Matukio ya Kusikitisha Uwanjani

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
1. Kujifunga goli kulikopelekea mauti ya mchezaji wa Colombia
2. Kifo cha Kiungo mahiri sana wa Cameroon, Marc Vivian Foe
3. Kitendo cha Ronaldinho kumfunga Seaman goli la kubahatisha
4. Kuumiza vibaya kwa Companero kulikomfanya atandike daluga
5.....
 
Ronaldinho ni kama maji...
Usipoyaoga ukiwa hai basi utaogeshwa ukiwa mauti.
Ronaldinho ni jina juu ya majina.
 
kweli wewe ni mtumwa hapa tanzania kuna matukio makwa kuliko hayo..

yataje - ndio maana umewekewa 5...hapo juu uendeleze mada; haya tuendelee:

5. Kifo cha mchezaji Tindwa uwanjani, Prof. Shaba anasema hajui aliwezaje kucheza maana moyo wake ulikuwa kama mkusanyiko wa nyuzi!

6. Beckham kuwafanyia fujo wazee wa Argentina na kutolewa kwa kadi nyekundu hivyo kuharibu kuibuka kwa kijana Michael Owen siku hiyo!

7. Kuvunjika mguu kwa mashine ya kupachika mabao ya Kiholanzi, Marco van Basten na kusababisha astaafu mpira kabla ya wakati wake!

8. Timu kutokea uwanjani kifua wazi kutokana na ukata uliotokana na kushindwa kutimiza njozi njema ya Ujamaa, Nyerere alisikitika sana!

9. Kuvunjika mguu kwa kiungo mchezaji machahari wa Argentina, Fernando Redondo, ambaye Man U hawatakaa wasahau tobo alilowapiga!

10. Kuonekana kwa kitambi cha Ronaldinho kilichoashiria kuisha kwake na kupelekea kuachwa kwenye Selecao na kuwasikitisha wasauzi!

11....
 
11. Rafu ya Boban kwa Kelvin Yondani iliyosababisha avunjike mfupa mmoja wa paja.
12. ..............................
 
1. Kujifunga goli kulikopelekea mauti ya mchezaji wa Colombia
2. Kifo cha Kiungo mahiri sana wa Cameroon, Marc Vivian Foe
3. Kitendo cha Ronaldinho kumfunga Seaman goli la kubahatisha
4. Kuumiza vibaya kwa Companero kulikomfanya atandike daluga
5.....

Kifo cha Peter Tino uwanja wa Taifa Dar.
 
marefa wa timu za zanzibar kuwaomba wachezaji waachie goli baada ya kuona kitim chao kimeibana simba s c.
 
kipa pesa mbili aliyeuliwa na daluga la mchezaji wa 44 KJ kule mbeya... miaka ya mwanzoni mwa 2000s
 
labda nimuweke sawa kaka,si pesambili aliyefia uwanjani bali ni nadhir mussa mchomba aliyefia uwanjani alikuwa kipa wa afc arusha ni kutokana na daluga la mchezaji keneth pesambili wa 44 kj ya mbeya,ilikuwa tarehe 5/5/2001 na nadhir ni baba yangu mdogo wa kuzaliwa tumbo moja na baba,asante kaka
 
Kipigo cha mbwa mwizi walichopata YANGA pale taifa!
Wadau mtajazia ilikuwa lini vile?
Walikojolewa ngapi?
 
Back
Top Bottom