Fahamu haya kuhusu mpira wa miguu

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Mpira wa miguu (pia soka au kandanda ) ni mchezo unaochezwa na jumla ya wachezaji ishirini na wawili katika timu mbili, kila timu ikiwa na wachezaji kumi na mmoja. Lengo hasa la mchezo huu ni wachezaji kuumiliki mpira kwa kutumia miguu na kufunga goli, yaani kuuingiza mpira katika wavu wa wapinzani mara nyingi zaidi.

Matumizi ya mikono ni marufuku isipokuwa kwa mlinda mlango katika eneo maalumu na wakati wa kurudisha mpira
baada ya kutoka nje ya uwanja.


HISTORIA YA MPIRA

Mchezo huu ulianza China, kwani huko kulikua na mchezo unaofanana na mpira wa miguu unaitwa tsu-tsu katika karne ya nne mwaka wa 1410 wataliani walicheza mchezo huo, mwaka wa 1585 waengereza nao waliucheza.

Mwaka wa 1803 ikaanzishwa jumuiya ya mpira wa miguu huko Uingereza na ikawa huko hadi mwaka wa 1930. Mwaka wa 1904 ulianzishwa huko paris umoja wa dunia wa mpira wa miguu na kufika sasa hivi umoja huo una zaidi ya nchi 130. Chini ya uongozi wa Paris yalioazishwa mashindano ya kombe ya la dunia la kwanza 1930 huko Montevideo Uruguay, hii ni baada kuangushwa Khilafah ya Kiislamu na mwenzi 3 1924.

Mpira wa miguu uliletwa kupumbaza ummah wa Kiislamu na kutofikiria kuleta mageuzi pamoja na kuwamakinishia waislamu fikra za kizalendo.


JOHAN CRUYFF


Johan Cruyff alikuwa wa kwanza kuweza kutumia falsafa ya Total Football iliyoundwa na Rinus Michels, na anajulikana kama mchezaji bora wa soka kuwahi kutokea katika historia ya soka. Katika miaka ya 1970 mpira wa Uholanzi uliibuka na kuwa na ushindani kwenye michuano.

Cruyff aliisaidia Uholanzi kufika kwenye fainali za kombe la Dunia mwaka 1974 na kupewa mpra wa dhahabu kama zawadi kwa mchezaji bora kwenye mashindano. Kwenye fainali ya 1974 alifanya mashambulizi yaliyoitwa "Cruyff Turn" ambao ni mfumo unaotumika kwa sasa. Katika ngazi ya klabu alianza kucheza na Ajax, na alishinda Eredivisie mara nane, European Cups mara tatu na Intercontinental Cup mara moja.

Mwaka 1973 alihamia Barcelona kwa kuvunja rekodi ya usajili, msimu wake wa kwanza alishinda taji la La Liga na kuitwa mchezaji bora wa Ulaya wa mwaka. Baada ya kustaafu mwaka 1984, Cruyff alikuwa kocha mwenye mafanikio makubwa wa Ajax na baadaye Barcelona baadaye alikuwa mshauri wa klabu zote mbili.


Baadhi ya wachezaji ambao wamepoteza maisha uwanjani kwa matatizo mbalimbali hasa wanaotoka katika bara la Afrika. wengi wakizitumikia timu zao katika mabara tofauti tofauti.

1. Papy Faty kutoka Burundi


Alizaliwa 18 September 1990 na kupoteza maisha 25 April 2019 akiwa na umri wa miaka 28.

Papy Faty nyota wa zamani wa Bidvest na timu ya taifa ya Burundi amefariki dunia baada ya kuanguka uwanjani akiwa na klabu yake ya Malanti Chiefs F.C. ya Eswatini (zamani Swaziland). Alifariki dunia kwenye mchezo wa ligi ya Eswatini leo baada ya kuanguka na kupoteza fahamu akiwa uwanjani.

Kitu ambacho kinawahuzunisha wengi ni kwamba, miaka mitatu iliyopita alishauriwa na madaktari kustaafu mpira kwa sababu ya matatizo ya moyo, aliwahi kupoteza fahamu mara kadhaa akiwa na klabu ya Bidvest, lakini mara moja ilikuwa kwenye mechi.

