Matumizi ya fedha za kigeni nchini yapigwe marufuku

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,067
Nilwahi kuuliza hapa iweje nchi kama Thailand wadhibiti matumizi ya dollar lakini hapa mambo ni holela,jana nimepata jibu toka kwa bwana Zitto kuwa kutodhibiti fedha za kigeni kunachangia kuporomosha uchumi.

Hivi watu wa Wizara ya fedha na BOT hawalijui hilo?

Watu wa uchumi tusaidieni kutuelemisha katika hili.
 
Watadhibiti fedha vipi fedha za kigeni wakati wao ndio wanahodhi maduka mengi ya kubadilisha fedha na ndio wanaonunua fedha za kigeni kwa wingi na kuzipeleka nje.

Hakuna mahala popote utakapoweza kuenda dukani na ukajichukulia fedha kiasi unachotaka.

Siku moja nilikuenda africa kusini na nilikuwa na nataka kubadilisha dola ili nipate randi nilizunguka MALL nzima mara waniambie subiri mara ngoja mara hatuna badala ya kukasirika niliona wale watu walikuwa na nidhamu sana kuhusu kulinda fedha yao hapa kila kitu ovyo.

Shamba la bibi hawatadhibiti hao ndio mwanya wao wakuzichota
 
Nilwahi kuuliza hapa iweje nchi kama Thailand wadhibiti matumizi ya dollar lakini hapa mambo ni holela,jana nimepata jibu toka kwa bw Zito kuwa kutodhibiti fedha za kigeni kunachangia kuporomosha uchumi.
Hivi watu wa wizara ya fedha na BOT hawalijui hilo?
Watu wa uchumi tusaidieni kutuelemisha katika hili.

kuna ambaye amesoma uchumi halijui hilo? kuna tofauti kati ya kujua kitu na kutekeleza unachokijua. nina uhakika kabisa wanalijua hilo, tatizo ni kwamba wanashindwa kutekeleza labda sababu ya external forces
 
Fedha za kigeni zinaathiri Uchumi kwani zinachangia sarafu yetu kushuka.

Pia sarafu yetu ikishuka na kwa kuwa uchumi wetu ni import oriented Economy basi gharama za kuagiza bidhaa nje ni kubwa ambazo mwananchi ndiye anabeba mzigo. Pia huathiri urari wa biashara

Bidhaa zinazozalishwa kutokana na malighafi ya nje huongezeka bei, huku pato la mwananchi likiwa lile lile.

Maisha yanazidi kuwa magumu kwa mtanzania hasa ukizingatia zaidi serikali yetu imeweka loose Tarriff Policy
 
Wana JF;

Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikiona wenye nyumba au ofisi/warehouses za kupangisha wanawadai wateja wao kulipa kwa fedha za kigeni (hasa US Dollar)

Mimi nauliza kitendo hiki kina athari gani katika mzunguko wa fedha na uchumi wa nchi kwa ujumla? Ni kwa nin basi BoT wasiidhinishe matumizi ya US Dollar katika mzunguko wa fedha wa kia siku i.e. kwenye biashara za rejareja, manunuzi na mauzo ya vifaa vya mtumiaji n.k?

Kama si sahihi/au kama kitendo hiki kinaathiri uchumi au kinamuathiri mtumiaji BoT wanapaswa wachukue hatua gani kudhibiti atahri zaidi zisitokee (kisheria)?

Nawasilisha huku nikiwatakieni Heri ya Krismas na Mwaka mpya wenye mafanikio!
Asante
 
I think hapa wengi huwa wanaqoute in US Dollars lakini unalipa in Tshs kulingana na value ya dollar kwa siku hiyo.

Pesa yetu inafluctuate sana... na ni rahisi mtu akiweka bei in US $ ambayo ni more stable hususan kwa watu wanaoagiza bidhaa kutoka nje.
 
Wana JF;

Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikiona wenye nyumba au ofisi/warehouses za kupangisha wanawadai wateja wao kulipa kwa fedha za kigeni (hasa US Dollar)

Mimi nauliza kitendo hiki kina athari gani katika mzunguko wa fedha na uchumi wa nchi kwa ujumla? Ni kwa nin basi BoT wasiidhinishe matumizi ya US Dollar katika mzunguko wa fedha wa kia siku i.e. kwenye biashara za rejareja, manunuzi na mauzo ya vifaa vya mtumiaji n.k?

Kama si sahihi/au kama kitendo hiki kinaathiri uchumi au kinamuathiri mtumiaji BoT wanapaswa wachukue hatua gani kudhibiti atahri zaidi zisitokee (kisheria)?

Nawasilisha huku nikiwatakieni Heri ya Krismas na Mwaka mpya wenye mafanikio!
Asante

Kuna thread Bubu Ataka Kusema aliianzisha kuhusu dollarization in Tanzania itafute kuanzia nyumba mpaka vocha za simu tukazitaja athari zake tunawashukuru vocha wameondoa in dollar bado kodi za nyumba maana hii ni sumu katika uchumi wetu na ndio moja ya sababu kuu shillingi yetu inaporomoka kila siku.
 
You mean hata hizi nyumba wanaagiza kutoka nje in terms of dollars? Pls try to be sincere to yourself. Sote tunajua kilochopo hapa ni ulafi wa hali juu na kutokujali watu wengine baada ya wenye opportunity kuzitumia na kujenga nyumba na kuzipangisha! Lengo la mabepari ni kunyonya and squeeze dry the poor! In most cases there is no justification ya nyumba iliyopo sinza hata mwenge kupangishwa kwa mswahili in terms of dollars!
 
hapana kaka nimesema hususan kwa watu wanaoagiza bidhaa kutoka nje...... siungi mkono kwamba ni vema kufanya hivyo natafuta justification ya wao kufanya hivyo.
 
tatizo unakuta hata machinga anayetembeza vitoto vya mbwa maeneo ya victoria anaquote bei in dollars! Huko mbele itabidi BoT wafanye kama Zimbabwe, kwani inaonekana dollar ni nzuri hata kwa mvuto kwa vingozi wetu ndo maana wako kimya pamoja na malalamiko yote!
 
Wana JF;

Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikiona wenye nyumba au ofisi/warehouses za kupangisha wanawadai wateja wao kulipa kwa fedha za kigeni (hasa US Dollar)

Mimi nauliza kitendo hiki kina athari gani katika mzunguko wa fedha na uchumi wa nchi kwa ujumla? Ni kwa nin basi BoT wasiidhinishe matumizi ya US Dollar katika mzunguko wa fedha wa kia siku i.e. kwenye biashara za rejareja, manunuzi na mauzo ya vifaa vya mtumiaji n.k?

Kama si sahihi/au kama kitendo hiki kinaathiri uchumi au kinamuathiri mtumiaji BoT wanapaswa wachukue hatua gani kudhibiti atahri zaidi zisitokee (kisheria)?

Nawasilisha huku nikiwatakieni Heri ya Krismas na Mwaka mpya wenye mafanikio!
Asante

Kama huna viwanda na asilimia 90 ya bidhaa madukani una-import kwa dola unategemea nini?
 
Hoja hii ya matumizi ya fedha za kigeni kwa biashara hapa nchini ipewe nguvu ya kisheria na wanaoendelea kufanya hivyo wakamatwe vinginevyo fedha yetu haiwezi kupata thamani.

Pia tour operators wengi wanaficha fedha nje ya nchi na wageni wanakuja na vocha tu hapa nchini. Wizara ya fedha na benki kuu hawatutendei haki katika maswala haya. Au wadau mnasemaje.
 
Hiyo ni sawa kabisa,uchumi wetu hautakuwa kama hatutaweka udhibiti katika fedha za kigeni.
Angalia nchi kama South Africa ambao wanatuzidi kiuchumi lakini bado ni kosa la jinai kumiliki feha za kigeni. Tuwe wakweli bila kuwa na mikakati ya dhati katika uchumi wetu tutaendelea kuwa ombaomba yaani vasco da gama.
 
1.Staafisha Gavana wa benki kuu kwani ni mzigo.
2.Piga marufuku matumizi ya sarafu ya dollar ya Marekani kwa matumizi ndani ya nchi.
3.Wasafiri wote nje ya nchi waonyeshe passport zenye viza na ticket wanaponunua fedha za kigeni kutoka benki au bureau de change kuthibitisha kuwa wanazihitaji kwa matumizi nje ya nchi.
4.Wakaguzi wa BOT wahakikishe kuwa bureau de change zote zinafuata sheria na zinazokiuka zifutiwe leseni.
5.Wananchi wawe wazalendo kwa kutoa taarifa BOT wanapoona mtu yeyote anauza bidhaa kwa fedha za kigeni hapa nchini.
6.BOT watoe namba ya simu ya bure(toll
free hotline) kwa wananchi kutoa taarifa.
7.Hatua hizi zitapunguza kabisa mahitaji ya fedha za kigeni hivyo zitapungua thamani na shilingi itapata nguvu. Majirani zetu wamefaulu kwa nini tushindwe?

Naamini sheria zipo lakini BOT ni jipu lingine linalohitaji kutumbuliwa.
 
Ubarikiwe mkuu....hakika wewe ni mzalendo wa kweli........
Matatizo ya taifa hili mzizi wake ni uzalendo miongoni mwa wananchi.....mambo yote uliyoyaoanisha hapo yanahitaji uzalendo wa kiwango cha juu.......kila mwananchi anapaswa kuipenda nchi yake kwa moyo wake wote na akili yake yote.....hapo tutakapoanza safari ya kuelekea utawala bora.......na uchumi wetu.......
Ni TANZANIA PEKEE AMBAPO MWANANCHI ANASHIRIKIANA NA MGENI KUKWEPA KODI.........ALAFU MWANANCHI HUYO HUYO ANALALAMIKIA KUHUSU UPUNGUFU WA MADAWA HOSPITALINI......
 
1.Staafisha Gavana wa benki kuu kwani ni mzigo.
2.Piga marufuku matumizi ya sarafu ya dollar ya Marekani kwa matumizi ndani ya nchi.
3.Wasafiri wote nje ya nchi waonyeshe passport zenye viza na ticket wanaponunua fedha za kigeni kutoka benki au bureau de change kuthibitisha kuwa wanazihitaji kwa matumizi nje ya nchi.
4.Wakaguzi wa BOT wahakikishe kuwa bureau de change zote zinafuata sheria na zinazokiuka zifutiwe leseni.
5.Wananchi wawe wazalendo kwa kutoa taarifa BOT wanapoona mtu yeyote anauza bidhaa kwa fedha za kigeni hapa nchini.
6.BOT watoe namba ya simu ya bure(toll
free hotline) kwa wananchi kutoa taarifa.
7.Hatua hizi zitapunguza kabisa mahitaji ya fedha za kigeni hivyo zitapungua thamani na shilingi itapata nguvu. Majirani zetu wamefaulu kwa nini tushindwe?

Naamini sheria zipo lakini BOT ni jipu lingine linalohitaji kutumbuliwa.
unajifanya hujui kuwa BOT imeajiri vitoto vya wakubwa halafu baba zao ndio wamiliki wa bureau de change unafikiri wanaweza kufunga bureau de change za babazao ziliwasomesha
 
Mawazo zuri sana, kuna kila haja ya kuyazingatia hasa (2-6) kwa maendeleo ya taifa letu.
 
Matumizi ya dollar yamekithiri,hadi baadhi ya mashirika ya umma hutoa huduma kwa rates za dolar! Safari ni ndefu sana.
 
Matumizi ya dollar yamekithiri,hadi baadhi ya mashirika ya umma hutoa huduma kwa rates za dolar! Safari ni ndefu sana.
Jamani ulivyo sema hapo juu vinachangia kwa asilimia chini ya 20%. Strength of currency depends more than 70 per cent of exports vs imports and tanzania is net importer more than 70 per cent. I will advise protection of local products and find ways of increasing our exports. Thanks
 
Back
Top Bottom