Matokeo ya Uchaguzi Mbeya

Tusitegemee mbunge wa Chama chochote kufa na kufanywa uchaguzi akapatikana mbunge wa Chama kingine ,kama alivyoondolewa Lowasa na wengine waliporudi kijijini kwao wakapokelewa ndio hivyo hivyo kwenye Chaguzi,kaondoka wa CCM piga ua galagaza lakini CCM iibuke mshindi na ndio hivyo hivyo Tarime na ndio hapo tulipo.
 
Matokeo ya Uchaguzi Arusha na Mbeya vijijini ni kithibitisho tosha cha yale niliyokuwa nikisema..Upinzani bila nguvu ya pamoja watashindwa siku zote!..
Mtasema weee na kutumia kila sababu lakini kwa mwenye kusoma alama atagundua kwamba vyama vya Upinzani vimejikanyaga vyenyewe..CCM wamepita kama kumsukuma mlevi vile..
 
Matokeo ya Uchaguzi Arusha na Mbeya vijijini ni kithibitisho tosha cha yale niliyokuwa nikisema..Upinzani bila nguvu ya pamoja watashindwa siku zote!..
Mtasema weee na kutumia kila sababu lakini kwa mwenye kusoma alama atagundua kwamba vyama vya Upinzani vimejikanyaga vyenyewe..CCM wamepita kama kumsukuma mlevi vile..

Mkuu wangu Mkandara, mimi siamini hivyo. Endapo kutakuwa na chama cha upinzani imara, kinachoaminiwa na wananchi basi wanaweza kushinda tu. Suala la kuungana linaweza kufanyika baada ya uchaguzi ili kuunda Serikali. Sitegemei na wala sipendi kuona muungano wa vyama vya upinzani vilivyopo Tanzania kwani vitahatarisha usalama wa nchi kama vikishinda. Believe me, kutakuwa na ugomvi mkubwa kuhusu vyeo, ruzuku, maamuzi, shutuma, vijembe nk.

Tanzania tunahitaji chama mbadala siyo muunganiko wa vyama. Kwa masikitiko makubwa bado hakuna dalili za chama mbadala. Maybe C...
 
Ni kweli tunahitaji chama kimoja chenye nguvu; vyama vilivyopo vina weakness zake nyingi tu. Pia tusisahau wengi wanasiasa wa hivi sasa ni wanafiki na ndumila kuwili. Mifano tunayo mingi sana. Ushauri wangu vijana siku zote ndio vuguvugu au chachu ya mafanikio na maendeleo. Tuangalie historia yetu na za wenzetu, tunawezza kuanza hivi sasa vijana tukaanzisha chama madhubuti na target yetu iwe ni 2015 maaana hii 2010 itakuwa ni ku-warm up msuli wetu then tunajifanyia tathmini tukiingia 2015 ni historia mpya. "YES WE CAN"!!!! nI Mtazamo wangu wadau.
 
CUF ni chama cha wabishi wasiokuwa na maana yoyote... ndio yale yale kwamba wapinzani wanashindwa kwa kusema uongo.

Kwa percent CCM iliyopata haiwezekani kwamba ati CCM hawakushinda waliotakiwa kushinda ni CUF ati ni kwa kuwa tu wameibiwa kura.
 
Nziku,
Mkuu hizo ni imani ambazo hazina ukweli uliosimama kisayansi. Ni ndoto ambayo haiwezi kusimama ktk Ulimwengu huu kwani hakuna nchi hata moja ktk dunia ya tatu kumekuwepo na chama mbadala pinzani ya chama Tawala bila kuunganisha nguvu zao kwanza..

Hii inatokana na ukweli kwamba vyama husajiliwa kutokana na uwezo wa watu na sio mrengo wa chama na tunafanya hivyo kuiga demokrasia ya nchi za magharibi ambao kwanza hawana Ukabila wala Udini.. Leo hii Tanzania kuna vyama zaidi ya 10 vyote vikisimamia vyeo, ruzuku, maamuzi, shutuma, vijembe na kadhalika in a positive theory kwamba Usalama wa Taifa unasimama ingawa haki ya wananchi inapuuzwa, kwa hiyo tunasimamisha Usalama wa gharama ya haki zetu.

