Matokeo ya Uchaguzi wa Madiwani October 28, 2012

Matokeo ya Uchaguzi wa Madiwani October 28, 2012

Ningeshangaa, ujiite Fisadi Mtoto halafu usiwe Mwanachama wa Magamba? Manake wenye majina kama yako wamejazana Mabwepande ndio maana huko kwa Wangoni mmenunua shahada za kupigia kura mkashinda. CCM ndio Baba yako? Na Mama yako ni nani, CUF ama? Na hii nchi mnayoijenga kwa zaidi ya miaka 50, ni ujenzi gani huo usioisha? Ama kweli wajinga ndio waliwao!
 
Tatizo wanachadema mlitegemea makubwa kwenye chaguzi hizi ndogo za kata na sasa hakuna jipya mlilolipata mnajifariji tu! 2015 mtaendelea kujifariji

hakuna jipya kivipi?chadema imeongeza kata na haijapoteza kata.hayo ni makubwa sana kuelekea 2015
 
Hahahaha wamejazana kushangilia ushindi wa daraja mbili wamesahau kulikuwa na kata 29. Hata huko Magomeni Bagamoyo wamepigwa kipigo cha mbwa mwizi.
Kama mpaka leo kunawatu wanachagua Ccm basi ukombozi utachelewa saaaaaaana
 
Nadhani utaratibu huu ni mzuri kuwakumbusha wanaoshangalia Kuwa hii ni Katika Kata 21 zilizo tangazwa....do the mathafaking mathematics

lazima tushangilie kwani siku hadi siku ccm inazidi kupoteza huku chadema ikinyakua maeneo yasiyotarajiwa.
ngoja tu analyse matokeo ya mwisho kwani tutagundua kuwa kuna maeneo chadema ilikuwa na idadi ndogo ya wapiga kura lakini sasa wameongezeka ingawa hawakuweza kuleta ushindi.kumbuka daftari la wapiga kura halijaboreshwa ku allow vijana wengi zaidi kupiga kura.2015 ni mwisho wa ccm kwa vyovyote vile.
 
Sio mchezo, ccm wamepigwa gape kubwa mno.
CHADEMA OBRIGADO!!! wana mvomero vema sana. hongera makamanda mstari wa mbele.

Kutoka moyoni mwangu naongeza kuwa hakika nimewapenda zaidi wanamvomero kwa werevu wao. Ahsanteni
 
Matokeo ya uchaguzi kata ya Bangata-Arumeru.
TLP=03.,CDM=881.,CCM=1177
Source: Live coverage from local radio Sunrise fm.
 
hakuna jipya kivipi?chadema imeongeza kata na haijapoteza kata.hayo ni makubwa sana kuelekea 2015
Yeah Chadema imepata mafanikio makubwa maana tumechukua kata za ccm lakini pia ikumbukwe wafuasi wa chadema hawakujiandikisha sana 2010 sasa 2015 itakuwa mafuriko
 
Tatizo wanachadema mlitegemea makubwa kwenye chaguzi hizi ndogo za kata na sasa hakuna jipya mlilolipata mnajifariji tu! 2015 mtaendelea kujifariji

Endeleeni kutuibia tu sisi Watanzania fanyeni mtakavyo sababu ni wakati wenu,ila mkumbuke hakuna mamlaka zinazodumu milele wakati wetu wananchi ukifika mtatafuta pa kutokea
 
sasa bro Deo na wewe si uvue gamba kivitendo na kuvaa gwanda?.Unatuangusha vijana wapenda mabadiliko.
 
baada ya matokeo kwenye kata zote ifanyike tathmini kuangalia kabla ya kuitishwa uchaguzi mdogo kwenye hizo kata zilikuwa zinashikiliwa na diwani kutoka chama kipi na baada ya uchaguzi huu mdogo chama gani kimeshinda.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeendelea kukiburuza Chama cha Mapinduzi (CCM) katika siasa, ambapo kwenye matokeo ya udiwani katika uchaguzi uliofanyika jana, chama hicho kimefanikiwa kutetea kata zake na kunyakua nyingine za CCM.
Hata hivyo uchaguzi huo ambao ulifanyika kwenye kata 29 katika halmashauri mbalimbali nchini, umemalizika huku vurugu kubwa zikitawala na kusababisha wafuasi wa vyama hivyo kuumizana.
Hadi tunakwenda mitamboni matokeo ya kata 14 yalionyesha kuwa CCM ilikuwa imefanikiwa kurejesha kata zake saba, huku CHADEMA ikinyakua kata sita, ambapo mbili zilikuwa za kwao na nne imewanyang’anya CCM na CUF ikiwa na kata moja.
matokeo ya udiwani katika baadhi ya kata yalikuwa yakiendelea kutolewa huku CHADEMA ikiendelea kuiliza CCM kwa kuzitwaa baadhi ya zilizokuwa kata zake.

Jijini Arusha katika Kata ya Daraja Mbili, CCM ilipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyozoa kura 2192 dhidi ya 1315 za chama tawala.
CHADEMA wameweza kuzirejesha kata zao mbili za Nangerea jimboni Rombo, ambapo mgombea wao Frank Sarakana alijizolea kura 2370 dhidi ya 1134 za Dysmas Silayo wa CCM pamoja na ile ya Mtibwa, mkoani Morogoro.
Wilayani Sikonge katika kata ya Ipole, CCM walipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyopata kura 577 dhidi ya 372 za washindani wao, na vilevile kuitwaa kata nyingine ya Lengali wilayani Ludewa iliyokuwa ya CCM.
CHADEMA pia ilikuwa ikiongoza katika kata ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, hadi tunakwenda mitamboni usiku.
Nayo CCM ilifurukuta kwa kuzirejesha kata zake za Msalato ya mkoani Dodoma, Bang’ata ya Arumeru Magharibi kwa kuwa 1177 dhidi ya 881 za CHADEMA, Mletele ya Songea CCM ilishinda kwa kura 950 na CHADEMA ilipata 295.
Pia CCM iliweza kutetea kata zake za Mwawaza mjini Shinyanga, Lwenzela mkoani Geita, Bungala wialayni Kahama na Bagamoyo mkoani Pwani kwa kuibwaga CHADEMA wakati Chama cha Wananchi (CUF) kilishinda kata ya Newala.
 
Matokeo yaliopatikana toka Songea mjini ni kuwa Chadema imepigwa kipigo cha mbwa mwizi kwa kutandikwa kama ifuatavyo:
Ccm kura 955
Chadema kura 297
Cuf kura 27
Na wapeni pole sana wana jf kwa matokeo haya naomba nilale usingizi mtamuuuuuuuuuuuuu Ccm ndio baba ccm yajenga nchi

Ni nani aliyekwambia kuwa CDM itachukua majimbo yote? Rejea kauli ya Zitto hapo jana halafu ndio urudi kwenye mada yako.
 
Kama mpaka leo kunawatu wanachagua Ccm basi ukombozi utachelewa saaaaaaana

Huo ndio upuuzi wenu hivi sasa ni mwaka 2012 bado mnaongelea ukombozi kazi waliyoimaliza Kina Nyerere, Karume na Samora Machel miaka ya 70. Mnataka kuturudisha nyuma badala ya kuongelea maendeleo mmekalia kupambana na waliyoyamaliza Babu zenyuuu.(kwa swaga)
 
Hapa daraja mbili tunachinja ng'ombe usiku huu,
Chadema hatutaki utani.
Karibuni sana wanachadema.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom