Matumizi makubwa yatishia uhai wa Bima ya NHIF

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imesema, imebaini Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unatengeneza nakisi katika mapato na matumizi, jambo ambalo linatishia uhai wa mfuko.

Mwenyekiti wa PIC, Jerry Silaa ameyasema hayo leo Alhamis Agosti 25, 2022 baada ya kupokea taarifa ya uwekezaji na hesabu za mfuko huo.

Amesema baada ya kufanyia uchambuzi taarifa hizo, kamati imeelekeza NHIF kufanya mchakato kwa kuongeza wanachama kwa sababu malipo ya huduma za wanachama yamekuwa yakiongezeka ukilinganisha na mapato yanavyoongezeka.

“Kwa hiyo gharama zinaongezeka kuliko mapato na hii inahatarisha uhai wa mfuko kwa hivyo kamati imeelekeza ifanye juhudi za makusudi za kuongeza wanachama,” amesema Silaa.

Pia, amesema wameuagiza mfuko huo kuwa na jitihada za makusudi za kuhakikisha kuna utaratibu mzuri wa kuthibiti matumizi.

Amesema kamati imeelekeza mfuko huo kuboresha mifumo ya Tehama kwasababu wameona kuna mapungufu ya mifumo ya Tehama.

Amesema kama NHIF itaimarisha mifumo yake ya Tehama kwenye majukumu yake yote manne wanaweza kupunguza udanganyifu na mapato yao yakaongezeka.

Ameyataja maeneo hayo ni uandikishaji wanachama, wanapopata huduma kwenye vituo vya kutolea huduma kuhakikisha mwanachama anapata huduma madhubuti inayoendana na uanachama wake pamoja na maradhi anayoumwa na udahili wa madai ya watoa huduma.

“Yote haya yakiwa katika mfumo, matumizi ambayo yanaonekana yana aina fulani ya udanganyifu yatapungua na mapato yataongezeka ili uweze kuhudumia wanachama wake wote,” amesema.

Amesema NHIF ikiendelea kuwa na nakisi katika mapato na matumizi kila mwaka kunaweza kusababisha mfuko huo kula mtaji uhai wa shirika ndio maana amesema uhai wa shirika unaanza kutishika.
 
Ukweli ni kwamba hospitali nyingi za private wanapika data na itaigharimu NHIF. Suluhisho hapa ni kwamba NHIF itumie hospitali za serikali kwa kuhakikisha kuwa hospitali zote za serikali zina jengewe uwezo wa kuwahudumia wateja kwa speed na ubora, kuimarisha miundombinu, vifaa tiba, kuwa na wataalamu wabobezi wa kutosha yaani specialist na pia kuhakikisha kunakuwepo na dawa za kutosha na namna bora ya kuwakarimu wateja.
 
Pia bei ya sawa iwekwe wazi na NHIF walipe bei za kawaida kama dukani au waongeze kidogo kama ni pcm inauzwa 1500 per dose basi wao walipwa 2000 siyo kama ilivyo sa hizi unakuta vituo vya afya A,B na C wako mji mmoja labda mwanza huduma Moja Kila kituo kina bei yake.
Hili haliko sawa na wanao ua mifuko ni wale WATUMISHI WA NHIF
 
Tunakoelekea NHIF inaenda kufa. la sivyo, itabaki kama iCHF. Kumekua na tabia ya Mfuko kukata madai ya wagonjwa waliohudumiwa kwa bima eti ya sababu ya codes. Sasa wakiuchukua ushauri wa jamaa, mfumo ndio kwishnei. Bora turudi kwenye malipo ya papo kwa papo. yanasaidia.
 
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imesema, imebaini Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unatengeneza nakisi katika mapato na matumizi, jambo ambalo linatishia uhai wa mfuko.

Mwenyekiti wa PIC, Jerry Silaa ameyasema hayo leo Alhamis Agosti 25, 2022 baada ya kupokea taarifa ya uwekezaji na hesabu za mfuko huo.

Amesema baada ya kufanyia uchambuzi taarifa hizo, kamati imeelekeza NHIF kufanya mchakato kwa kuongeza wanachama kwa sababu malipo ya huduma za wanachama yamekuwa yakiongezeka ukilinganisha na mapato yanavyoongezeka.

“Kwa hiyo gharama zinaongezeka kuliko mapato na hii inahatarisha uhai wa mfuko kwa hivyo kamati imeelekeza ifanye juhudi za makusudi za kuongeza wanachama,” amesema Silaa.

Pia, amesema wameuagiza mfuko huo kuwa na jitihada za makusudi za kuhakikisha kuna utaratibu mzuri wa kuthibiti matumizi.

Amesema kamati imeelekeza mfuko huo kuboresha mifumo ya Tehama kwasababu wameona kuna mapungufu ya mifumo ya Tehama.

Amesema kama NHIF itaimarisha mifumo yake ya Tehama kwenye majukumu yake yote manne wanaweza kupunguza udanganyifu na mapato yao yakaongezeka.

Ameyataja maeneo hayo ni uandikishaji wanachama, wanapopata huduma kwenye vituo vya kutolea huduma kuhakikisha mwanachama anapata huduma madhubuti inayoendana na uanachama wake pamoja na maradhi anayoumwa na udahili wa madai ya watoa huduma.

“Yote haya yakiwa katika mfumo, matumizi ambayo yanaonekana yana aina fulani ya udanganyifu yatapungua na mapato yataongezeka ili uweze kuhudumia wanachama wake wote,” amesema.

Amesema NHIF ikiendelea kuwa na nakisi katika mapato na matumizi kila mwaka kunaweza kusababisha mfuko huo kula mtaji uhai wa shirika ndio maana amesema uhai wa shirika unaanza kutishika.
Namba hazidanganyi
 
Back
Top Bottom