Aliacha soka kwa muda lakini alirejea uwanjani na alizungumza wazi kupitia gazeti moja la Afrika Kusini na kukiri wazi kuwa aliamua kukiuka ushauri wa madaktari na kuamua kurudi kucheza mpira wa miguu kwa sababu hayo ndiyo maisha yake. Atakumbukwa kama mmoja wa wachezaji ambao waliwahi kuonesha uwezo mkubwa lakini kwa bahati
mbaya aliichezea timu ya taifa lake (Burundi) mchezo mmoja tu.

2. Patrick Ekeng kutoka Cameroon

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alipoteza fahamu dakika saba tu baada ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine katika timu yake ya Dinamo Bucharest katika mji mkuu wa taifa hilo, Bucharest.

Hakuwa amegusana wala kukaribiana na mchezaji mwingine alipoanguka uwanjani. Matabibu walimkimbiza hospitalini ambako madaktari walijaribu kumfufua kwa zaidi ya saa moja bila kufaulu. Kwa muda wa miaka michache iliyopita wachazaji kadhaa Waafrika wamefariki walipokuwa wakicheza uwanjani.

3. Marc Vivien Foe kutoka Cameroon

Marc Vivien Foe alikufa kutokana na mshituko wa moyo katika mchezo dhidi ya Colombia na kifo chake kimechukuliwa kama fundisho kwa wadau wa mpira wa miguu duniani kuhakiki afya za wachezaji na hasa vipimo vya moyo kila wakati.Jambo hilo bado linasugua vichwa vya watafiti wa afya na bado hakuna majibu ya moja kwa moja ya kwa nini wachezaji wanakufa viwanjani kwa matatizo ya moyo ilhali wanapimwa afya zao ipasavyo. Wengi bado wanakumbuka mkasa uliompata mchezaji wa ligi kuu ya England Fabrice Muamba aliyezimia kwa siku kadhaa baada ya kuanguka uwanjani kutokana na matatizo ya moyo, Muamba alisalimika na amejiuzulu kucheza mpira kabisa licha ya umri wake mdogo wa miaka 23.

Tarehe 26 mwezi Juni mwaka 2013,ilitimia miaka kumi tangu kufariki kwa mchezaji wa Kimataifa wa Cameroun Marc Vivien Foe, aliye anguka uwanjani wakati wa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FIFA la Mabara mwaka 2003 nchini Ufaransa.

4. Cheick Tioté kutoka Ivory Coast.

Alianza uchezaji wake wa soka ya kulipwa Ubelgiji akiwa na klabu ya Anderlecht mwaka 2005 kabla ya kuhamia FC Twente ya Uholanzi ambapo alicheza mechi 86 na kushinda taji la ligi ya Eredivisie msimu wa 2009-10 chini ya meneja Steve McLaren. Tiote, ambaye ni kiungo wa kati mkabaji, kisha alihamia Newcastle mwaka 2010 kwa £3.5m.

Je, wajua?

Mara ya mwisho Liverpool kuchukua ubingwa wa Uingereza ilikuwa siku ya Jumamosi, Aprili 28, 1990 baada ya kuifunga
QPR goli 2-1.

Man United ilikuwa imeshatwaa ubingwa wa ligi mara 7 tu na Liverpool mara 18. Lakini leo hii Man United keshatwaa mara 20 na Liverpool bado hizo hizo 18.

TANZANIA

Timu maarufu kwenye ligi ya Tanzania ukiachia Simba na Yanga, zilikuwa Pilsner, Sigara, Tukuyu Stars, Lipuli, Ushirika
Moshi, Pamba, Nyota Nyekundu, Milambo, Reli, MECCO, Coastal Union, Pan African, Ujenzi Rukwa na RTC Kagera.

Je, wajua?

Ndege haziruhusiwi kupita juu ya makazi ya mchezaji bora duniani Lionel Messi kwa mujibu wa sheria za jiji la
Barcelona?

Hii haitokei dunia kote lakini fahamu kuwa fanya ufanyavyo kamwe huwezi kupita na ndege juu ya nyumba ya mchezaji bora kabisa duniani wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi.

Hivyo basi ndege kutoruhusiwa kupita kwenye anga hiyo kamwe hakuhusiani na uwepo wa mchezaji huyo maarufu duniani bali ni kutokana na sheria ambazo zimewekwa, ndege kutopita maeneo hayo ambayo ni Gava Mar, Viladecans na Castelldefels yaliopo karibu na fukwe za bahari ili kuepusha uchafuzi wa mazingira.

