ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 1,964
- 3,895
Jeshi la Polisi Tanzania Lina utaratibu la kuwapa vitendea kazi trafki yaani askari wa usalama barabarani vikiwemo Mashine ya Risiti na Tochi ya kukamatia waozidi mwendo wa 50 jambo ambalo ni tofauti na nchi za wenzetu ambapo trafiki wao hupewa Silaha, gari na nyenzo nyingine muhimu.
Jambo hili limeondoa maana ya askari kufanya shughuli takwa na inaonekana lengo kubwa kwao ni kukusanya fedha ,na huwa wamejipanga barabarani sehemu ambayo imejengwa kwa Kodi Ili raia wapite kwa usalama na bila hofu.
Kitendo cha Trafki kusimama barabarani na Mashine ya Risiti na Tochi kinaleta hofu kubwa sana kwa Madereva , na hivyo kuwaletea Msongo mkubwa wa mawazo na kuwasababishia magonjwa ya Moyo, presha na sukari. Hakuna jambo baya barabarani Kama kusimamishwa na Trafki akiwa na vitendea kazi vyake.
Kila dereva akiingia barabarani jambo la kwanza kuwaza ni Trafki, na wahanga wakubwa ni Madereva wa Mafuso ya mchanga, virikuu, pickup, malori ya mizigo, watu Hawa wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa ya Msongo ikiwemo presha sababu ya kukutana na stress za Trafki kila siku.
Jambo jingine kitendo Cha Trafki kuwa barabarani ni kitendo Cha mambo ya Rushwa, Polisi wanafundisha raia kutenda makosa ya Rushwa, Polisi huko barabarani wamewafundisha watu kuwa Rushwa ndo tiba ya matatizo yako,
Hali iliyopelekea na Madereva nao huko mtaani wanakoenda wanaeneza elimu ya Rushwa waliofundishwa barabarani na hivyo kupelekea nchi nzima kunuka Rushwa.
Itafutwe namna nyingine nzuri ya kudeal na usalama kuliko hao jamaa wenye nguo nyeupe na kofia nyeupe, ukiwaona tu moyo unastuka