CAG: Wastaafu na wenza wao wanaigharimu NHIF Tsh 84.7 billion kila Mwaka Bila Wao kuchangia

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,039
CAG Kichere amesema Hasara nyingine wanayoingia NHIF inatokana na Wastaafu na Wenza Wao kufaidika na Fedha za Mfuko huo Bila Wao kuchangia

Kicheere amesema Wastaafu na Wenza Wao wanaugharimu Mfuko wa Bima tsh 84.7 billion kila Mwaka Bila Wao kuchangia.

Mlale Unono
 
CAG Kichere amesema Hasara nyingine wanayoingia NHIF inatokana na Wastaafu na Wenza Wao kufaidika na Fedha za Mfuko huo Bila Wao kuchangia

Kicheere amesema Wastaafu na Wenza Wao wanaugharimu Mfuko wa Bima tsh 84.7 billion kila Mwaka Bila Wao kuchangia

Mlale Unono
Hajajielekeza vizuri katika tafsiri/maana ya bima, kuwa unachotoa siyo unachokipata, mtu anaweza asiumwe hata zaidi ya miaka mitano, lakini bado akaendelea kuchangia, je hizo fedha anazochangia zinakwenda wapi?.

Kwa mantiki hiyo, Kichere alitakiwa aseme pia faida wanayoipata NHIF kwa kukusanya fedha za wachangiaji ambao hawajaugua/kupata matibabu kupitia bima kwa kipindi cha mwaka mzima, maana hao nao wapo wengi, na mfuko unanufaika pia.
 
Huyu CAG hapo kwa wastaafu amechemka!!!

Kwenye issue ya wastaafu kutibiwa na NHIF wakati hawachangii chochote. Hapa itabidi wapaache hivyo hivyo.

Kwa mfano mimi binafsi toka tulipoanza kuchangia mfuko mwanzoni mwa miaka ya 2000's sikuwahi kuugua na kutumia kadi ya NHIF.

Kwa nini leo mfuko wa NHIF usinitibu wakati nimestaafu??

Si hivyo tu, hii inaondoa dhana nzima ya Bima ya Afya.
In fact the major concept of Health Insurance Scheme is that "Insurance is a way to manage your financial health risks". That is When you buy insurance, you purchase protection against unexpected health financial losses.

Hii ikiwa na maana ya kwamba, mtu anaweza kushambuliwa na maradhi/ugonjwa wakati wowote, na kuna kipindi mtu anakuwa hana pesa za kumudu gharama za matibabu, sasa hapo Bima ndio inachukuwa nafasi yake.

Funny enough, it was just last week in a TV programme (Kipima joto), kuna kiongozi mmoja wa Chama Cha Wamiliki Hospitali Binafsi (APHFTA) alipokuwa akielezea sababu za NHIF kushindwa kumudu kujiendesha ipasavyo, ni kwamba mfuko unahudumia wagonjwa wengi kuliko wachangiaji wakiwemo wastaafu, amesahau kwamba hawa wastaafu ndio walio wekeza kwenye huo mfuko wa Bima kwa maana ya kuweza kumudu tiba hapo baadae.

Kwa kweli ni kauli yenye kusikitisha na yenye kukatisha tamaa, iliyo tolewa na mtu ambae haelewi dhana nzima ya Bima.

Ni dhahir CAG nae ameshindwa kutafakari vema hapo na kuamua kuiona hiyo kama hoja inayojenga.
 
Wazee wamechangia NHIF zaidi ya miaka 10 na zaidi kuhitimu kupewa KADI ya wastaafu mke na mume.
-Mifuko ya bima iwe ya afya au magari,mfuko husika unapaswa kuwekeza kwenye Treasury bills na bond au financial institution zingine kwa Madhumuni ya kukuza mifuko na kupata fedha za uendeshaji.
-Lakini NHIF inatumia michango ya wanachama kulipana posho na kukopesha watumishi au kuwekeza kwenye miradi ya Serikali kama vile ujenzi wa UDOM nk ambayo return on investment ni ndogo au Serikali inashindwa kulipa mkopo
-Aidha Serikali mwaka 2015 ilifanya uamuzi mgumu wa fedha zote za taasisi za UMMA kuwekwa Benki kuu badala ya Benki za biashara au kuwekeza kwenye Treasury bond na Treasury bills.
-Ni wakati muafaka sasa fedha za mifuko ya hifadhi za jamii ziwe zinawekezwa kwenye Treasury bond na Treasury bills au ujenzi wa viwanda vyenye high return au kununua hisa za kwenye makampuni yanafanya vizuri
 
CAG Kichere amesema Hasara nyingine wanayoingia NHIF inatokana na Wastaafu na Wenza Wao kufaidika na Fedha za Mfuko huo Bila Wao kuchangia

Kicheere amesema Wastaafu na Wenza Wao wanaugharimu Mfuko wa Bima tsh 84.7 billion kila Mwaka Bila Wao kuchangia

Mlale Unono
Hapo ukiweka Pensheni na huduma nyinginezo, utakuta Wastaafu wanakula 0.5T kwa mwaka, Na Bado utasikia Mwigulu kasafiri kwenda Sweden kuomba msaada wa 100B.
 
Wazee wamechangia NHIF zaidi ya miaka 10 na zaidi kuhitimu kupewa KADI ya wastaafu mke na mume.
-Mifuko ya bima iwe ya afya au magari,mfuko husika unapaswa kuwekeza kwenye Treasury bills na bond au financial institution zingine kwa Madhumuni ya kukuza mifuko na kupata fedha za uendeshaji.
-Lakini NHIF inatumia michango ya wanachama kulipana posho na kukopesha watumishi au kuwekeza kwenye miradi ya Serikali kama vile ujenzi wa UDOM nk ambayo return on investment ni ndogo au Serikali inashindwa kulipa mkopo
-Aidha Serikali mwaka 2015 ilifanya uamuzi mgumu wa fedha zote za taasisi za UMMA kuwekwa Benki kuu badala ya Benki za biashara au kuwekeza kwenye Treasury bond na Treasury bills.
-Ni wakati muafaka sasa fedha za mifuko ya hifadhi za jamii ziwe zinawekezwa kwenye Treasury bond na Treasury bills au ujenzi wa viwanda vyenye high return au kununua hisa za kwenye makampuni yanafanya vizuri
Kairuki Hospital wametengeneza kiwanda cha Dawa sasa ivi wanasambaza TZ yote, ila hao NHIF kazi kulipana posho na kupeana mikopo isiyo na riba. Hizo fedha wanazo kopesha wangewekeza kwenye viwanda vya dawa, saizi wangekuwa mbali sana.

Ndio mana watu hawataki kustaafu, kama mstaafu anaonekana ni tatizo dah! na wanataka hata hiyo bima ya afya anyang'anywe! hii ni laana
 
Hawa wastagu ni akinanani,,mbona pesa nyinginhivi?
Hao ndio walewale wanao Lipwa pia mabilioni kama pension, huduma mbalimbali majumbani kwao kumbe hata matibabu pia hawalipii Bima?
Ona mwanajeshi mzee aliyepigana vita Uganda kumtoa Nduli Amin au Daktari aliyestaafu mwaka 2000 na bado yuko hai ila mzee kule Hazina wanamlipa Laki moja kwa mwezi na hakuna cha Bima wala hata aspirin ya bure!
Tuna laana sisi!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu akili ni ziro kabisa wastaafu ni watu ambao hawapo tena katika UTUMISHI WA UMMA hajamaanisha Wastaafu viongozi kwa akili hizi that's why tupo nyuma kila siku
Hebu tutajie wastaafu gani wengine wanalipiwa huduma za afya kwa kutumia NHIF zaidi ya wastaafu viongozi na wenza wao?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
CAG Kichere amesema Hasara nyingine wanayoingia NHIF inatokana na Wastaafu na Wenza Wao kufaidika na Fedha za Mfuko huo Bila Wao kuchangia

Kicheere amesema Wastaafu na Wenza Wao wanaugharimu Mfuko wa Bima tsh 84.7 billion kila Mwaka Bila Wao kuchangia

Mlale Unono
Kwanza matibabu kwa wazee si ni bure? Sasa hii ya wastaafu kutibiwa halafu mnadai wananufaika huku hawachangii kuna shida gani?? Hapa wanalenga mstaafu kuendelea kuchangia ilihali huyu mtu hana kazi tena na wala nguvu za kufanya kazi.
 
Back
Top Bottom