Matokeo ya Uchaguzi wa Madiwani October 28, 2012

Matokeo ya Uchaguzi wa Madiwani October 28, 2012

Hahahaha wamejazana kushangilia ushindi wa daraja mbili wamesahau kulikuwa na kata 29. Hata huko Magomeni Bagamoyo wamepigwa kipigo cha mbwa mwizi.

Umechukia??
Chadema haikupaswa kushinda kata hata moja kama ccm ni chama makini.
Mtaendelea kujipa moyo na kutandikana makofi wenyewe kwa wenyewe lakini sisi chadema tunawaharibu vibaya.
Kwa sasa tuko zizini tunachagua ng'ombe mnono wa kumchinja.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mkuu tunashukuru sana kwani tuko huku mamtoni na Jamvi la JF ndilo pekee la kutupa habari muhimu kama hizi. Great meeeeeeeeeeeeeen. Bado 2015, watalia na kusaga meno. Nitakuwa nimerudi kupigisha watu jaramba mpaka kieleweke
 
Hongera ccm. waje hapa akina crashwise, mungi, molemo wamwage pumba zao..

Huko c kwa magamba!!embu elimikeni bana!badilikine na fungukeni akili!anayeshabikia uchindi wa ccm ni dhaifu km ccm na mwenyekiti wake!
 
Huo ndio upuuzi wenu hivi sasa ni mwaka 2012 bado mnaongelea ukombozi kazi waliyoimaliza Kina Nyerere, Karume na Samora Machel miaka ya 70. Mnataka kuturudisha nyuma badala ya kuongelea maendeleo mmekalia kupambana na waliyoyamaliza Babu zenyuuu.(kwa swaga)

ni ukombozi wa pili wa mtanzania!ni ukombozi dhidi ya mkoloni mweusi!
 
Linaloniuma zaidi ni kuwa watu niliodhani wanazo timamu kabisa, bado wanaipigia kura CCM? Kazi bado tunayo!
 
m4c inahitaji support ya hali ya juu! Tusilale hadi tuhakikishe 2015 kinaeleweka
 
Natoa pongezi kwa Uongozi wa Juu wa CHADEMA, wajumbe na wananchi wapenda mabadiliko kwa kazi nzuri waliyoifanya. Natahadharisha KAZI BADO.... M4C~ Izungukuke nchi Nzima, asubuhi, mchana na jioni
MPAKA~KIELEWEKE
 
Inaonekana Ccm bado ni imara sana

How? Ume-conclude kwa vigezo gani??

Kama ni matokeo yaliyo hapo kwenye Thread, Chadema wana viti vitano, TLP kimoja, na CCM Vinne.

Wewe umetumia kigezo gani kusema CCM bado imara?
 
Kiburi cha ccm kinaelekea ukingoni.Ni swala la muda tu kabla ya wana ccm kuanza kuhamia chadema na kuacha kulalama wakiwa ndani ya ccm kama hawana pa kukimbilia.
 
hakuna jipya kivipi?chadema imeongeza kata na haijapoteza kata.hayo ni makubwa sana kuelekea 2015

wajua elimu kwa wapiga kura bado ni tatizo na hili ni jukumu la oposition, rushwa lazima ikikomeshwe, wananch lzm wajue kura wanayo piga inamaana gan kwa maisha yao na vizaz vyao, wananchi wakiacha ushabiki na kuelewa thaman ya kura wanayopiga natmai apo tutasogea, ni miaka 50 sasa imepita mpaka sasa tnaamini umaskin ni mipango ya mungu. na tnaamin labda akiamua mungu hali zetu ztakuwa bora otherwise tutaendelea tu na ufukara, na ujinga huu ndo ccm amekuwa anacapitalise on it kwa kuwapa neema kt kampeni km kuwapa pilau, chunv, elf5 elf2 na ata elf10 apo wananch wanaona baraka kubwa imewajia kwavyovyote lzm watoe fadhila ya 2vote for ccm, mijin tshaelewa ccm ni janga lkn vijijin ndo mwaona hawajajitambua japo bado wanakula mlo m1 dhiki kibao, lkn kias chadema kafanya kweli, bright future 4CDM iko waz tuendelee kshikamana 2tafanya vyema zaid, elimu ya uraia iendelee ni muhimu sana.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeendelea kukiburuza Chama cha Mapinduzi (CCM) katika siasa, ambapo kwenye matokeo ya udiwani katika uchaguzi uliofanyika jana, chama hicho kimefanikiwa kutetea kata zake na kunyakua nyingine za CCM.
Hata hivyo uchaguzi huo ambao ulifanyika kwenye kata 29 katika halmashauri mbalimbali nchini, umemalizika huku vurugu kubwa zikitawala na kusababisha wafuasi wa vyama hivyo kuumizana.
Hadi tunakwenda mitamboni matokeo ya kata 14 yalionyesha kuwa CCM ilikuwa imefanikiwa kurejesha kata zake saba, huku CHADEMA ikinyakua kata sita, ambapo mbili zilikuwa za kwao na nne imewanyang'anya CCM na CUF ikiwa na kata moja.
matokeo ya udiwani katika baadhi ya kata yalikuwa yakiendelea kutolewa huku CHADEMA ikiendelea kuiliza CCM kwa kuzitwaa baadhi ya zilizokuwa kata zake.

Jijini Arusha katika Kata ya Daraja Mbili, CCM ilipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyozoa kura 2192 dhidi ya 1315 za chama tawala.
CHADEMA wameweza kuzirejesha kata zao mbili za Nangerea jimboni Rombo, ambapo mgombea wao Frank Sarakana alijizolea kura 2370 dhidi ya 1134 za Dysmas Silayo wa CCM pamoja na ile ya Mtibwa, mkoani Morogoro.
Wilayani Sikonge katika kata ya Ipole, CCM walipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyopata kura 577 dhidi ya 372 za washindani wao, na vilevile kuitwaa kata nyingine ya Lengali wilayani Ludewa iliyokuwa ya CCM.
CHADEMA pia ilikuwa ikiongoza katika kata ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, hadi tunakwenda mitamboni usiku.
Nayo CCM ilifurukuta kwa kuzirejesha kata zake za Msalato ya mkoani Dodoma, Bang'ata ya Arumeru Magharibi kwa kuwa 1177 dhidi ya 881 za CHADEMA, Mletele ya Songea CCM ilishinda kwa kura 950 na CHADEMA ilipata 295.
Pia CCM iliweza kutetea kata zake za Mwawaza mjini Shinyanga, Lwenzela mkoani Geita, Bungala wialayni Kahama na Bagamoyo mkoani Pwani kwa kuibwaga CHADEMA wakati Chama cha Wananchi (CUF) kilishinda kata ya Newala.

Asante mkuu, taarifa yako imeshiba vya kutosha.
 
Hongera CCM - Halisi kwa ushindi mzito na wa kishindo katika uchaguzi wa madiwani hayo ni matokeo kidogo ya ujenzi mpyaa wa chama katika ngazi ya matawi na mashina. Mabadiliko mapya ya CCM Taifa na haya yatatikisa Mafisadi wote na washika pembe wa cdm
 
Back
Top Bottom