Matumizi ya fedha za kigeni nchini yapigwe marufuku

Jambo kubwa kabisa ambalo lingeimarisha sarafu yetu ni kuiondoa ccm madarakani.

Hii ingejenga morari ya uwajibikaji ambayo kwa sasa imekufa imebaki ya wizi.

ili uuze nje lazima uzalishe ndani kwanza, ccm imetengeneza wezi sio wazallishaji, kwa hiyo usitegemee kupata cha kuuza nje kutoka kwa zao la ccm.

Hifadhi ya dhahabu hu stabilize sarafu, pamoja na wingi wa dhahabu nchini kwetu sidhani kama tuna hifadhi ya dhahabu hata "Tola" moja pale bank kuu tulimowajaza watoto wa wenye ccm.

hata sospita muhongo haitambui Tsh.
rejea mawasiliano yake kwa umma "..................umeme utauzwa kwa cent za kimarekani ......."

Watanzania wana morari ya kuiba kama Chenge, wanahamu ya kuvunja rekodi ya Liyumba, wanausongo wa kufanya kama Karamagi, wana hamu ya kumzidi masamaki idadi ya "mijengo" wanataka wampiku "Dewiji" kumiliki wingi wa mahekari ya ardhi.

CCM IMETUTENDA VIBAYA!!!!!!!!

Eti watanzania nao wana ndoto za kuishi kimarekani!!!!! (ref. baba mwanaasha)

eti wana ndoto ya kuwa na viwanda kama bakhresa!!!!!!

Sukita tu imewashinda,

Wenye Ubongo wamenielewa.
 
Kwanza nnakuuliza ni nani alikuambia kuwa shillingi ya Tanzania inahitaji kuimarishwa?

Umeandika kichwa cha habari kingine na utumbo mwingine.

Unataka kuimarisha shillingi au unataka kushusha thamani ya dollar? Fikiri.

Faiza ulikuwa wapi ! Pili unaonekana we si mtz kwa sababu hutaki MTU atoe mawazo ya kizalendo siyo ???? We ni wa nchi gani dola ikishuka we unaasilika vipi ??? Wtz zaidi ya million 40+ hawajui matumizi ya dollars Leo hii unaitete yaa nn
 
Matumizi ya dollar yamekithiri,hadi baadhi ya mashirika ya umma hutoa huduma kwa rates za dolar! Safari ni ndefu sana.

Si unajua wenye nyumba ndogo kipindi cha baba riz walianza kuhonga dola, si uliona hata wema alimpatia zawadi mh Magufuli ya noti za dola
 
Nchi haina wa kusilikiza. Maoni kama haya huko BOT na kwingineko wanjua sana.Ni kama walivyokuwa wanajua wizi wa makontena bandarini lakini wanapiga kimya. Haingii akilini pale Waziri wa fedha anapodai eti nchi haiwezi kwenda bila dola za marekani. Kupiga marufuku matumizi ya dola haihitaji kufikiri sana.

Wananunua dola zote, wanagiza bidhaa nje, halafu hizo bidhaa hazilipiwi kodi halafu wanakuja kuuza kwa dola. Nchi feki kabisa. Hata house girl anaweza kuiongoza.
 
Ubarikiwe mkuu....hakika wewe ni mzalendo wa kweli........
Matatizo ya taifa hili mzizi wake ni uzalendo miongoni mwa wananchi.....mambo yote uliyoyaoanisha hapo yanahitaji uzalendo wa kiwango cha juu.......kila mwananchi anapaswa kuipenda nchi yake kwa moyo wake wote na akili yake yote.....hapo tutakapoanza safari ya kuelekea utawala bora.......na uchumi wetu.......
Ni TANZANIA PEKEE AMBAPO MWANANCHI ANASHIRIKIANA NA MGENI KUKWEPA KODI.........ALAFU MWANANCHI HUYO HUYO ANALALAMIKIA KUHUSU UPUNGUFU WA MADAWA HOSPITALINI......



Mwananchi kulalamika ni sawa na haki isipokuwa anyefanya hivyo ni yule aliyepewa dhamana,usipotoshe umma.
 
Hebu tuangalie kwanza kibiashara hapa kwa majirani zetu wanafanyaje? Je ni kweli haya malipo ya forodha ni moja? Kwanini watz wanakwenda Kenya, Uganda kununua bidhaa takribani za aina zote tena wakienda huko wanapeleka dola.Nina was was wanaigeuka Tz na wao wanaweka kiwango kidogo cha kodi.

Miaka ya nyuma ilikua wao ndio wanakuja hapa Tz kununua na walikua wanaacha dola.

Tukianza kurudisha wageni kuja kununua hapa tutasimmisha uchumi wetu vizuri sana wa viwanda na kilimo, mifugo na uvuvi na sio tupeleke bidhaa kule kwenda kutafuta solo.
 
kombi gani umesoma;

kama hujui kitu ; Omba msaada;

KAMA HUNA DEGREE YA UCHUMI KAA KIMYA ; AU SOMA KWA NJIA YA POST




Nazungumzia sheria ya fedha za kigeni. Hii haina uhusiano na kombi wala uchumi. Hata tungekuwa na uzalishaji mkubwa na kuuza bidhaa nyingi nje ya nchi kama hizi sheria za fedha za kigeni tulizo nazi hazisimamiwi ni kazi bure. Leo hii ukitaka kuagiza bidhaa nje ya nchi unaweza kwenda bureau de change ukanunua kiasi chochote cha fedha za kigeni bila kuulizwa nyaraka yoyote! Hata ukitumia benki huulizwi nyaraka za kodi (SBE)kwa malipo ya bidhaa au huduma unayyolipia nje ya nchi!

Inaonekana wewe bado uko shule au chuo. Sisi tuko kwenye field miaka mingi na tumeona nchi jirani wanavyosimamia uchumi wao. Nenda hapo Nairobi kama utauziwa foreign currency bila kuonyesha passport na kupewa receipt ya Central Bank of Kenya! Kuwa na uzalishaji na export ni swala lingine na usimamiaji wa sheria ni swala lingine. Kama wewe siyo mkaguzi wa BOT mla rushwa utakubaliana nami.
 
Jamani ulivyo sema hapo juu vinachangia kwa asilimia chini ya 20%. Strength of currency depends more than 70 per cent of exports vs imports and tanzania is net importer more than 70 per cent. I will advise protection of local products and find ways of increasing our exports. Thanks

Umesahahu kuwa pamoja na importation ya Goods, lakini pia sisi tuna export Dolar nyingi nje kama faida kutoka makampuni mengi ya kigeni, Vodacom, Cement companys, Beer companys, Sugar companys hizi zote zinauza bidhaa kwa madafu, na wanatakiwa wapeleke faida kwao, na kazima wapeleke interms of Dollar.
 
Faiza ulikuwa wapi ! Pili unaonekana we si mtz kwa sababu hutaki MTU atoe mawazo ya kizalendo siyo ???? We ni wa nchi gani dola ikishuka we unaasilika vipi ??? Wtz zaidi ya million 40+ hawajui matumizi ya dollars Leo hii unaitete yaa nn

= unaathirika

Kanisome tena labda utanielewa na usitake kutia maneno yako kinywani mwangu.
 
Naomba elimu hapo kwenye kuimarisha shilingi na kushusha thamani ya dollar. Siwezi fikiri bila elimu ya kuanzia. Pls nimekuwa nikitatizwa sana na hivi vitu. Kuna kipindi China walishusha thamani ya pesa yao, watu wakawajia juu kumbe wao walikuwa na strategy yao kiuchumi. Honestly sielewi haya makitu

Naam. Hilo la Uchina ni kweli kabisa, walishusha thamani na "wakubwa" wakapiga kelele, hususan USA.

Mleta mada anajaribu kuchora picha ambayo hata yeye mwenyewe haelewi.

Kwa ufupi, uchumi unaotegemea kuuza nje (export) hupenda dollar ikawa juu ili wauze zaidi.

Uchumi unaotegemea kununua nje (import) hupenda dollar iwe chini ili wapate kununua zaidi.

Kwa ufupi, wenye kuzimiliki dollar wao wanafaidika kila mnaponunua au kuuza bidhaa kwa hiyo wao hawaathiriki na hivi visenti vyenu vya madafu vikipanda au vikishuka.

Kwa nchi kama Tanzania inayotakiwa iwe muuzaji nje (exporter) ni vyema dollar ikawa inanunua zaidi shillingi na ni fursa ambayo mimi binafsi sitaki iondoke, kwani sasa hivi nnauza mikeka na majamvi yangu kwa faaida nzuri zaidi.

Mfano, wakati dollar 1 ni sawa na 1,500 jamvi lililokuwa linanigharimu dollar 10 au Shilingi 15,000/= kulisafirisha nje, sasa hivi (kwa bei ya dollar 1 = shillingi 2,100) jamvi hilohilo linanigharimu dollar 7.14 utaona kuwa Dollar 2 na ushee ni faida iliyoongezeka kwa kila jamvi.

Nnawashauri Watanzania tutumie fursa hii kusafirisha zaidi (export). Wataolia hapa ni wale wale wanaoagiza vitu nje halafu tumeona baadhi yao wanakwepa kuvilipia kodi. Wanalitia Taifa hasara juu ya hasara.
 
Napata shida sana kurespond kwenye hii thread...huitaji degree ya uchumi ili kujua kinachosibu sarafu yetu kuendelea kuporomoka. Nashangaa unaniuliza issue za Somalia...what has Somalia have to do with the discussion? Ila kwa haraka-haraka Somalia ni nchi mojawapo inayoongoza kwa pesa chafu Africa. Wanazipataje dola na ku-stabilize currency yao...I suggest u watch Captain Phillips movie by the legendary Tom Hanks ili ujionee 'Shadow Economy' yao inavyofanya kazi.
 
Back
Top Bottom