binti aliyejeruhiwa ndiye mchumba wa huyo muuaji.
 
Back
Top Bottom