Matokeo ya CO mwaka wa pili yashikiliwa NACTE Tanzania nzima

Yaani nyie mnachobishana ni kama mtu aseme technician ni sawa na engineer!
CO- diploma
MD- Bachelor degree
Umekosea kujua hili!! hapa mkuu hatubishani!! tunaelimishana kwa hoja za msingi!!
kwa wale wanaojua na wale wasio jua wanaelimishwa!!
 
Sema wa Tz sijui tuna shida gani, hivi mtu akiitwa Dr inakuathiri nini. Kama kuitwa Dr mtu ambaye sio MD au PhD ni big issue na kunadharirisha fani basi anzeni na Dr. Khalid Aucho(Daktari wa mpira).

Mbona sie ma-injinia huku viwandani hadi macasual labour wanajiita ma-injinia wakifika mtaani kisa wanavaa helmet, reflector na safety boots lakini inakuwa fresh tu tunacheka tu na kusogeza siku.

Hizi nguvu za kupambania majina bora uwekeze kwenye kusaka tonge, mafanikio yako yaonyeshe utofauti unaoukazia misuli humu.
 
Umeongea ukweli mtupu watanzania Wana husda na roho mbaya tu
 
unaelewa unachoandika lakini ? mi sikuelewi bwana mganga
 
I'm an Engineer, siijui vema kada ya Afya.. ila Ninachojua CO ni Mganga sio Daktari!

Ni miongoni mwa elimu zinazotakiwa kufutwa.
Unachoandika ni sawa na kusema technicians wanatakiwa kufutwa ili engineers wabaki peke yao. Je, hiyo ni sawa?
 
Ni sawa na kusema bruda aitwe padre kwa sababu anachapa kazi vizuri. Au mchanganya zege aitwe engineer kwa sababu anachapa kazi sana. Wengi wanaomfananisha CO na MD, mara nyingi ni CO wenyewe kwa sababu hawajui MD kasoma nini.
Unatoa maelezo ya kueleweka ila naona ma CO wanakaza shingo.
 
Mada ilikuwa kufutwa kwa matokeo lakini hoja zilizojadiliwa ni Nani ni Nani Kati ya afisa tabibu na daktari dah! Nchi ngumu hii hatari...
 
Utaratibu umeshatangazwa na lini mtihani utarudiwa ....
 

Attachments

  • 4_5771526749707831972.pdf
    872.4 KB · Views: 8
Mitihani haijavujishwa na vyuo kwakuwa kwa level 5&6 mitihani na marking scheme hailetwi vyuoni isipokuwa level 4.
Tayari Wizara kwa maelekezo ya Nacte wameshakaa vikao vyao na wametoa taarifa ya kurudiwa kwa mitihani kuanzia January 2022 wakati wa mitihani ya supplementaries ikiendelea.
 
Vilaza bila kuiba paper hawatoboi, hawa ndo wanakuja kutusumbua wanaprescribe ampiclox asubuhi mpaka jioni hamna dawa nyingine wanajua
 
Hii kada ilikuwa inaheshimika sana zamani lakini siku hizi magumashi anajipenyeza kabisa na kumaliza tena MD kabisa wakati zamani ukisoma PCB tu usipokaa vizuri unakuwa mwehu.
Mimi ni mhenga. Tukiwa pale KHS mwenzetu mmoja alitaka kuhifadhi kile kitabu cha Biology kilichoandikwa na Vines and Reeds. Matokeo yake akili zilifyatuka akawa chizi kabisa. Hili ni kweli tupu na Mungu anisaidie.
 
Mimi ni mhenga. Tukiwa pale KHS mwenzetu mmoja alitaka kuhifadhi kile kitabu cha Biology kilichoandikwa na Vines and Reeds. Matokeo yake akili zilifyatuka akawa chizi kabisa. Hili ni kweli tupu na Mungu anisaidie.
Mkate volume 1 and two sii mchezo. Siku hizi vijana wa madesa na biological science, too simplified wanaenda muhimbili na wanatoboa😀😀😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…