Kuwepo kwa chama Mbadala nchini ni ndoto mkuu wangu na hakika kama itakuja tokea basi huo Usalama wa Taifa ndio utakuwa mashakani zaidi kwani tumeoyaona Zimbabwe, Kenya, Liberia, Sierra Lione na kadhalika ambako kote wameweza kusimamisha chama kimoja dhidi ya chama tawala..Kuna risk kubwa sana kama tutajaribu kutumia Usalama wa taifa kuwa sababu kubwa mbele ya haki iliyopotea..

Kama nilivyokwisha sema mkuu wangu WATU na MAZINGIRA ni chanzo kizuri sana cha kutazama tuendako..Nimesoma kwa makini sana matokeo ya Uchaguzi Arusha na Mbeya na wanabodi wameeleza kwa kusimamia kila pande lakini hakika utaona kwamba CUF wameanguka kwa sababu ya Chadema, na Chadema wameanguka kwa sababu ya CUF na TLP sio CCM..rudia kusoma maelezo yote utaona wazi kabisa niliyoandika.
Kisha ni muhimnu ukubali kwamba nchi maskini vymama mbadala kupatikana kwa kuzingatia tofauti zetu hasa ktk Makabila na dini jambo ambalo hadi kesho CCM inawafunga magoli vyama pinzani. Laukama swala la Upinzani lingekuwa kuunda timu ya ushindani kama mpira wa miguu ambapo timu mbili hushindana na magoli kuwa matokeo ya mchezo ningekubaliana na mawazo yako lakini Uchaguzi wa viongozi hutokana na matakwa ya wananchi..Haijalishi uwezo wa Chadema, CUF TLP au CCM isipokuwa mapenzi na ushabiki wa mpiga kura..

Trust me, mkuu wangu huwezi kukifanya Chadema, TLP au CUF kuwa chama mbadala kwa sera, Maazimio n.k -U name it ikiwa wananchi tayari wamekwisha jenga ushabiki na unazi ktk maamuzi ya kura zao na hawa ndio watakao piga kura kesho ktk uchaguzi..Yes, ktk vyama vya Upinzani kuna viongozi ambao nia na madhumuni yao ni mbaya, wapo kwa maslahi yao binafsi ama watumiwa wa chama tawala kutokana na mfumo wa vyama hivi toka mwanzo..Hakuna asiyefahamu kwamba vyama hivi vimeundwa ili kukidhi matakwa ya nchi za magharibi na Mwalimu alifanya mawasukuma kina Mrema na Seif ku challenge tu uongozi mbaya na sio siasa za chama wala mrengo wa chama CCM..
Chadema wamekuja na sura mpya, sura ambayo Wadanganyika kamwe hawawezi kuifahamu ikiwa nao watajiingiza ktk vijembe badala ya kutangaza sera zao. lakini pia huwezi kutangaza sera kwa watu ambao wameweka kipaumbele ktk vijembe na mambo ya ZeUtamu mbele ya habari zote..Hawa ndio Wadanganyika unaotaka kuwaongoza mkuu, Wadanganyika ambao ndio waamuzi ktk kura zao na hakika asilimia 80 yao husoma zaidi ZeUtamu, ZeComedy na Kipanya kuliko JF, MwanaHalisi au Daima..
 
CUF ni chama cha wabishi wasiokuwa na maana yoyote... ndio yale yale kwamba wapinzani wanashindwa kwa kusema uongo.

Kwa percent CCM iliyopata haiwezekani kwamba ati CCM hawakushinda waliotakiwa kushinda ni CUF ati ni kwa kuwa tu wameibiwa kura.

- Mkuu Kasheshe, tupo pamoja sana hapa, saafi sana.
 
Nziku,
... huwezi kutangaza sera kwa watu ambao wameweka kipaumbele ktk vijembe na mambo ya ZeUtamu mbele ya habari zote..Hawa ndio Wadanganyika unaotaka kuwaongoza mkuu, Wadanganyika ambao ndio waamuzi ktk kura zao na hakika asilimia 80 yao husoma zaidi ZeUtamu, ZeComedy na Kipanya kuliko JF, MwanaHalisi au Daima..

Nikifikiria hili huwa nachoka na kuamua kuangalia pembeni... yaani kuna Watanzania wanaoweza kusaidiwa kuto kuwa wadanganyika. Ninaamini kabisa kwamba wananchi wenye elimu ya angalau form iv ni potential resource to bring change. Wananchi hawa wanaweza kusikia hoja na kuzichambua na kufanyauamuzi.

