Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,899
- 4,623
Wakati rais akiwahutubia wanadiplomasia kuhusu kusikitishwa kwake na yali yaliyotokea huko Arusha, Rpc wa Arusha yeye pamoja na wapambe wake alikuwa akitoa tamko la kuunga mkono hatua yake ya kutawanya maandamano yaliyopelekea hayo yanayomsikitisha JK.Kikwete ni mnafiki mkubwa sana, kuonyesha kusikitika ni kutaka kuwaaminisha watanzania kwamba yeye hausiki
na kutaka kuwapoza wananchi ambao tayari wameonyesha kutokuwa na imani na CCM, Kweli bado viongozi wanawaona watanzania ni wajinga.
Sasa hapa unaweza pata picha ya ni nani rais wa Tz. Maana yule tunaedhani ndio rais anatoa malalamishi kwa watendaji wake ambayo wao wanayapuuza na kusisitiza wako sahihi.
No wonder kuna mtu mmoja mwenye kuheshimika hapa nchini aliwahitoa kauli kwamba Tanzania kwa sasa hatuna rais ila tuna mtu aliyeshikilia hiyo nafasi hadi hapo atakapopatikana rais.
.