Matokeo ya Uchaguzi Igunga: Radio One

Status
Not open for further replies.
Zitto,
Sidhani kama ni busara kwa wewe kulitolea ufafanuzi suala hili.
Tumeona tangu kule kwenye twitter....unaonekana umekuwa mstari wa mbele sana kutoa taarifa za "ushindwi" wa chadema. Zaidi ya wewe hatujaona kiongozi mwingine yeyote wa chadema aliyezungumzia hilo. Je umetumwa na chama au ni msukumo wako binafsi?
Nadhani ni vema kuiachia tume ifanye kazi yake badala ya wewe kuzunguka kila kona kueleza eti tumeshindwa.

Nakubaliana na ww kwa kiongozi kama yeye kukimbilia haraka haraka kukubali kushindwa wakati NEC bado wajatangaza mshindi. sio aina ya uongozi mzuri
 
Ndugu zangu, tuwe wakweli tu, tumepoteza Igunga.

Tumepoteza kwa sababu moja kubwa- shahada za wapiga zimenunuliwa sana. Kata zote ambazo chadema imeshunda, turn out ilikuwa kubwa. Kata zote ambazo ccm imeshinda turn out ni ndogo sana sana. Hii tabia ya kununua shahada inayofanywa na ccm inaharibu kabisa maana ya uchaguzi. Kuna haja kufikiria kama itabidi tuwe na compulsory voting.

Toka jana usiku saa tano sisi tulishahitimisha kuwa kwa figures za matokeo toka vituoni hatuwezi kutangazwa washindi.
Ni muhimu kwenda mahakamani ili mahakama iweze kuamua masuala fulani fulani kwa mfano Mawaziri kushiriki katika kampeni na kutoa ahadi za kiserikali. Pili, tume kukataza watu ambao majina yao yamo kwenye daftari lakini hawana shahada, kupiga kura.

Suala la Kafumu kukataa kusaini, nadhani tuache masuala haya ambayo ndani ya dakika chache yatagundulika ni uwongo. Toka tunahesabu mpaka tunamaliza hatukuona 'margin' kubwa.

Kata ya Igunga mjini ndio imechangia sana matokeo mabaya.

Bitter but truth
Kwanza nikupongeze, pamoja na makamanda wote, kwa kazi kubwa na ya mafanikio makubwa huko Igunga. Sasa wa-Tanzania hawana wasiwasi tena kwamba hili dude muda wake wa kuondoka u karibu sana.

Ningeomba kwa upande mwingine hili la kwenda mahakamani lifanyike kwa haraka sana, ikiwezekana Kafumu awe mbunge wa kwanza katika historia ya taifa hili kukalia kiti cha ubunge kwa kipindi kifupi sana. Kampeni chafu za Magufuli na wenzake ni sababu tosha kabisa kumng'oa kitini Kafumu. Ilitokea Warioba akiwa waziri mkuu, na jopo la mawakili, akatenguliwa ubunge wake na ofisa tawala wa wilaya ambaye hakuwa hata na wakili mmoja kwa sababu kama hizo hizo. Ilitokea pia Kigoma mjini miaka ya 90 Kabourou alipombwaga mahakamani Premji.

Uchaguzi ukitenguliwa na kurudiwa, japo ni gharama sana kwa CDM, lakini itakuwa maumivu zaidi kwa CCM.
 
Kiukweli Chama cha Chadema kinapaswa kupongezwa sana sababu upinzani kilioupata ni mkubwa sana.Ccm wamesaidiwa na vitu vingi mno,BAKWATA na matamko yao,wanalo jeshi la polisi,walisaidiwa na maraisi wastaafu viongozi Wa kiserikali kina magufuli kushiriki kutoa ahadi ktk kuisaidia ccm
 
Hebu tupeni matokeo na updates zote milioko huko Igunga, ili nasi tulio mbali tuungane nanyi huko vilivyo.
 
Australia kuvote ni cmpulsory na usipovote fine $150.00, usipolipa mahakamani, just that simple!

Mkuu badala ya ku-waste time na kuanza kutafuta sheria ambazo ni hard to implement bora waanze kampeni na kuhamasisha watu kama suala ni kununua shahada pia hata mtu anaweza akauza shahada na kusema shahada imepotea (au itakuwa faini kwa kupoteza shahada) au anaweza akasema yupo safarini (back to square one...) alafu ni Belgium na Australia pekee ambao wanao huu mfumo na wenyewe hata implementation yake ni ngumu sababu mtu akisema alikuwa mgonjwa hoi utabisha...!!?

Hawa jamaa wajipange wote na wapinzani pamoja na kuwa nguvu moja (hayo mengine ni impractical especially Bongo.., ).., na badala ya ku-talk the talk waanze kampeni za vitendo kwenda mpaka vijijini na kuwasaidia wanavijiji wenye njaa na shida hata kuwachimbia visima... (nina uhakika come 2015 wakionesha waliyofanya practically hakuna mtu atakaekubali kupewa tshirt au kofia...) tatizo kuna watu hawaamini kama kweli hawa jamaa wataleta change..., hivyo basi wakionesha waliyofanya watakuwa wamejenga trust ambayo haitaondolewa na propaganda za kofia wala Tshirt...
 
matokeo hewani tayari kafumu hs bn declared a winner bt jiulizeni Zambia nchi hawakuchua cku Igunga full utata wanajua wenyewe walichokua wanafanya behind the curtain
 
Ndugu zangu, tuwe wakweli tu, tumepoteza Igunga.
Tumepoteza kwa sababu moja kubwa- shahada za wapiga zimenunuliwa sana. Kata zote ambazo chadema imeshunda, turn out ilikuwa kubwa.

Kata zote ambazo ccm imeshinda turn out ni ndogo sana sana. Hii tabia ya kununua shahada inayofanywa na ccm inaharibu kabisa maana ya uchaguzi. Kuna haja kufikiria kama itabidi tuwe na compulsory voting.

Toka jana usiku saa tano sisi tulishahitimisha kuwa kwa figures za matokeo toka vituoni hatuwezi kutangazwa washindi.

Ni muhimu kwenda mahakamani ili mahakama iweze kuamua masuala fulani fulani kwa mfano Mawaziri kushiriki katika kampeni na kutoa ahadi za kiserikali. Pili, tume kukataza watu ambao majina yao yamo kwenye daftari lakini hawana shahada, kupiga kura.

Suala la Kafumu kukataa kusaini, nadhani tuache masuala haya ambayo ndani ya dakika chache yatagundulika ni uwongo. Toka tunahesabu mpaka tunamaliza hatukuona 'margin' kubwa.

Kata ya Igunga mjini ndio imechangia sana matokeo mabaya.
Bitter but truth

Ni vigumu kujustify ununuzi wa shahada kama kosa linalothibitika mahakamani. Hii maana yake ni kwamba, ni eneo hili tu ndipo CHADEMA wanashindwa kudhibiti uchakachuaji. Ni eneo ambalo huhitaji kukaa na kulinda kura.

Kwa msingi huo na kwa mbinu hiyo hta kama siipendi CCM basi sitarajii iondoke madarakani.
 
Kama nilivyosema mwanzo, waliokataa kusaini ni magwanda na wamesusia matokeo kama kawaida yao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom