Wao kuhudumiwa na serikali hakufanyi zawadi wanazopewa zisiwe na maana. Wanafanya mambo mengi sana yakiwemo maamuzi magumu yenye kugusa maslahi ya mataifa makubwa.

Kumbuka kuwa hizi zawadi zote mbili zilikuwa zitolewe na Hayati JPM. Katiba ni muhimu siku zote japo sidhani kama italeta chochote kipya kwa maana ya kuwaenzi marais waliotangulia.

JPM alitoa mpaka tausi kwa marais majirani zetu. Uungwana ni jambo jema sana.
Wanafanya mambo mengi sana yakiwemo maamuzi magumu yenye kugusa maslahi ya mataifa makubwa. Mh..mmh..mmh....!!!
Hawa hawako madarakani Philipo hawa ni wastaafu tena wa kitambo ndugu yangu...!!!!
 
Wanafanya mambo mengi sana yakiwemo maamuzi magumu yenye kugusa maslahi ya mataifa makubwa. Mh..mmh..mmh....!!!
Hawa hawako madarakani Philipo hawa ni wastaafu tena wa kitambo ndugu yangu...!!!!
Mzee Kikwete alikuwa akipewa special assignments na Hayati JPM mara nyingi tu. Pia Mama ataendelea kumtumia katika awamu yake tatizo la sasa ni uviko19, vinginevyo Mzee wa Chalinze angekuwa anaendelea kufunga mikanda ndani ya ndege akitabasamu kwa wale wahudumu wenye sura laini laini.

Mwinyi amekuwa mtu mzima sana, miaka 96 ni mingi sana, vinginevyo hata yeye angekuwa anapewa majukumu fulani ya kumsaidia Rais Samia.

Rais anabakia na heshima yake ile ile hata baada ya kustaafu hivyo muda wowote anaweza kutumiwa kwa faida ya taifa lake.
 
Wao kuhudumiwa na serikali hakufanyi zawadi wanazopewa zisiwe na maana. Wanafanya mambo mengi sana yakiwemo maamuzi magumu yenye kugusa maslahi ya mataifa makubwa.

Kumbuka kuwa hizi zawadi zote mbili zilikuwa zitolewe na Hayati JPM. Katiba ni muhimu siku zote japo sidhani kama italeta chochote kipya kwa maana ya kuwaenzi marais waliotangulia.

JPM alitoa mpaka tausi kwa marais majirani zetu. Uungwana ni jambo jema sana.
Mkuu angalia zawadi aliyopewa Nyerere na hizi zinazotolewa kwa sasa. Je huko mbeleni akitokea Dictator itakuaje? Rais anaemaliza muda wake anaweza kuhakikisha anaepokea Kijiti ni Swaiba wake. Sasa Si anaweza kugawa Mbuga ya Serengeti au Mgodi Tanzanite Mirerani kama zawadi ya kumuenzi Mtangulizi wake??
 
Mkuu umekwenda mbali sana na sidhani kama tunaweza kufika huko.
 
Mzee Kikwete alikuwa akipewa special assignments na Hayati JPM mara nyingi tu. Pia Mama ataendelea kumtumia katika awamu yake tatizo la sasa ni uviko19, vinginevyo Mzee wa Chalinze angekuwa anaendelea kufunga mikanda ndani ya ndege akitabasamu kwa wale wahudumu wenye sura laini laini.

Mwinyi amekuwa mtu mzima sana, miaka 96 ni mingi sana, vinginevyo hata yeye angekuwa anapewa majukumu fulani ya kumsaidia Rais Samia.

Rais anabakia na heshima yake ile ile hata baada ya kustaafu hivyo muda wowote anaweza kutumiwa kwa faida ya taifa lake.
Sijakataa wala sikubishii ... Wapo wastaafu wengi tu hutumika hata baada ya kustaafu lakini hawatumiki bure na wala hawafanyi hisani.. Hulipwa sawia na kazi husika

Ndio heshima yao iko palepale na hilo halina shida kabisa.. Ndio maana kupitia kodi zetu tunawatunza na kuwalea kwa kila kitu wao na familia zao

Mjadala wangu ulijikita kwenye bakshish nono (fat bonus) kwenye matukio binafsi ambapo hata hivyo nimesema wazi kuwa si lawama kwakuwa aliye nacho huongezewa!
 
Mkuu angalia zawadi aliyopewa Nyerere na hizi zinazotolewa kwa sasa. Je huko mbeleni akitokea Dictator itakuaje? Rais anaemaliza muda wake anaweza kuhakikisha anaepokea Kijiti ni Swaiba wake. Sasa Si anaweza kugawa Mbuga ya Serengeti au Mgodi Tanzanite Mirerani kama zawadi ya kumuenzi Mtangulizi wake??
 
Kama nna kumbukumbu nzuri mr mshana pia jpm alisha watunuku nyumba kule masaki sasa sijajua hiz ni nyingine au zile zile??
 
Kumpa mzee ruksa "zawadi" ya Benzi siku ambayo anazindua kitabu kinachoeleza kwa nini alipindua azimio la arusha ni kumsimanga mzee wetu.

Mambo ya kupeana zawadi mali ya umma enzi za azimio la arusha ilikuwa ni mwiko, na ingekuwa sababu ya kukufanya upate shida sana wewe mtoaji na mpokeaji!
 
Kuna vitu umeviruka kwa makusudi ama kwa bahati mbaya! Aya ya kwanza ya mada yangu inaweza kukupa mwanga wa kile nilichokusudia kukiandika halafu aya ya mwisho ni mtazamo binafsi katika ujumla wake
BTW hawa ni wastaafu ambao wakati wa kustaafu hupewa kila kitu zikiwemo nyumba na magari na huishi kwa kutunzwa na serikali mpaka kifo!
Kubwa kuliko yote hawa ni watumishi wa umma kama watumishi wengine.... Zawadi kubwa kubwa za kuja kupeana baadae hazina budi kuhojiwa na kutupa tafakuri hata kama tutapewa majina mabaya
Turudi nyuma tuseme ukweli watu weusi tuna akili chafu sana
 
Kama nna kumbukumbu nzuri mr mshana pia jpm alisha watunuku nyumba kule masaki sasa sijajua hiz ni nyingine au zile zile??
Ni mwendo wa kupeana tuu...na shida iko kwenye katiba..ndio maana hawataki kabisa kusikia kuhusu katiba mpya
 
Aliye nacho huongezewa hii ni kanuni ya kiasili ya maisha hivyo hakuna haja ya kulalama huku maisha yakikupita mbio..Viongozi wanaitendea haki asili.. Wananchi wawe wapole tuu... Its a game of fierce fight.. Survival of the fittest...!

Kweli jpm alikua raisi wa wanyonge, sasa hivi tunaona maraisi wakipeana mema ya nchi huku maskin hata mia ya kula hawana, magufuli upumzike kwa amani, ulikua dictator ila uliwakumbuka maskini
 
Naomba nisipingane na asili ambayo inalandana hata mitazamo ya kiimani kwamba ALIYE NACHO HUONGEZEWA! Kuna uwezekano mkubwa mabepari walijifunzia huku.

Matukio haya mawili ni ya ma rais wetu wastaafu ambao kupitia kwao weekend iliyopita walisababisha mijadala mipana mitandaoni

1.TUKIO LA KWANZA
Aliyekuwa rais wa pili wa Tanzania baada ya uhuru wa Tanganyika mzee Ali Hassan Mwinyi alizindua kitabu cha maisha yake..! Hili si tukio la dharura ni tukio lililoandaliwa kwa muda mrefu na kwa kuzingatia protokali mgeni rasmi si mwingine bali ni rais aliyeko madarakani

Mipango ya Mungu si ya mwanadamu hivyo inawezekana kabisa aliyekuwa kaandaliwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hili kubwa ni aliyekuwa rais wa awamu ya tano hayati Pombe John Magufuli na inawezekana kabisa na zawadi ya mgeni rasmi kwenda kwa mhusika ilikuwa imeshaandaliwa!

Kudra za Mwenyezi Mungu zikamuangukia aliyekuwa makamu wa rais kuwa rais kamili wa Tanzania baada ya kifo cha maradhi cha mtangulizi wake..Na huyu ndio kawa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha mzee Mwinyi

Kilicholeta mjadala ni ukarimu wa zawadi aliyotunukiwa na rais Samia Hassan Suluhu..zawadi ya gari la kifahari la bei ghali aina ya Mercedes Benz linalofikia kiasi cha Tsh milion 250 kabla ya usafiri na usajili na kodi

Lawama zimeenda kwa mama kwa matumizi mabaya ya pesa za wananchi.. Lakini pengine si kosa lake inawezekana kabisa ni kitu kilichokuwa kimeshapangwa kitambo

Wengine wamesema sababu iliyotolewa haikidhi ama angetafutiwa walau gari la bei ndogo zaidi... Ama la angepewa zawadi nyingine... Waswahel wanasema usimuingilie aliyepewa kapewa! Mzee mwinyi hana shida ya chochote ana kila kitu cha kimaisha katika level ya kibinadamu... Zawadi aliyopewa ni bakshish tu... Aliye nacho huongezewa! Tafakuri yangu kwenye hili tukio ni kile kitendo cha mzee Mwinyi kugoma kupokea zawadi ile! (Tetesi)!!! Pengine kaona ni kufuru sasa tena ukizingatia huu ni mwezi wa toba kwa imani yake!

2.TUKIO LA PILI
Mzee Jakaya Kikwete rais mstaafu wa awamu ya nne kukabidhiwa nyumba aliyojengewa na serikali...Hii ni kwa marais wote wastaafu wamefanyiwa hivyo...! Kwa picha tu za nje si nyumba ya kitoto bali ni jumba kubwa la kifahari

Hili nalo si tukio la dharura ni tukio lililokuwa limepangwa kitambo na kwa muktadha uleule mgeni rasmi angekuwa JPM kama angekuwa hai!

Tafakuri yangu kwenye hili..! Hivi ni kweli kabisa JK anashida na nyumba? Tena lijumba kubwa kama lile? Lakini tukirejea kwenye ile kanuni ya asili ya aliyenacho huongezewa basi kauli inakata na mjadala unaisha

JK pia ana kitabu cha maisha yake.. Sina kumbukumbu kama alishakizindua na katika hafla ile alipewa zawadi gani na mgeni rasmi!

Mzee Mwinyi kwa tetesi ni kwamba kaikataa zawadi nzuri ya gari la kifahari .. Sina hakika kama atakapokabidhiwa jumba lake la kifahari nalo atalikataa... Nasema sina hakika.

Viongozi wakuu wa nchi ni viongozi ambao hulelewa na serikali zao mpaka kifo... Na kwa viongozi wetu wa Afrika huingia madarakani wakiwa watupu na kutoka wakiwa na ukwasi wa kutisha wao na ndugu zao na familia zao...Lakini bado katika kulelewa huko na ukwasi huo bado huongezewa bakshish ya hiki na kile

Yaani ni kama vile wananyang'anya kile kidogo ambacho kingewasaidia wanyonge fukara na maskini wa Taifa hili...!!! Na hawajali ama macho yao yamejaa upofu kuyaona haya... Ni kilevi cha madaraka na kupata hupofusha mpaka weledi wetu..!!!
Mwinyi alishapokea jumba Lake

Jumba la Mwinyi ni nzuri mara 100 ya kikwete

Mwinyi alikabidhiwa nyumba na JPM

Ya kikwete ilikuwa haijaisha na JPM aliwawakia wajenzi kuwa iishe mapema
 
Mwinyi alishapokea jumba Lake

Jumba la Mwinyi ni nzuri mara 100 ya kikwete

Mwinyi alikabidhiwa nyumba na JPM

Ya kikwete ilikuwa haijaisha na JPM aliwawakia wajenzi kuwa iishe mapema
Kanuni ya asili aliyojitungia mwanadamu pengine inasema ALIYE NACHO HUONGEZEWA! wanaitendea haki hii kauli..!!! Lakini bila TAFAKURI
 
Back
Top Bottom