JK tangu astaafu yuko kwake Msoga au hulijui hilo? Na kama ni ishu ya usalama kwanini sasa na si wakati ule? Hivi unajua kwamba JK ana mji wake mwingine pale Moroco?
Mama yangu mkubwa ni mwalimu alistaafu mwaka 2019 akiwa katika nyumba yake Tabora ila baada ya kustaafu serikali ikampa pesa zake za mafao kwa mujibu wa sheria. Sasa mwalimu huyu ana tofauti gani na mfano wa mzee JK ulioutoa hapo juu?
 
Hebu soma ulichoandika hapa kama kinaakisi nilichoandika mimi

Mkuu, hivi unajua kadri unayofahamu mengi ya nchi ndivyo unavyokuwa katika hatari ya kuwindwa na maadui wa taifa? Waliotayari kufa kwa ajili ya kuitetea nchi ndio wanaofaa kuiongoza.

Viongozi wastaafu hutunzwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.

Acha kufananisha viongozi waandamizi na wananchi wa kawaida. Katika nchi yoyote ni lazima kuwe na kundi dogo litakalowaongoza wengine ndio maana hapa Tanzania kundi hilo linakaa maeneo kama Oysterbay na Masaki
 
Mkuu "Infantry Soldier"mtoa mada (Mshana Jr) hakuwa na maana hiyo unayofikiria wewe. Yeye kaeleza wazi kuwa Wastaafu wale wanalelewa na Serikali kwa maisha yao yote yaliyosalia Duniani pamoja na wenzi wao. Nyumba na magari wanayoyatumia hivi sasa yanahudumiwa na Serikali kwa 100%.

Tukiachilia mbali magari watakapohamia kwenye makazi yao mapya bado huko yataendelea kuhudumiwa. Hata zile nyumba za awali zitaendelea kuhudumiwa na Serikali. Kwako wewe huoni ni mzigo usio wa lazima kwa nchi kama hii yenye hospt zisizokuwa na madawa? Na shule zisizokuwa na madawati??

Kwa tafsiri yangu mimi hii ni namna ya Kiongozi aliyeko Madarakani kuwaziba midomo Watangulizi wake ili wasimkosoe pale anapoboronga. Nasema hivyo kwasababu nyumba hizi hazina uwiano kwenye dhamani bali hutegemea utashi wa Rais aliyeko Madarakani. "Katiba Mpya ni Muhimu".
 
Chokochoko zenu msingi wenu ni roho za wivu.
Hata asingepewa Mwinyi still usingezifaidi kwa namna yoyote
Ungekuwa Namba1 ungeelewa haraka, ila sasa itabidi tukumegee kidogo kwa fumbo, "Inawezekana Mkeo au Mumeo anatumika pia kwa mtu mwingine bila wewe kujua hata kuhisi tu kuwa anatumika hujui, ikiwa hivyo ujue hali hiyo haiwezi kukuathiri, sasa ikifika time ukaona, ukasikia mwenyewe, shida ndipo inapooanzia"

Anachokisema Mshana Jr ni juu ya hawa viongozi kujitungia sheria za kujilimbikizia mali ilihali hawana shida ukilinganisha na sehemu kubwa ya watu wasio na mali! Viongozi wanapaswa kutathmini kwa nini wananchi wame-react kiasi hicho na ikiwapendeza basi wafanye utaratibu wa kubadili sheria zinazowafanya walalamikiwe kwa issue kama hizo!
 
Hebu soma ulichoandika hapa kama kinaakisi nilichoandika mimi

Mkuu, hivi unajua kadri unayofahamu mengi ya nchi ndivyo unavyokuwa katika hatari ya kuwindwa na maadui wa taifa? Waliotayari kufa kwa ajili ya kuitetea nchi ndio wanaofaa kuiongoza.

Viongozi wastaafu hutunzwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.

Acha kufananisha viongozi waandamizi na wananchi wa kawaida. Katika nchi yoyote ni lazima kuwe na kundi dogo litakalowaongoza wengine ndio maana hapa Tanzania kundi hilo linakaa maeneo kama Oysterbay na Masaki
Basi tusiende mbali mkuu. Have a wonderful day brother.
 
Mkuu mtoa mada hakuwa na maana hiyo unayofikiria wewe. Yeye kaeleza wazi kuwa Wastaafu wale wanalelewa na Serikali kwa maisha yao yote yaliyosalia Duniani pamoja na wenzi wao. Nyumba na magari wanayoyatumia hivi sasa yanahudumiwa na Serikali kwa 100%.

Tukiachilia mbali magari watakapohamia kwenye makazi yao mapya bado huko yataendelea kuhudumiwa. Hata zile nyumba za awali zitaendelea kuhudumiwa na Serikali. Kwako wewe huoni ni mzigo usio wa lazima kwa nchi kama hii yenye hispt zisizokuwa na madawa? Na shule zisizokuwa na madawati??