Ninachokipinga mimi ni CUF, Chadema,TLP,UDP,NCCR-Mageuzi, DP nk kuungana. Hii ni kujidanganya! pia ni kuweka rehani nchi yetu. Mkuu wangu, kweli unawajua vizuri hawa jamaa? mimi ninaamini kabisa kuwa ume-base kwenye dhana zaidi kuliko uhalisia. Kwangu mimi dhana ya kuwa na chama mbadala ina-sound kuliko hivi vyama kuungana.

wazo kama la Mkuu Aljuniortz nadhani linamaana sana kwa upande mmoja. Upande mwingine ni kukua, kujengeka na kustawi kwa chama kimoja wapo kati ya hivi vilivyopo.
 
Inaonekana Kasheshe & Field Marshall mnawachukia sana CUF? But inabidi muwavumilie ndio fursa ya kuwa na vyama vingi, kila chama kinakuwa na sera zake. Ndio maana ili chama kisajiliwe ni lazima uorodheshe sera zako pamoja na masharti mengine ndio hupata usajili wa muda then wakudumu. So far wana-weakness zao lakini pia wana mazuri yao, kama ambavyo CHADEMA walivyo na mazuri yao na mabaya yao. Huo ndio ukweli japo ni mchungu na unauma.
 
Mbeya by-election: Low turnout explained



Speaking from Mbeya, Tendwa admitted that it was quite possible that the Chadema aspirant`s disqualification adversely affected the turnout.

However, he added that Chadema`s own mobilisation campaign code-named Operation Sangara had undermined the by-election ``precisely in that its thrust was on sensitising people not to vote after its own aspirant was disqualified``.

``When we got here many Mbeya residents could be heard openly saying some Chadema officials had told them not to vote. The NEC intervened by saying it was completely against this but it is evident that the harm had already been done, and hence the low turnout,`` he explained.

Abere Amon, a resident of Chapakazi at Mbalizi in Mbeya, said Chadema aspirant Sambwee Shitambala`s disqualification left many people ``utterly disappointed``.

Contacted for comment, returning officer Juliana Malange admitted that the turnout was ``astonishingly low`` but noted that she did not know why it was so. ``It is true that very few people came to vote but I cannot explain why. I will have to investigate,`` she said.


SOURCE: Guardian

Meaning CHADEMA is now a power to reckon in Tanzania politics. The fact that CHADEMA has no established network in Mbeya and manage to "sabotage" the election says something......

Tanzanianjema
 
Mgombea wa CUF amayakubali makubali matokeo na kusaini fomu lakini inaonekana anawahohia viongozi wake hivyo kutokuwa tayari msimamo wake kuandikwa kwenye vyombo vya jabari.

Wakati anahojiwa na waandishi wa habari jana, Mgombea huyo- Mponzi alisema yeye haoni sababu ya kuendelea na malumbano hadi mahakamani kupinga matokeo, alikubali kushindwa lakini alipoulizwa iwapo maelezo hayo ni msimamo wake rasmi aliruka na kusema anasubiri viongozi wake watoe msimamo.

Hili ni tatizo kubwa katika vyama vya upinzani.

Ni kawaida kusikia kuwa wanachama/viongozi wa ngazi za chini wanakuwa na msimamo tofauti na uongozi wa kitaifa. Kwa CUF ndio kumezidi. Hata wakati wa ushirikiano wao na CHADEMA haya yamekuwa yakitokea. Hata katika uchaguzi wa Tarime ndicho kilichotokea. Wakati uongozi wa kitaifa ulikuwa na msimamo wa kuwatibulia CHADEMA, uongozi wa wilaya/jimbo ulikuwa katika ushirikiano na CHADEMA. Hata CHADEMA haya yamewahi kutokea.....

Tatizo hili ni moja ya challenges lukuki zinazozuia kuwa na umoja/ushirikiano wa upinzani kama ambavyo watanzania walio wengi wangelipenda kuona..

Hata hivyo naamini haya yatapungua wakati hivi vyama vikikua kiasasi

Tanzanianjema
 
Nziku,
Ninachokipinga mimi ni CUF, Chadema,TLP,UDP,NCCR-Mageuzi, DP nk kuungana. Hii ni kujidanganya! pia ni kuweka rehani nchi yetu. Mkuu wangu, kweli unawajua vizuri hawa jamaa? mimi ninaamini kabisa kuwa ume-base kwenye dhana zaidi kuliko uhalisia. Kwangu mimi dhana ya kuwa na chama mbadala ina-sound kuliko hivi vyama kuungana.
Mkuu wangu soma vizuri maelezo yako mwenyewe utaona kwamba tatizo sio chama isipokuwa ni WATU..Je, ni wakati gani tunaweza kuamini watu ama viongozi wetu ktk chama chochote kile kitakachoweza kuundwa ili kifikie kuwa mbadala!..Ikiwa leo hii wewe na mimi hapa tunashindwa kuwaamini kina Dr. Slaa, au Lipumba na wao kati yao wanashindwa kuaminiana iweje iwe rahisi kusimamisha chama mbadala... kumbuka maneno ya FMES kuwa viongozi wetu ni reflection yetu!..sisi wote tunapendana Kichina tu tusidanganyane hapa...Unless kama tunaweza kuviua kabisa vyama hivi vyote yaani Chadema kife, CUF ife, TLP ife na kisha kipatikane chama kingine ambacho sijui kitakuja na sera au hoja zipi tofauti na vyama hivi vilivyotangulia.
Nitarudia kusema kuwa Chadema sio Mbowe wala Dr. Slaa, CUF sio chama cha Lipumba, Sief au sijui nani, vile vile TLP sio Mrema na kadhalika..
Tatizo letu kubwa ni kuendelea kujenga imani hizo na kuabudu kisiasa kuwa hawa ndio miungu au wajenzi wa vyama hivyo. Na kibaya zaidi ni kwamba hata maamuzi yote nje ya Policies za vyama hivi hutolewa na watu hawa hawa hata kama zinahusu personal issues zao.. vijembe na vituko vyote vimejengwa na kundi la watu wachache sana kupindisha ukweli ambao ni muhimu sana kwa maslahi ya Taifa...I believe kuwa wanachama wengi wa vyama hivi wana imani zaidi ya muungano ktk kupata ushindi kuliko viongozi ambao wana personal issues within..Ebu nipe sababu ya msingi hasa ktk kuvunjika kwa muungano wa awali kati ya CUF na Chadema!..

Hivyo, kwa nini tunazidi kufikiria kuwa TLP haitaki kuungana na Chadema wakati asiyetaka kuungana ni Mrema na kundi lake..Kwa nini tuamini kwamba CUF hawataki kuungana kwa sababu kasema Lipumba, hali kadhalika Mbowe na Mbatia kwa vyama vyao..Je, sisi sote tunawajua vizuri watu hawa!...jibu lake, hatuwajui hata wale wanaotuongoza leo kina Kikwete hatuwajui!..
Kama unakumbuka Kikwete aliwahi kutishia kujiunga na Chadema kama CCM isingemsimamisha, leo hii ni rais wa Jamhuri kwa tiketi ya CCM!..huyu mtu anaamini mrengo gani? au CCM wanamchagua kiongozi kwa malengo gani!..Kabourou alitoka Chadema yuko CCM na ukiuliza sababu utaambiwa ni mtu fulani sio chama na hakika problem ni yeye mwenyewe -MTU sio chama Chadema..Hivyo chama mbadala hakiwezi kupatikana ikiwa sisi tunashindwa kuelewa tatizo la siasa zetu ni kitu gani - WATU.

Let's do what is possible leo ya kesho yatafuata. Kuanzisha chama kipya kabisa from no where ni ndoto ya mwendawazimu kwa sababu mazingira yetu - chama ni WATU na hatuna watu hao isipokuwa kundi dogo ambalo tayari limekwisha jitoa mhanga..Nina hakika tukisha mwondoa CCM na utawala wake unaofuata watu, then huko mbele ndiko tunaweza kujenga vyama mbadala vinavyotetea maslahi ya wananchi..
 
Nimefuatilia mjadala wa umuhimu wa vyama vya upinzani kuungana, Nashindwa kumwelewa Mkandandara anaposema tatizo ni watu. WATU kwa maana ya wananchi/ wapigakura au WATU kwa maana ya viongozi wa vyama vya siasa.

Kwa upande wangu siamini kwamba leo hii wananchi wa kawaida bado ni tatizo katika siasa za Tanzania na mifano ipo mingi kuthibitisha hilo.

Kwa mfano, iwapo tatizo lingekuwa wananchi basi CCM wangeweza kushinda kule Tarime ikizingatiwa nguvu waliyoitumia na upinzani uliokuwepo wa vyama vya upinzania dhidi ya Chadema. Kitendo cha wapigakura wa Mbeya Vijini kususia kwa kiwango kile cha asilimia 65 kutojitokeza kipiga kura ni ushahidi mwingine, japokuwa wapo wanatetea uchache ule wakisema ni kawaida chaguzi ndogo kupata wapigakura wachache.

Wananchi wa Mbeya Vijijini walieleza mapema, mara baada ya kuenguliwa kwa mgombea wa Chadema kwamba hawatapiga kura kwa sababu mgombea waliyemtaka ameenguliwa, na tumeshuhudia wengi wakisusia.

Nakubaliana na mtazamo wa Kasheshe na Field Marshal, CUF ni wakorofi, wanataka ku dominate siasa za Tanzania, wanataka kuiendesha Tanzania kutokea Pemba. Walielewa wazi kwamba Mbeya hawakubaliki lakini wakafanya fujo, wenzao walipendekeza vyama vyote viteue wagombea then wawashindanishe kupata anayekubalika na wananchi kati yao, waligoma na kuanza kuendesha kampeni za kuisakama chadema.

Hapa nadhani tuongelee tatizo la viongozi wa vyama vya upinzani kwamba ni wabinafsi mno, wengi wamehamia huko na matatizo yao toka CCM, huwezi kuwabadili leo hii. Ili kupata mabadiliko ya kweli ni wakati muafaka kwa kizazi kuchukua nafasi badala ya kuwazungumzia kina Lipumba, Seif, Mrema n.k hawa wamechoka, wanachumia tumbo tu.

Hebu fikiria mwaka 1995 pale NCCR Mageuzi ilipoiteka nchi, walikubalika vilivyo lakini badala ya kuwashukuru wananchi kwa kuonyesha mwelekeo mpya, waliwageuka kwa kuanza kufukuzana na kutwangana wenyewe kwa wenyewe, wananchi wakapoteza matumaini, majimbo ya Mbeya Mjini na Iringa yakarudi CCM.
 
Hapa nadhani tuongelee tatizo la viongozi wa vyama vya upinzani kwamba ni wabinafsi mno, wengi wamehamia huko na matatizo yao toka CCM, huwezi kuwabadili leo hii. Ili kupata mabadiliko ya kweli ni wakati muafaka kwa kizazi kuchukua nafasi badala ya kuwazungumzia kina Lipumba, Seif, Mrema n.k hawa wamechoka, wanachumia tumbo tu.

- Hapa tupo pamoja sana mkuu, saafi sana.
 
Wakati mwingine vyama vya upinzani vinajibania vyenyewe. Relatively, Chadema inakubalika maeneo mengi ya bara, CUF visiwani. Lakini wakati mwingine wananchi wanaangalia mgombea, si chama. Hebu angalia matokeo haya ya uchaguzi wa diwani uliofanyika juzi, nimeitoa hii katika HabariLeo:

Katika Kata ya Mkundi, mgombea wa CCM, Nilinga Shaweje, alishinda kwa kura 1,154 na kuwabwaga wapinzani wake wa CUF, Maundo Omari aliyepata kura 1,098 na Rashidi Matumla wa Chadema aliyeambulia kura 127.

Sasa angalia:
CCM : 1,154
CUF : 1,098
CHADEMA : 127

Kama CUF ingeungwa mkono na CHADEMA, wapinzani wangepata kura 1225 dhidi ya 1154 za CCM. Nimesema CUF ingeungwa mkono na si CHADEMA ingeungwa mkono, kwa sababu mgombea wa CUF huko alikubalika zaidi. Na CUF nao nadhani watakuwa wamejifunza huko Mbeya Vijijini kuwa Shitambala alipaswa kuungwa mkono, na si kuwekewa pingamizi. Itakuwa ajabu CUF wakimsimamisha Mponzi tena 2010 huko Mbeya
 
Na CUF nao nadhani watakuwa wamejifunza huko Mbeya Vijijini kuwa Shitambala alipaswa kuungwa mkono, na si kuwekewa pingamizi. Itakuwa ajabu CUF wakimsimamisha Mponzi tena 2010 huko Mbeya
Bandiko lako lote linakosa maana kwa kuendelea kumuunga mkono mtu ambae amejaribu kupindisha taratibu na kanuni za uchaguzi. Iwapo jamii inakusudia kuwa na mabadiliko kwa faida yao, watu dizaini ya Shitambala hawana nafasi na hawafai katika mabadiliko. Na hao Wanambeya vijijini watakuwa ni vipofu na mabwege sana iwapo watamchagua Kihiyo Shitambala hapo 2010.
 
Back
Top Bottom