Matoleo ya baiskeli Tanganyika

Matoleo ya baiskeli Tanganyika

Ila issue ya kutoa baiskeli naona hawakufikiria vizuri .

Kwanza wamewadharau wananchi
Pili , hakukuwa na ulazima hizo baiskeli kuandikwa SSH

Na wangebarikiwa zaidi ikiwa wangewapa wahitaji bila kuweka vyama .


Mimi ningekuwa mshauri wa ccm.

Zile pikipiki ningeshauri zikae maeneo ambayo ni remotely , (Hayafikiki) then tungempatia Mtendaji , na kumpa utaratibu maalumu kuwa katika shughuli za kijamii ndo pikipiki zitumike pasipo kuangalia vyama .

Mfano, kumuhaisha Mama mjamzito hosptali , wagonjwa , n.k.


Then hao makatibu na Mabalozi ili kurahisisha shughuli zao za kisiasa wangepewa vishikwambi vyenye unlimited bundle .

Kwakuwa 70-90% shughuli za kisiasa zinaweza kufanyika online .

Kwakuwa ukipiga hesabu hizi pikipiki mpaka sasa watu wamezibaki kisa kukosa Mafuta , na wengine wameziuza , pia utumiaji wake wa mafuta ni mkubwa tofauti na pikipiki za kawaida.
 
Rajan
Swala
Phoenix (poeniki kwa sisi la 3B)
Avon
Hero jet
Sinderela
Baiskeli za mama Abudula.
Watendaji na wahudumu wa afya vijijini ndio zilikuwa VIETE zao.
f08b9c76-5ef6-4b17-94d4-c700e5a7b1f0.jpeg
 
Hii Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ni kitu cha ajabu sana.

Mali za Mwaka 70 ni imara sana wakati wa Poor tech kuliko mali za 2025 nyakati za Advanced Tech??
Tunalenga faida zaidi
 
Hizi zamani wasukuma walikuwa wanatoa mud guard, kwenye mashindano ya mbio za baiskeli unakatwa kama upepo na baiskeli yako ya gia.
Walikuwa wanatoka mwanza hadi Dar kwa baiskeli kuwahi mashindano ya baiskeli
 
Ndio asili ya jina la boda boda kwa maana ziliitwa bodaboda zikitumika kubeba abiria stand vijijini hadi vijiji vya mbali zikibeba abiria na mizigo.
Zikiwemo maiti kabla ya ujio wa pikipiki hizi za kisasa.
Pikipiki zamani ilikuwa ni honda 110 za watendaji na mabwana shamba
 
Ndio asili ya jina la boda boda kwa maana ziliitwa bodaboda zikitumika kubeba abiria stand vijijini hadi vijiji vya mbali zikibeba abiria na mizigo.
Zikiwemo maiti kabla ya ujio wa pikipiki hizi za kisasa.
Pikipiki zamani ilikuwa ni honda 110 za watendaji na mabwana shamba
Sio kwamba hili jina lilianzia kampala wakati wa ujio wa pikipiki za mchina? Wakati huo wakisafirisha bidhaa kutoka na mipakani? Boarder to boarder ndio ikazaa bodaboda?
 
Back
Top Bottom