Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
161,679
2,000
Naomba nisipingane na asili ambayo inalandana hata mitazamo ya kiimani kwamba ALIYE NACHO HUONGEZEWA! Kuna uwezekano mkubwa mabepari walijifunzia huku.

Matukio haya mawili ni ya ma rais wetu wastaafu ambao kupitia kwao weekend iliyopita walisababisha mijadala mipana mitandaoni

1. TUKIO LA KWANZA
Aliyekuwa rais wa pili wa Tanzania baada ya uhuru wa Tanganyika mzee Ali Hassan Mwinyi alizindua kitabu cha maisha yake..! Hili si tukio la dharura ni tukio lililoandaliwa kwa muda mrefu na kwa kuzingatia protokali mgeni rasmi si mwingine bali ni rais aliyeko madarakani.

Mipango ya Mungu si ya mwanadamu hivyo inawezekana kabisa aliyekuwa kaandaliwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hili kubwa ni aliyekuwa rais wa awamu ya tano hayati Pombe John Magufuli na inawezekana kabisa na zawadi ya mgeni rasmi kwenda kwa mhusika ilikuwa imeshaandaliwa!

Kudra za Mwenyezi Mungu zikamuangukia aliyekuwa makamu wa rais kuwa rais kamili wa Tanzania baada ya kifo cha maradhi cha mtangulizi wake. Na huyu ndio kawa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha mzee Mwinyi.

Kilicholeta mjadala ni ukarimu wa zawadi aliyotunukiwa na rais Samia Hassan Suluhu..zawadi ya gari la kifahari la bei ghali aina ya Mercedes Benz linalofikia kiasi cha Tsh milion 250 kabla ya usafiri na usajili na kodi.

Lawama zimeenda kwa mama kwa matumizi mabaya ya pesa za wananchi. Lakini pengine si kosa lake inawezekana kabisa ni kitu kilichokuwa kimeshapangwa kitambo.

Wengine wamesema sababu iliyotolewa haikidhi ama angetafutiwa walau gari la bei ndogo zaidi... Ama la angepewa zawadi nyingine... Waswahel wanasema usimuingilie aliyepewa kapewa! Mzee mwinyi hana shida ya chochote ana kila kitu cha kimaisha katika level ya kibinadamu. Zawadi aliyopewa ni bakshish tu. Aliye nacho huongezewa! Tafakuri yangu kwenye hili tukio ni kile kitendo cha mzee Mwinyi kugoma kupokea zawadi ile! (Tetesi) Pengine kaona ni kufuru sasa tena ukizingatia huu ni mwezi wa toba kwa imani yake!

2. TUKIO LA PILI
Mzee Jakaya Kikwete rais mstaafu wa awamu ya nne kukabidhiwa nyumba aliyojengewa na serikali. Hii ni kwa marais wote wastaafu wamefanyiwa hivyo! Kwa picha tu za nje si nyumba ya kitoto bali ni jumba kubwa la kifahari.

Hili nalo si tukio la dharura ni tukio lililokuwa limepangwa kitambo na kwa muktadha uleule mgeni rasmi angekuwa JPM kama angekuwa hai!

Tafakuri yangu kwenye hili! Hivi ni kweli kabisa JK anashida na nyumba? Tena lijumba kubwa kama lile? Lakini tukirejea kwenye ile kanuni ya asili ya aliyenacho huongezewa basi kauli inakata na mjadala unaisha.

JK pia ana kitabu cha maisha yake. Sina kumbukumbu kama alishakizindua na katika hafla ile alipewa zawadi gani na mgeni rasmi!

Mzee Mwinyi kwa tetesi ni kwamba kaikataa zawadi nzuri ya gari la kifahari .. Sina hakika kama atakapokabidhiwa jumba lake la kifahari nalo atalikataa. Nasema sina hakika.

Viongozi wakuu wa nchi ni viongozi ambao hulelewa na serikali zao mpaka kifo. Na kwa viongozi wetu wa Afrika huingia madarakani wakiwa watupu na kutoka wakiwa na ukwasi wa kutisha wao na ndugu zao na familia zao. Lakini bado katika kulelewa huko na ukwasi huo bado huongezewa bakshish ya hiki na kile

Yaani ni kama vile wananyang'anya kile kidogo ambacho kingewasaidia wanyonge fukara na maskini wa Taifa hili. Na hawajali ama macho yao yamejaa upofu kuyaona haya. Ni kilevi cha madaraka na kupata hupofusha mpaka weledi wetu.
 

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,228
2,000
Gari sio lolote kulinganisha na mchango wa Mzee Mwinyi aliyekuwa ameachiwa nchi na Hayati Nyerere ikiwa hoi kiuchumi.

Wenzangu na mimi tuliokuwa tunaelewa nini kinaendelea duniani miaka ile ya 1980 mwanzoni tutakumbuka kula ugali wa Yanga na yale maduka ya kaya, kila nyumba inakuwa na daftari la bidhaa za kununuliwa hapo dukani. Mwinyi alifanya mengi mpaka hali ikaanza kuwa njema.

Zawadi ya Nyumba ya Mzee Kikwete sio lolote kulinganisha na miradi aliyoianzisha na yenye kuendelea kuleta mabadiliko ya kijamii.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na wagonjwa wa moyo wanaotibiwa na kupona pale MOI.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na wasafiri wote wanaotumia mwendo kasi asubuhi mchana na jioni.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na namna umeme wa REA unavyoibadilisha kabisa Tanzania kiuchumi.

Umaskini wa kichwani ni mbaya sana, kwani siku zote mtu analalamika mpaka anasahau kuwa kwa kufanya hivyo anamkufuru Mungu aliyemjalia vipaji vingi.
 

Jiang Ze Dong

JF-Expert Member
May 28, 2020
285
1,000
Aliye nacho huongezewa hii ni kanuni ya kiasili ya maisha hivyo hakuna haja ya kulalama huku maisha yakikupita mbio..Viongozi wanaitendea haki asili.. Wananchi wawe wapole tu. Its a game of fierce fight. Survival of the fittest!
Nakumbuka mzee mwinyi kashapewa nyumba yake kipindi Jpm yupo hai lakin nyumba ya JK ilikua haijamaliziwa ujenzi.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
161,679
2,000
Kuna vitu umeviruka kwa makusudi ama kwa bahati mbaya! Aya ya kwanza ya mada yangu inaweza kukupa mwanga wa kile nilichokusudia kukiandika halafu aya ya mwisho ni mtazamo binafsi katika ujumla wake.

BTW hawa ni wastaafu ambao wakati wa kustaafu hupewa kila kitu zikiwemo nyumba na magari na huishi kwa kutunzwa na serikali mpaka kifo!

Kubwa kuliko yote hawa ni watumishi wa umma kama watumishi wengine. Zawadi kubwa kubwa za kuja kupeana baadae hazina budi kuhojiwa na kutupa tafakuri hata kama tutapewa majina mabaya.
 

Namba7

JF-Expert Member
Nov 12, 2020
554
1,000
Aliye nacho huongezewa hii ni kanuni ya kiasili ya maisha hivyo hakuna haja ya kulalama huku maisha yakikupita mbio..Viongozi wanaitendea haki asili.. Wananchi wawe wapole tu. Its a game of fierce fight. Survival of the fittest!
Tuache mawazo ya kifukara, Benz silolote ukilinganisha na mchango wa mstaafu rais katika nchi, hawa watu hukutana na madhila mengi, hutengwa na familia zao kwa miaka 10 kutokana na majukumu, hawana uhuru kamili wawapo madarakani, tusiangalie bakshishi hizi pekee tugeukie na majukumu na madhila yao.
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,777
2,000
Yaani ni kama vile wananyang'anya kile kidogo ambacho kingewasaidia wanyonge fukara na maskini wa Taifa hili...!!! Na hawajali ama macho yao yamejaa upofu kuyaona haya. Ni kilevi cha madaraka na kupata hupofusha mpaka weledi wetu..!!!
Mkuu, hivi unajua kadri unayofahamu mengi ya nchi ndivyo unavyokuwa katika hatari ya kuwindwa na maadui wa taifa? Waliotayari kufa kwa ajili ya kuitetea nchi ndio wanaofaa kuiongoza.

Viongozi wastaafu hutunzwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.

Acha kufananisha viongozi waandamizi na wananchi wa kawaida. Katika nchi yoyote ni lazima kuwe na kundi dogo litakalowaongoza wengine ndio maana hapa Tanzania kundi hilo linakaa maeneo kama Oysterbay na Masaki.

Sio kwamba kukaa huko ni kwa sababu hawawapendi wale wa Mbagala na Tandale, hapana. Hizo ni assets za taifa mzee baba. Kuna watu/wataalam wakifa nchi inayumba. Hata huko USA wapo watu kama hawa. Fuatilia kisa cha contractor wa Marekani aliyeuwawa Iraq ndio utajua kwamba binadamu ni sawa lakini sio sawa sawa.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
161,679
2,000
Tuache mawazo ya kifukara, benz silolote ukilinganisha na mchango wa mstaafu rais katika nchi, hawa watu hukutana na madhila mengi, hutengwa na familia zao kwa miaka 10 kutokana na majukumu, hawana uhuru kamili wawapo madarakani, tusiangalie bakshishi hizi pekee tugeukie na majukumu na madhila yao.
Kumbuka si kwamba anastaafu sasa. Alishastaafu na kupewa kila alichopaswa kupewa na bado kwenye makala yangu nimeweka wazi aya ya kwanza nini maana ya kupata hizi bakshish.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
161,679
2,000
Naona umepotoka kabisa na pengine hujaelewa kabisa nilichoandika. Tafadhali rudia kusoma tena.

JK tangu astaafu yuko kwake Msoga au hulijui hilo? Na kama ni ishu ya usalama kwanini sasa na si wakati ule? Hivi unajua kwamba JK ana mji wake mwingine pale Moroco?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom