Jambo Unalolipenda na Kulitumikia Lina Uhusiano wa Moja Kwa Moja na Kifo Chako


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,028
Likes
5,490
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,028 5,490 280
Jambo Unalolipenda na Kulitumikia Lina Uhusiano wa Moja Kwa Moja na Kifo Chako
MUNGU ni wa ajabu. Ajabu yake inakamilishwa na yaliyomo ulimwenguni, ikiwemo yanayoonekana na yale ya kusadikika. Uwepo wa uhai umekamilisha pande mbili za shilingi ambazo ni uhai na kifo/mauti.

Upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya kile unachokipenda na kifo chako. Wazungu wanaita “hobby”, hivyo hobi yako inaweza kuwa njia kuelekea safari ya mwisho wa maisha yako.

Mpenzi wa kuogelea anaweza kuyapoteza maisha yake katika maji, mwanamuziki anaweza kufa kwa kuanguka jukwaani ama chumba cha rekodi, mwanamasumbwi anaweza kufa akiwa na mpenzi, mwendesha gari anaweza kufikwa na mauti akiwa katika usukani vivyo hivyo kwa tasnia zingine na watendaji wake.Paul William Walker.

Hii inaonyesha kifo kinaweza kusababishwa na mfumo wa maisha unayoishi kupitia jambo lile ulilolipenda. Starehe unayoipenda zaidi, ile yenye kuufurahisha moyo wako inaweza kuwa tiketi ya kuelekea safari yako ya mwisho. Ipo mifano hai ya watu maarufu na mashuhuri ambao mapenzi yao dhidi ya jambo fulani yamekamilisha safari yao ya kurejea kwa Mwenyezi Mungu.

Tumrejelee Paul William Walker aliyekuwa muigizaji mashuhuri ulimwenguni aliyezaliwa mwezi Septemba 12, 1973 huko Glendale, Califonia, na kufariki dunia Novemba 30, 2013 huko Santa Clarita katika jimbo la Califonia kwa ajali ya gari. Walker alifariki akiwa na rafiki yake Roger Rodas.

Kifo cha Paul Walker kiliibua simanzi kwa wapenzi wa filamu ulimwengu. Hisia hizo zilisindikizwa na wimbo wa Wiz Khalifa “See You Again” uliotumika katika filamu ambayo alishiriki Furious 7 (2015) lakini hakushiriki mpaka mwisho hivyo baadhi ya vipande walimtumia mdogo wake kukamilisha filamu hiyo.

Aliyekuwa nguli wa muziki wa dansi mwenye uraia wa Jamhuri ya Kidemodrasia ya Kongo, Papa Wemba, alifariki dunia kwa kuanguka jukwaani akitumbuiza. Janga hili linathibitisha mada yetu ya uwepo wa mahusiano ya kifo katika kile unachokipenda au kazi unayoifanya.Marc-Vivien Foé .

Papa Wemba alianguka jukwaani akifanya shoo huko Abdjan, Ivory Coast, na mitandao mingi ikaripoti kuwa ameuawa baada ya kuwa na hali ya utata kwa mtu asiyefahamika kuoneka kukatiza jukwaani.

Bondia wa ngumi za kulipwa maarufu kama Thomas Christopher Malifedha Mashali, alishambuliwa na silaha za jadi na watu wasiojulikana, ni baada ya kushindwa kuelewana na kuleta ubabe wa ulingoni mtaani. Zipo stori tofauti-tofauti mtaani ambazo zinaongelea kifo ambacho bado kina majonzi mabichi.

Ni Jumapili ya wiki iliyopita maeneo ya Kimara, Bonyokwa, jijini Dar es Salaam, ndipo pumzi za Mashali ilipouacha mwili. Jambo alilolipenda zaidi Mashali ni masumbwi na ndiyo sababu ya mauti yake ambapo inasemekana baada ya kuleta ubabe akaitiwa kelele za mwizi.Thomas Mashali.

Tuhitimishe na mchezaji wa mpira wa miguu kiungo wa zamani wa Cameroon, Marc-Vivien Foé ambaye alifariki dunia kwa kuanguka uwanjani na kudhaniwa kazimia lakini taarifa zikathibitika kuwa amekufa baada ya kufikishwa hospitali.

Foé alianguka wakati wa mechi ya nusu fainali katika mpambano wa Kombe la Mabara dhidi ya Colombia mjini Lyon, Ufaransa, Juni 2003. Enzi za uhai wake marehemu aliwahi kuichezea West Ham United, Manchester City na mauti yalimfika akiichezea Lyon.

Salum Milongo

GPL
 

Attachments:

kelao

kelao

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Messages
5,874
Likes
2,284
Points
280
Age
40
kelao

kelao

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2012
5,874 2,284 280
Kweli inawezekana kabisa,mf:kuna ndugu yetu alipoteza maisha akiwa shambani kwake,haijulikani aligongwa na nyoka au la ila alipenda sana kazi za shambani
 
swissme

swissme

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2013
Messages
13,620
Likes
18,001
Points
280
Age
19
swissme

swissme

JF-Expert Member
Joined Aug 15, 2013
13,620 18,001 280
Na wale wapenda ngono wengi wao hufa kitandani au lile libaba lao UKIMWI.


SWISSME
 
Econometrician

Econometrician

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2013
Messages
9,573
Likes
10,003
Points
280
Econometrician

Econometrician

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2013
9,573 10,003 280
kwenye siasa ndio kiboko--maisha yako yanakuwa mafupi kama ya nzi
 

Forum statistics

Threads 1,274,097
Members 490,586
Posts 30,500,880