Zipo baadhi ya sehemu duniani ndege kamwe haziruhusiwi kupita ambapo kwa kimombo wanaita ‘flight restriction zone’ na baadhi yake ni kama Washington, D.C. Mecca nchini Saud Arabia na baadhi ya maeneo nchini Malaysia.

Lionel Messi huishi kwenye halmasahauri ya Castelldefels jijini Barcelona nchini Hispania na ndege haziwezi kupita kwenye maene yake ni kutokana na sababu hizo za kimazingira kwa mujibu wa sheria za Barcelona.

Eneo hili la Castelldefels hulindwa zaidi katika kuhakikisha linatunzwa mazingira yake kwakuwa lina uoto mwingi wa asili na hivyo kupelekea sheria za jiji la Barcelona kupiga marufuku ndege, kwasababu husababisha uchafuzi wa mazingira (Noise pollution) kwa viumbe hai wa porini wanaopatikana maeneo hayo.

Kwenye maeneo hayo ndege haziruhusiwi kabisa kupita pembezoni mwa fukwe za bahari mahala ambapo nyumba ya Messi pamoja na watu wengine maarufu wanaishi na sheria hiyo huwasaidia yeye na mastaa wengi mahala hapo kutobuguziwa na makelele ya ndege kupita angani ambapo ni kilomita 10 kufikia uwanja ulipo.

Kunapata umbali wa maili 12 kutoka Castelldefels hadi kufika kwenye uwanja wa Barcelona, Nou Camp huku wachezaji wengi wa timu hiyo wakiwa wamenunua nyumba zao za kuishi maeneo hayo.

Kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya watu hasa lilipokuja wazo la kutaka kuupanua uwanja wa ndege uliyo umbali wa kilomita 10 kutoka kwenye Manispaa hiyo na kushindikana wakati rais wa mashirika ya ndege Kimataifa ‘International Airlines Group (IAG),’ Javier Sanchez-Prieto aliposema ni karibu na makazi ya Messi.

Je, wajua?

31/1/2020 Mfalme wa Instagram afikisha followers Milion 200. Cristiano Ronaldo anakuwa mtu wa kwanza kufikisha Followers 200M kwenye mtandao wa Instagram.

Je, wajua?

SIMBA ILINUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

Je wajua?

Mwanasoka mkongwe wa brazil Pele, alijipatia jina hilo la utani lenye maana katika lugha ya kibrazil na kireno “ miguu sita” (six feet), kutokana na kuwa na vidole sita katika kila mguu.

Je wajua?

Mnamo mwaka 1998 Radi iliua wachezaji wote kumi na moja (11) wa timu moja na kuacha wachezaji wa timu pinzani wakati wa mchezo nchini DRC na kudhuru watazamaji wapatao thelathini.

Je, wajua?

Ismail Mrisho Khalfan alifariki dunia 4/12/2016 baada ya kuanguka uwanjani alipogongana na beki wa Mwadui FC katika michuano ya Ligi ya Vijana U20.

Je, wajua?

Mrtinho Eduardo Orige kutoka Brazil ndio mchezaji pekee kuchezea mpira kwa muda mrefu zaidi duniani! Alichezea mpira kwa muda wa masaa 19.5, alivunja record hiyo mnamo mwaka 2003.

Je wajua?

Pele alipokwenda Nigeria kucheza soka katika mchezo wa hisani mnamo mwaka 1967, pande mbili zinapigana vita, zilikubaliana kusimamisha vita kwa muda wa masaa 48.

Je, wajua?

Mnamo mwaka 1964 simu aliyopokea mwamuzi wa mchezo (refa) akiwa uwanjani huko nchini Peru ilisababisha vurugu
iliyopelekea watu mia tatu (300) kufariki. 6.Washabiki wa soka nchini Columbia waingia na jeneza uwanjani la mshabiki mwenzao aliyeuawa kwa kupigwa risasi siku ya kuwania kuingia fainali akiwa na umri wa miaka17. Washabiki hao waliingia nae siku ya fainali.
 
Stendi ya mabasi ya Mikoani ilikuwa Kisutu na Mnazi Mmoja
Timu maarufu kwenye ligi ya Tanzania ukiachia Simba na Yanga, zilikuwa Pilsner, Sigara, Tukuyu Stars, Lipuli, Ushirika Moshi, Pamba, Nyota Nyekundu, Milambo, Reli, MECCO, Coastal Union, Pan African, Ujenzi Rukwa na RTC Kagera.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom