Matumizi ya Magufuli, tuyajadili

Matumizi ya Magufuli, tuyajadili

Mimi kiongozi akiwa anaongea anafoka huwa namtoa thamani sana
najiuliza hajawahi kumuona Clinton au Obama akiongea?
hafuatilii rekodi zao?
au anafikiri hata USA hakuna ufisadi?
Vile ndio alivyo MAGUFULI mzee ulikuwa masomo ni ulaya nini ndio umerudi
 
Ktk vitu vilivyonifanya nimshushe point Magufuli ni tabia yake yakulalama hovyo!!!

Ameshika nafasi sasa aonyeshe anaweza kuliko kuendelea kupiga kelele tumefikishwa hapa na watubwachache ambao hatutajii na hachukui hatua dhidi yao...

Visionary leader halalamiki!! Huchukua matatizo kama changamoto na kuzifanyia kazi...

Ktk vitu ambavyo Magufuli hana na vitamgharimu ni kukosa intelligence...

Viongozi wanahitaji kuwa na maarifa sana ili kuwaongoza watu wao waende wapi...

Lkn huyu bwana ameonesha zaidi uwezo Wa kusimamia kuliko kuongoza!!!

Huu mfumo Wa one man army ni mbaya na hauna tija ktk dunia hii ya Leo...

Hapo mwanzo nimesema tunahitaji fundamental changes. Na sio hizi blah blah zake.

Fundamental change ni kubadili mfumo ambao umetufikisha hapa.

Kama yeye haoni au washauri wake, basi atamaliza miaka 10 hajafanya lolote zaidi ya kushtukiza na kufukuza kama anavyofanya sasa.

Mabadiliko makubwa yanaanza na kuwa na katiba imara inayombana kila kiongozi katika njia inayotakiwa aende.
 
Barabara ya Dar es salaam Chalinze itagharimu zaidi ya USD million 500.
 
Anasema Darisaramu ndiyo kira kitu, sasa kwa sababu wao (wakuu) wanakaa darisaramu ndiyo maana wameona waujenge mji wao.

The Boss hayo mapato yanayopatikana ni kwa ajili ya kuijenga darisaramu yao wanayoishi.

Jamaa still ana upeo mdogo sana, nilimshangaa alivyokuwa anasifia kujenga daraja la coco beach to aghakhan[emoji15] [emoji15] [emoji15].

Barabara sita Chalinze-Dar, yaani barabara kuu inayoisambaa from Dar to mikoa mingi TZ na nje ya nchi unajisifu leo kwa three lane. Magu acha utani bana.
Raila ni best yako, nenda hapo Kenya tu ukaangalie ile Thika highway kisha kurudi hapa kichwa kitafunguka coz nikikwambia uende SA utasema huko ni kwa wazungu.

Hatujawahi kuwa na vipaumbele Tanzania.

Atleast hata Nyerere alianzisha viwanda wakati ule wakati mambo yalikuwa tight.
 
Kwa maelezo ya jana ina maana waziri wa miundu mbinu ni yeye
aliepo hana mamlaka ya kupanga chochote

Unajua mkuu wakati watu tuliposema Magufuli hafai kuwa rais watu hawakutuelewa tunamaanisha nini....

Rais ni kiongozi si mtawala!! Magufuli ni mtawala si kiongozi...

Dunia ya Leo nchi zetu hizi zinahitaji viongozi smart wakutuvusha na sio wafokaji na wenye vitisho!!!

Akina Mugabe na jeuri zao Leo wanaomba omba hovyo dola bilioni mbili ziwaokoe ilhali Zimbabwe ilikua juu na strong kiuchumi hapo awali...
 
Napata shida sana kila nikimtafakari Magu,
Hakika haelewi nini anakitaka na nini hataki
 
Ni Kama mpira vile, kila mtu ni MESSI akiwa nje, Kumbe wengine hata dana dana mbili hawawezi, wengine hata mambo ya familia zetu tu ni shida kuziendesha, ila ndio wa kwanza kukosoa.
 
Daraja la kigamboni bilioni 200
daraja la furahisha mwanza bilioni 200 (nakaribisha masahisho)
daraja la coco beach-bilioni 200 zimetengwa
barabara ya dar-chalinze-zaidi ya trilioni 1.3(dollar milioni 500)
mabasi yaendayo kasi -zaidi ya bilioni 200
flyover ya ubungo bilioni 100

Iwapo serikali ingeamua kujenga treni za umeme
badala ya mabasi yaendayo kasi ingetumia dollar milion 430
kwa km 32...yaani karibu Dar yote ingekuwa unapanda treni dakika 10
uko popote pale hata kigamboni treni ingefika kupitia Mbagala..
hii ni link ya Ethiopia inaelezea gharama za treni hizo na tayari wenzetu wanatumia..
Ethiopia gets first sub-Saharan Africa metro - CNN.com

na kama hizo bilioni zingetumika kujenga vyuo vikuu
UDOM gharama zake ilikuwa kiasi cha bilioni 25....
Naunga mkono hoja!
Ujue shida imemfunga Mkuu wa nchi!
Tumetatizwa sana na barabara kiasi tunaona njia pekee ya kutatua kero za wananchi ni barabara!
JPM anapaswa kufungua akili zaidi na kuitazama hii changamoto kwa jicho la ziada!
Matumizi ya reli pia yataondoa Malori barabarani ambao nao wanachangia foleni, uharibifu wa barabara na ajali wakati mwingine!
 
Hatujawahi kuwa na vipaumbele Tanzania.

Atleast hata Nyerere alianzisha viwanda wakati ule wakati mambo yalikuwa tight.

Nilitegemea Jana tuelezwe wamejipanga vipi... Watafanya nini....lini...wapi na kwa njia zipi!!!

Nilitegemea magu aseme vision yangu ni hiii...

Asijidanganye kwa kufoka na kushtukiza akifikiri urais ni uwaziri! Atachoka mwenyewe maana kila kitu kinamhusu!!!

Bado najiuliza hiyo kasi isemwayo ni katika nn?

Bahati mbaya nchini kwetu hatunaga mijadala ya wazi hasa kwa viongozi wetu...

Ingekuwepo tungewaita akina JK watueleze ni vipi ARI MYA.... NGUVU MPYA & KASI MPYA vilikwama...

Coz utafoka na kufukuza watu kazi mpaka lini?
 
Hatujawahi kuwa na vipaumbele Tanzania.

Atleast hata Nyerere alianzisha viwanda wakati ule wakati mambo yalikuwa tight.
Vipaumbele tumekuwa navyo vya kutosha ktk kipindi cha miaka 15 iliyopita.
Kuuwa tembo na kupandisha twiga ndege ni vipaumbele hivyo.

Madawa ya kulevya.

Ufisadi wa kutisha.
Ni vipaumbele vyetu hivyo ndiyo maana hata magu sasa hivi akili yake imeshakuwa dormant vipaumbele anajua ni metro coach wakati reli na viwanda vinaangamia
 
Napata shida sana kila nikimtafakari Magu,
Hakika haelewi nini anakitaka na nini hataki

Kama hadi gazeti tu linawafanya waingie kazini
ni kama vile hawana 'master plan'
so wanaenda na matukio.....

Hawakuwa na masterplan na masuala ya mafuta kabisa nahisi
 
Jamani Rais ana wa shauri wengi sana wenye utaalam kwenye issue iliyopo mezani kwa wakati huo tusijifanye wajuaji sana hapa. Hivi unapoweka train morogoro road alafu sehemu zingine za mji hamna ndio utakuwa umesolve tatizo gani, kwa mji kama dar es salaam tatizo ni msongamano wa magari sio msongamano wa abiria na hicho ndio tunachokishudia sasa hivi mchana daladala nyingi zimepaki au zinatembea hazina watu kabisa lakini foleni Tazara, ubungo chang'ombe ,Magomeni na Morocco ni kubwa sana,nafikiri mngeanza kusoma problem statement na implication of doing nothing kwenye proposal ya hii project ndio mje hapa msifanye watu hawana akili. Nyinyi mnafikiri gharama ni kujenga au kununua train tu, Je gharama za uendeshaji na matengenezo kama wangeamua kujenga mifumo ya reli mnazijua, ACHENI BWANA HIZO ON AIR CALCULATION ZENU ZA AJABU AJABU
 
Kama hadi gazeti tu linawafanya waingie kazini
ni kama vile hawana 'master plan'
so wanaenda na matukio.....

Hawakuwa na masterplan na masuala ya mafuta kabisa nahisi
Gazeti lilitoa taarifa ambayo wao tayari walikua nayo mezani. Sio kwamba walifanyia kazi taarifa za Gazeti.
 
Tubadili mfumo then huo mfumo usimamiwe na watu gani?.

Kwa viongozi walio kuwa wanagombea aliekuwa na dira na muelekeo ni mama Ana tu.Lakini hawa wote walio baki hasa mshindi na mshindwa ni walewale.

Tukibadili mfumo usimamiwe na watu gani?.

Magufuli?.
Lowasa?.

Heri magufuli mara mia nane kuliko Lowasa.Hii mitandao yao ndio imetufikisha hapa hasa uyo jeikei na mwenzake Elowasa.
 
Kuna hili daraja la Coco beach mpaka Agha Khan. Do we really need this...now!? Hii ni anasa. Bilioni 200 si nafuu akajenge barabara za ndani ndani huko zisaidie wananchi masikini (Bonyokwa - Segerea; Mbezi to Segerea)
 
Hawa wanaochangia hii thread ni watanzania au wanyarwanda? Too negative
Sasa mkuu unataka wachangie nini mambo yenyewe ni kama unavyoyaona? Mtu gani akiamka tu anatamka yeye bila kufuata utaratibu? Serikali duniani zingekuwa zinaendeshwa namna hii haki ya nani kusingekalika! Ajirekebishe bwana.
 
Nilitegemea Jana tuelezwe wamejipanga vipi... Watafanya nini....lini...wapi na kwa njia zipi!!!

Nilitegemea magu aseme vision yangu ni hiii...

Asijidanganye kwa kufoka na kushtukiza akifikiri urais ni uwaziri! Atachoka mwenyewe maana kila kitu kinamhusu!!!

Bado najiuliza hiyo kasi isemwayo ni katika nn?

Bahati mbaya nchini kwetu hatunaga mijadala ya wazi hasa kwa viongozi wetu...

Ingekuwepo tungewaita akina JK watueleze ni vipi ARI MYA.... NGUVU MPYA & KASI MPYA vilikwama...

Coz utafoka na kufukuza watu kazi mpaka lini?

Uzuri sasa hivi kila mtu anaimba wimbo wa Hapa Kazi Tu bila kufungua macho na kujadili nini kinatakiwa kufanyika.

Viongozi wetu wote hawajui Tanzania inataka nini?
 
Back
Top Bottom