Phiri hajawa 100% Fit, ila Presha ya Ufungaji na Mayele inamfanya ajilazimishe Kapona ili apangwe

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,737
109,165
Nimemuona Jana tena kwa Jicho langu Kali la Kiuchunguzi na Kimaono na kugundua kuwa Mshambuliaji Moses Phiri bado hajawa Fiti kuanza Kucheza Mechi zozote zile.

Najua kuna Majuha ( Fools ) watakuja Kunishambulia na kuhoji je, Mimi GENTAMYCINE ni Daktari mpaka niseme hivi?

Majibu yangu Kwao ni kwamba Wachezaji wengi ( hasa wa Tanzania ) wa hizi Timu Kubwa hudiriki hata Kuwahonga Madaktari wa Timu ili Wadanganye na waseme Wamepona ili Wacheze na wakipangwa huwapa 10% ya ama Posho zao au Mishahara yao.

Kuna Golikipa wa Timu Moja Kubwa ilipokaribia Kariakoo Derby ambayo alishaichungulia kwa Mganga wake mkubwa huko Kwao Mang'ula Mkoani Morogoro akachonga Dili na Daktari wa Timu yake kuwa ameumia Dressing Room hivyo hatoweza Kucheza na akapangwa Kipa Mlokole japo Mkewe ni Mshirikina sana na Kufungwa hiyo Derby Kubwa.

Kinachomgharimu na Kumtesa Moses Phiri ni Ufungaji Bora na kwanini apitwe na Fiston Mayele wa Yanga SC hivyo anataka Kulazimisha kwa kila namna ili acheze na afunge aweze ama Kumfukuzia na Kumpata.

Na Presha kwa Moses Phiri sasa imeongezeka maradufu baada ya kuona akina John Boko na Saido Ntibanzokinza nao wanakuja na Wanafunga mno hivyo anaogopa watampita huku Yeye ndiyo akitaka kuwa Mfungaji pekee ndani ya Kikosi cha Simba SC ili aimbwe na awe Mfalme ndani ya Mioyo ya na Roho za Wanasimba ( SSC )

Wasiwasi wangu mkubwa kwa Mshambuliaji Moses Phiri Kulazimisha kurejea Uwanjani kunaweza Kusababisha hivi sasa akakamiwa Vikali zaidi na Mabeki Makatili na ama akaumizwa pakubwa au akatoneshwa na kukaa nje muda mrefu zaidi.

Na najua hata huu Ujio wa Mshambuliaji Hatari kutoka Congo DR ( kwa akina Bandeko Nangai ) aitwae Jean Baleke umemshtua na ameshtuka zaidi baada ya Kumuona Mechi ya mwisho Kafunga Goli pekee na Gumu huku pia akiupiga mwingi vile vile na kutuonyesha wana Simba SC kuwa yuko vyema na tukimuamini atatusaidia Ndani na Kimataifa.

Ifike muda hawa Wachezaji waambiwe kuwa Afya zao Kwanza na hawachezi kwa ajili yao bali wanacheza kwa Manufaa ya Klabu ya Simba SC na Nembo ya Simba Sports Club.

Mwanasaikolojia Nguli anahitajoka sana na mno ndani ya Kikosi cha Simba SC kwani nimeanza kuona Mapungufu ya baadhi ya Wachezaji wa Simba SC ambayo GENTAMYCINE nina uhakika wakipatiwa tu Thorough Counseling watakuwa bora zaidi na kuiletea Mafanikio makubwa Simba SC yangu ( yetu )

Kila la Kheri dhidi ya Coastal Union FC leo kwa Mkapa na kwa Shughuli niliyoiona kwa Kiungo mpya Mkabaji Ismael Sawadogo kama akirejesha Utimamu wake Kiuchezaji huyu ni Marc Vivien Foe aliyezaliwa upya kwani anajua Kuziba Mashimo, kupiga Pasi za uhakika, ana Nguvu, Mipira ya Juu anaicheza vyema na ni Muhuni sifa ambayo Mchezaji yoyote wa Kiungo wa Chini ( Defensive Midfielder ) anatakiwa awe nayo kama alivyokuwa nayo Patrick Viera ( Fundi ) enzi zake. Kikubwa tu Watoto Wawili wa Morogoro walioko Simba SC wasimpige tu Miba ( Wasimroge ) kwani nawajua ndani nje tabia zao.
 
Kuna wakati unaikosea sana Simba. Nadhani unatamani sana ujulikane una akili sana kuzidi wengine. Kuna wakati chill kidogo bro.

Ni wazi baada ya Simba kumuona Phiri ni mfungaji mzuri na alikuwa anaelekea kuwa na nafasi nzuri ya kuwa mfungaji bora ndiyo maana walikuwa wanamlisha mipira aipachike nyavuni. Isingekuwa majeraha yake angekuwa mbali saaaana sasa hivi na nadhani Simba wangefarijika kuona hivyo.

Kwenye ufungaji magoli kwa sasa pale Simba, hakuna mtu wa level ya Phiri, hata Boko wa sasa hamfikii na Baleke bado hatujamuona vya kutosha kumlinganisha naye. Na mimi ningekuwa pale benchi la ufundi ningewaambia Baleke, Chama, Saido na wengine waendelee kumtafutia Phiri nafasi ya kupachika magoli.
 
My favorite player hua ni Defenders.
Kwa namna hua wanatenda KAZI Yao Kwa mbinu za kivita bila hujali chchte hata wapate adhabu Kali.

Nakumbuka ila game ya Madrid vs altetical,
Hapa morata aliwasumbua sana Hawa defender kianzia walinz WA Kati had beki WA nyuma zaid.

Na ndipo alipoa kwenye nasafi akidribo boli akimsogelea kipa aweze funga goli kilaini.

Ndipo iliosikika saiuti ya ramosi kua UA huyo mjinga.

Fede valvede alitenda KAZI yake na kumuweka chini Morata.

Kwa nmana kubwa aliisaidia tumu ingawa ilipata adhabu.

Ma huyu phiriii watamlamba kichwa siku sio nyingi nikwamba tu ligi saiv imekua na walinzi wastaarabu wanaoninyima Raha kabisa.
 
Wacha mechi ichezwe kama Phiri mgonjwa tutajua tu, mchezaji asie fit hujulikana mapema sana..
 
Nimemuona Jana tena kwa Jicho langu Kali la Kiuchunguzi na Kimaono na kugundua kuwa Mshambuliaji Moses Phiri bado hajawa Fiti kuanza Kucheza Mechi zozote zile.

Najua kuna Majuha ( Fools ) watakuja Kunishambulia na kuhoji je, Mimi GENTAMYCINE ni Daktari mpaka niseme hivi?

Majibu yangu Kwao ni kwamba Wachezaji wengi ( hasa wa Tanzania ) wa hizi Timu Kubwa hudiriki hata Kuwahonga Madaktari wa Timu ili Wadanganye na waseme Wamepona ili Wacheze na wakipangwa huwapa 10% ya ama Posho zao au Mishahara yao.

Kuna Golikipa wa Timu Moja Kubwa ilipokaribia Kariakoo Derby ambayo alishaichungulia kwa Mganga wake mkubwa huko Kwao Mang'ula Mkoani Morogoro akachonga Dili na Daktari wa Timu yake kuwa ameumia Dressing Room hivyo hatoweza Kucheza na akapangwa Kipa Mlokole japo Mkewe ni Mshirikina sana na Kufungwa hiyo Derby Kubwa.

Kinachomgharimu na Kumtesa Moses Phiri ni Ufungaji Bora na kwanini apitwe na Fiston Mayele wa Yanga SC hivyo anataka Kulazimisha kwa kila namna ili acheze na afunge aweze ama Kumfukuzia na Kumpata.

Na Presha kwa Moses Phiri sasa imeongezeka maradufu baada ya kuona akina John Boko na Saido Ntibanzokinza nao wanakuja na Wanafunga mno hivyo anaogopa watampita huku Yeye ndiyo akitaka kuwa Mfungaji pekee ndani ya Kikosi cha Simba SC ili aimbwe na awe Mfalme ndani ya Mioyo ya na Roho za Wanasimba ( SSC )

Wasiwasi wangu mkubwa kwa Mshambuliaji Moses Phiri Kulazimisha kurejea Uwanjani kunaweza Kusababisha hivi sasa akakamiwa Vikali zaidi na Mabeki Makatili na ama akaumizwa pakubwa au akatoneshwa na kukaa nje muda mrefu zaidi.

Na najua hata huu Ujio wa Mshambuliaji Hatari kutoka Congo DR ( kwa akina Bandeko Nangai ) aitwae Jean Baleke umemshtua na ameshtuka zaidi baada ya Kumuona Mechi ya mwisho Kafunga Goli pekee na Gumu huku pia akiupiga mwingi vile vile na kutuonyesha wana Simba SC kuwa yuko vyema na tukimuamini atatusaidia Ndani na Kimataifa.

Ifike muda hawa Wachezaji waambiwe kuwa Afya zao Kwanza na hawachezi kwa ajili yao bali wanacheza kwa Manufaa ya Klabu ya Simba SC na Nembo ya Simba Sports Club.

Mwanasaikolojia Nguli anahitajoka sana na mno ndani ya Kikosi cha Simba SC kwani nimeanza kuona Mapungufu ya baadhi ya Wachezaji wa Simba SC ambayo GENTAMYCINE nina uhakika wakipatiwa tu Thorough Counseling watakuwa bora zaidi na kuiletea Mafanikio makubwa Simba SC yangu ( yetu )

Kila la Kheri dhidi ya Coastal Union FC leo kwa Mkapa na kwa Shughuli niliyoiona kwa Kiungo mpya Mkabaji Ismael Sawadogo kama akirejesha Utimamu wake Kiuchezaji huyu ni Marc Vivien Foe aliyezaliwa upya kwani anajua Kuziba Mashimo, kupiga Pasi za uhakika, ana Nguvu, Mipira ya Juu anaicheza vyema na ni Muhuni sifa ambayo Mchezaji yoyote wa Kiungo wa Chini ( Defensive Midfielder ) anatakiwa awe nayo kama alivyokuwa nayo Patrick Viera ( Fundi ) enzi zake. Kikubwa tu Watoto Wawili wa Morogoro walioko Simba SC wasimpige tu Miba ( Wasimroge ) kwani nawajua ndani nje tabia zao.
certified f..l
 
Usisahau hata mashabiki wanamhitaji huyo mwanasakilojia sababu kuna kiongozi wao alisema wanaugua umbumbumbu hapo msimbazi.
 
Back
Top Bottom