Matokeo ya viongozi dhaifu kuongoza nchi kubwa

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,897
3,201
Wakati Babeli inaanza kuwa Taifa kubwa, haikuwa na raslimali nyingi kama vile madini, bandari, maziwa, eneo zuri la kijiografia, idadi kubwa ya watu, mbuga za wanyama, n k.

Raslimali kubwa iliyokuwa nayo Babeli mpaka kufikia kilele cha mafanikio yake iikuwa ni uongozi imara na ubunifu wa raia wake pamoja na mto Frati (Euphrate).

Lakini cha kusikitisha sana, wakati Babeli ikiwa Taifa kubwa duniani (Super Power), ikapata 'mkosi' wa kuongozwa na kiongozi dhaifu na asiyejielewa kwa jina Belshazar. Kiongozi huyu aliendekeza sana safari zisizo na tija, starehe, umalaya n.k.(ubadhilifu wa mali za Umma kwa ajili ya ufuska).

Hali hii ilipelekea Babeli kuporomoka kwa kasi ya 5G na kuishia mikononi mwa maadui zake, hali iliyopelekea Babeli kufutika kabisa katika ramani ya dunia!

Leo, tumebaki kusoma tu kwenye Historia kwamba kuliwahi kuwepo na nchi ya Babeli/Babilonia na kwamba haijawahi kutokea "Superpower" duniani mithili ya Babeli.

Hicho kilichotokea Babeli kinaweza kutokea kwa Taifa lolote duniani. Nchi inapoongozwa na viongozi imara na wabunifu, huinuka na kuendelea kwa kasi bila kujalisha masuala mengine. Lakini pale nchi kubwa na mashuhuri inapoongozwa na Viongozi/Kiongozi "dhaifu" basi huanza kushuka na kupoteza kabisa ukuu wake wa awali kama ilivyokuwa kwa Babeli au Babilonia ya zamani.

Kwa maelezo zaidi, unaweza kujisomea kwa muda wako kitabu cha "The Richest Man In Babylon ".
 
THE RICHEST MAN IN BABYLON
 

Attachments

  • The_Richest_Man_In_Babylon.pdf
    804 KB · Views: 2
Back
Top Bottom