Matumizi ya chumvi kuondoa mikosi

Duh! Hii itakuwa kati ya zile zile zetu wabongo. Nakumbuka nikiwa chalii, tulikuwa tunaambiwa ukikutana na kinyonga unajitemea mate kiaina mwili mzima ili kuzuia asichukue rangi yako. Sikumbuki kama ilikuwa inafanya kazi.
Hahaha au ukikutana na zeru zeru unajitemea mate kifuani.....
 
->msindikize mgeni usiempenda huku umeshika chumvi kiganjani mkono wa kushoto,wakati mnaachana kwa kupeana mikono,hasa wakati unageuka kurudi irushe Juu nyuma yako huku ukisema," kismass and never come to me again"ondoka bila kuheuka nyuma straight to home...
Hahaha hiyo balaaaah
 
Mkos ni jambo au hali ya kupatwa na mambo mabaya yaan kila kitu ukihitaji kufanikiwa kinagoma. Mfano kila jambo unalofanya huwez kufanikiwa hata ufanye nin unakuwa mtu wa kushindwa tu
Dah hii mara nyingi mipango hufiaga mwishoni kabisa!

Yani ishu inatakiwa ikamilike unashangaa majanga yametokea. Mara mteja kabadili mawazo, mara simu umepigiwa hupatikani wakati iko hewani, mara umeachwa solemba yani mambo kibao, au unapanga kufanya kitu ila unajikuta mzito kweli bila sababu! Yani unapanga kesho ntafanya kitu flani ila ikifika hio siku unapatwa na uzito wa ajabu unaghairisha!
 
YESU aliwaambia wanafunzi wake hivi: “Nyinyi ndio chumvi ya dunia.” (Mathayo 5:13) Nao Waarabu husema kwamba, “Kuna chumvi kati yetu,” na Waajemi husema kuhusu “asiye wa kweli kwa chumvi” (asiye mwaminifu au asiye na shukrani). Kwa kuwa chumvi inaweza kuhifadhi vitu, neno “chumvi” limeheshimiwa na kustahiwa katika lugha za kale na hata za leo.

Chumvi pia imekuwa alama ya uthabiti na udumifu. Hiyo ndiyo sababu, katika Biblia agano muhimu liliitwa “agano la chumvi,” na wale waliokubaliana mara nyingi walikula mlo pamoja, uliotiwa chumvi ili kuidhinisha agano hilo. (Hesabu 18:19) Chini ya Sheria ya Musa, chumvi ilitiwa kwenye matoleo madhabahuni, bila shaka ikionyesha hali ya kutokuwa na ufisadi au uharibifu wowote.



Jr
Nakumbuka kuna kipindi ni lilala na mwana mke moja aisee week karibia nzima nilikua na mikosi ya ajabu ajabu nika kaa chini na kufikiria nini hiki nikakumbuka kua ni mwanamke niliye lala naye na fikiri ndo amaniachia maroho na mikosi ya ajabu ajabu.

Nakumbuka kuna uzi nilisoma humu kuhusaian na chumvi , nikaamka asubuhi inayofuata nika chemsha maji nika chukua chumvi kidogao nikainenea nainyunyuzia hi chumvi DAMU YA YESU iniondole mkosi,na balaa ,na hatari zote kisha nikaitia ndani ya Maji nikaenda kuoga

Aise kwanza nilivyo toka kuoga nilijisiakia amani flani hivi nanutulivu usio wakawaida , alafu nikaingia job asikuambie mtu hiyo siku Mambo yalienda fresh sana mpk leo.

Miinamini kuna nguvu katika chumvi endepo imani yako ni thabiti.
 
Nakumbuka kuna kipindi ni lilala na mwana mke moja aisee week karibia nzima nilikua na mikosi ya ajabu ajabu nika kaa chini na kufikiria nini hiki nikakumbuka kua ni mwanamke niliye lala naye na fikiri ndo amaniachia maroho na mikosi ya ajabu ajabu..
Nakumbuka kuna uzi nilisoma humu kuhusaian na chumvi , nikaamka asubuhi inayofuata nika chemsha maji nika chukua chumvi kidogao nikainenea nainyunyuzia hi chumvi DAMU YA YESU iniondole mkosi,na balaa ,na hatari zote kisha nikaitia ndani ya Maji nikaenda kuoga
Aise kwanza nilivyo toka kuoga nilijisiakia amani flani hivi nanutulivu usio wakawaida , alafu nikaingia job asikuambie mtu hiyo siku Mambo yalienda fresh sana mpk leo..
Miinamini kuna nguvu katika chumvi endepo imani yako ni thabiti.
Maji ya moto ulifanyia nn mkuu?
Au ndo uliogea?
 
Maji ya baraka ya kibongo yanauzwa toka kiwandan vile vile yakiwa sealed! ni utapeli tu
 
Ni kweli kabisa mkuu, chumvi ni tiba iloyowekwa na mungu kiroho na hata kwenye vitabu vitakatifu imetajwa kwenye kuponya watu, mimi mwenyewe nimefanikiwa vitu vingi sana kupitia kujitakasa kwa chumvi ya mawe pamoja na mafuta ya zaituni.
Heshima kwenu wakuu.

Kuna hii dhana ya matumizi ya chumvi kuondoa mikosi katika maisha, hivi hii kitu ni kweli na inafanyaje kazi.niliona sehemu watu wakitoa ushuhuda kuhusu wao kuchoma chumvi na ikawatendea kama vile walivotamani iwe.

Nawasilisha na natamani kujua kama ni kwel.
 
Back
Top Bottom