Kwa tafsiri yangu mimi hii ni namna ya Kiongozi aliyeko Madarakani kuwaziba midomo Watangulizi wake ili wasimkosoe pale anapoboronga. Nasema hivyo kwasababu nyumba hizi hzina uwiano kwenye dhmani bali hutegemea utashi wa Rais aliyeko Madarakani. "Katiba Mpya ni Muhimu".
Ungekuwa Namba1 ungeelewa haraka, ila sasa itabidi tukumegee kidogo kwa fumbo, "Inawezekana Mkeo au Mumeo anatumika pia kwa mtu mwingine bila wewe kujua hata kuhisi tu kuwa anatumika hujui, ikiwa hivyo ujue hali hiyo haiwezi kukuathiri, sasa ikifika time ukaona, ukasikia mwenyewe, shida ndipo inapooanzia"

Anachokisema Mshana Jr ni juu ya hawa viongozi kujitungia sheria za kujilimbikizia mali ilihali hawana shida ukilinganisha na sehemu kubwa ya watu wasio na mali! Viongozi wanapaswa kutathmini kwa nini wananchi wame-react kiasi hicho na ikiwapendeza basi wafanye utaratibu wa kubadili sheria zinazowafanya walalamikiwe kwa issue kama hizo!
Naona wapinga hoja hawajasoma na kuelewa nilichoandika
Hawa wastaafu ni watumishi wa umma ambao tulishamalizana nao kitambo kabisa.. Na kwa level yao mpaka sasa sisi ndio tunawahudumia kupitia kodi zetu...
Nimezungumzia BAKSHISH wanayopewa ..bakshish ni bonus... Bonus ni ziada... Na kama ni ziada je lazima iwe nono? Ndio maana Mzee Mwinyi kaikataa kwakuwa roho inamsuta sana
 
Mkuu mtoa mada hakuwa na maana hiyo unayofikiria wewe. Yeye kaeleza wazi kuwa Wastaafu wale wanalelewa na Serikali kwa maisha yao yote yaliyosalia Duniani pamoja na wenzi wao. Nyumba na magari wanayoyatumia hivi sasa yanahudumiwa na Serikali kwa 100%.

Tukiachilia mbali magari watakapohamia kwenye makazi yao mapya bado huko yataendelea kuhudumiwa. Hata zile nyumba za awali zitaendelea kuhudumiwa na Serikali. Kwako wewe huoni ni mzigo usio wa lazima kwa nchi kama hii yenye hospt zisizokuwa na madawa? Na shule zisizokuwa na madawati??

Kwa tafsiri yangu mimi hii ni namna ya Kiongozi aliyeko Madarakani kuwaziba midomo Watangulizi wake ili wasimkosoe pale anapoboronga. Nasema hivyo kwasababu nyumba hizi hazina uwiano kwenye dhamani bali hutegemea utashi wa Rais aliyeko Madarakani. "Katiba Mpya ni Muhimu".
Wao kuhudumiwa na serikali hakufanyi zawadi wanazopewa zisiwe na maana. Wanafanya mambo mengi sana yakiwemo maamuzi magumu yenye kugusa maslahi ya mataifa makubwa.

Kumbuka kuwa hizi zawadi zote mbili zilikuwa zitolewe na Hayati JPM. Katiba ni muhimu siku zote japo sidhani kama italeta chochote kipya kwa maana ya kuwaenzi marais waliotangulia.

JPM alitoa mpaka tausi kwa marais majirani zetu. Uungwana ni jambo jema sana.
 
Unyonge wa wananchi ni pale ambapo serikali ikikosea au kuwakandamiza ni kuwa hawana lolote la kufanya.

Serikali huona haki ya wananchi ni kama fadhila na maendeleo kwa wananchi tena kwa kodi zetu wenyewe ni kama hisani tu.

Serikali haishauriki, serikali mufilisi. Viongozi wa serikali wanajiona miungu watu, hawafikirii wengine.

I'm out.
 
Gari sio lolote kulinganisha na mchango wa Mzee Mwinyi aliyekuwa ameachiwa nchi na Hayati Nyerere ikiwa hoi kiuchumi.

Wenzangu na mimi tuliokuwa tunaelewa nini kinaendelea duniani miaka ile ya 1980 mwanzoni tutakumbuka kula ugali wa Yanga na yale maduka ya kaya, kila nyumba inakuwa na daftari la bidhaa za kununuliwa hapo dukani. Mwinyi alifanya mengi mpaka hali ikaanza kuwa njema.

Zawadi ya Nyumba ya Mzee Kikwete sio lolote kulinganisha na miradi aliyoianzisha na yenye kuendelea kuleta mabadiliko ya kijamii.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na wagonjwa wa moyo wanaotibiwa na kupona pale MOI.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na wasafiri wote wanaotumia mwendo kasi asubuhi mchana na jioni.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na namna umeme wa REA unavyoibadilisha kabisa Tanzania kiuchumi.

Umaskini wa kichwani ni mbaya sana, kwani siku zote mtu analalamika mpaka anasahau kuwa kwa kufanya hivyo anamkufuru Mungu aliyemjalia vipaji vingi.
Ubarikiwe sana.
 
Back
Top Bottom