Matokeo ya CO mwaka wa pili yashikiliwa NACTE Tanzania nzima

Yaani nyie mnachobishana ni kama mtu aseme technician ni sawa na engineer!
CO- diploma
MD- Bachelor degree
Umekosea kujua hili!! hapa mkuu hatubishani!! tunaelimishana kwa hoja za msingi!!
kwa wale wanaojua na wale wasio jua wanaelimishwa!!
 
Sema wa Tz sijui tuna shida gani, hivi mtu akiitwa Dr inakuathiri nini. Kama kuitwa Dr mtu ambaye sio MD au PhD ni big issue na kunadharirisha fani basi anzeni na Dr. Khalid Aucho(Daktari wa mpira).

Mbona sie ma-injinia huku viwandani hadi macasual labour wanajiita ma-injinia wakifika mtaani kisa wanavaa helmet, reflector na safety boots lakini inakuwa fresh tu tunacheka tu na kusogeza siku.

Hizi nguvu za kupambania majina bora uwekeze kwenye kusaka tonge, mafanikio yako yaonyeshe utofauti unaoukazia misuli humu.
 
Sema wa Tz sijui tuna shida gani, hivi mtu akiitwa Dr inakuathiri nini. Kama kuitwa Dr mtu ambaye sio MD au PhD ni big issue na kunadharirisha fani basi anzeni na Dr. Khalid Aucho(Daktari wa mpira).

Mbona sie ma-injinia huku viwandani hadi macasual labour wanajiita ma-injinia wakifika mtaani kisa wanavaa helmet, reflector na safety boots lakini inakuwa fresh tu tunacheka tu na kusogeza siku.

Hizi nguvu za kupambania majina bora uwekeze kwenye kusaka tonge, mafanikio yako yaonyeshe utofauti unaoukazia misuli humu.
Umeongea ukweli mtupu watanzania Wana husda na roho mbaya tu
 
Wenzako wana toboa kwenye hii fani kwa sababu iko kwenye Damu!! tangu mababu zao, nyie mnatamani tu ajira ndo mna hangaika hivi ....cha kushangaza nini hapo?

Tatizo hujui kuna ushirikiano mkubwa hapo kati ya Medicine ya kisasa na jadi? mpaka kesho? yaani kati ya mtumia ungo na tiba za kisasa? siyo siri Nili bebwa kabisaa kutoka kilingeni kwa bibi nikosomee!!

tena kwa lazima nikasomee hiyo fani na walio nichuka mie ni madaktari babu kubwa mpaka leo! ambao hawa waliku wa field so walikuja kwa bibi for emergency kutafuta dawa ya kuwasaidia wodi ya wazazi!

Ndo maana ya Emergency Caravan za Ikulu kamwe Daktari huchukuliwi hovyo km siyo MD, au Co mwenye asili ya ulozi, km ikitokea ivo wa ivo, utakuwa umeteuliwa tu huko! ukatalii!! Dogo Tiba manake ni za kienyeji zaidi na za kisasa zaidi .

Historia ya Medicine inasema wanajeshi Madaktari wengi wali gundua dawa! kwa kuteka vijiji vya waganga wa kienyeji bila kujua, huko wakakuta rundo la wagonjwa wakitibiwa magonjwa km yale yalioua baadhi yao! so wakawa wapore! hence forth wakatoka na kitu hapo!

Kwa sababu hii wakarudi kwaokufungua mijiviwanda, na wakawa matajiri vizazi na vizazi mpaka kesho! kwa sababu wana hati Milki ya formula ya dawa zao! hizo walizo dai wao ndo wamezivumbua! kuumbe mvumbuzi anakula vumbi Cameroon!

Na ukiangalia sana, kwa jicho la tatu Koo za kitajiri(kibepari) kufuru, huko UK, USA, France nk, Babu wa Babu wa Babu, alikuwa mjeda pia Immernce Wealth pharmaceutical Industrie za Ulaya na Marekani takribani miaka 200 ilopita, km BAYER, asili yao ni wajeda!

ajabu leo hii karne ya 21, kuna MDs tumemsomesha bado ana sinto fahamu wa kibabu cha kale ivi! jamani mtatoka Africa kweli?

Ndo hizi dawa unazotumia leo kwa majidai! jua chanzo chake zilichumwa hpo kwenu kwa ungo! tena kinyume nyume basi! asubuhi! sasa MD hujui History ya kazi yako! so sad wewe sema tu ukweli mizimu ya kichawi umekaa nayo mbali kwenye hii field haufiki mbali mkuu! usione aibu kushindwa!

Reff; ni Davidson Principle en practice of Medicine! soma choote! ndo utajua km mie muongo au mkweli!! Wa south wamesoma vizuri wale! wana heshimu ungo km nini! jadi pale huwaambii chochote mzulu hata masai tu!.. angalia zulu people vizuri usiwachukulie poa wale.....

Bongo amebakia Masai pekee!! anae heshimu Medicine ya jadi! Madaktari km wewe mnawadharau masai ni kosa! sababu mizimu asilia za dawa inayo waongoza kutambua kada ya Medicine bora hamna,

lkn Jamii ya watu wachafu vile wana kitu wale hujui tu!...sababu huna asili ya tiba! umefuata pesa!

Ndo unaumia sasa!! manake una ongea km mtu aliye kosa mafanikio hivi! ajili ya watu flani flani hivi!! na asikwambie mtu Medicine yoote Duniani inatokana na ..mizizi, viungo vya wanyama na Binadamu, sasa km huna connection na mizimu utaishia kulalama tu!

hata mtu ambae hakusoma shule ya Medicines anajua tu neno medicine ni dawa tu! hence forth Dr of Medicine! kwisha ndugu yangu!

MDs jamani jueni kuwa kunakurogwa? manake labda wee hujakutana na kesi ngumu! inayokutoa jasho!! mnazikimbia au mna reffer vi- case vidogo vidogo tu! ndo maana Madaktari wa MNH wanawachukia! uongo jamani? au

basi hizi chuki utakuwa umerogwa wewe! ila hujijui! kuwa mpole wakufunze hao wenzako, kwani field work practical hamkufanya kazi na waganga wa kienyeji? au huja chaguliwa na Mizimu?

km hukufanya basi hujafauru rudi kasome tena upya!! vinginevyo Field hii haikufai!! Wenzako sisi field work tumepiga mpaka kwa Chikanga wa Malawi!! akatuwekea Mikono! km mnamjua huyu jamaa ana Palace Pav. kubwa si kawida kulee nchini Malawi!

Sasa hii MD's Ni kizungu zaidi! na upande ule kuleee!! ni kiafrica zaidi!! Tanganyika Medical Board officers ya leo kamwe usiwajaribu kichawi wako vizuri na wale wa sasa hawarogeki! ukitaka sarakasi za kichawi wajaribu wale uone!! yaani Medicine ya kisasa ile.

Waliomo kunako Board ni wachawi watupu wa kiwango cha uelewa wa hali ya juu mno! usidhanie kuwa sisi tulio soma yote! tuna m-mind yesu wenu mzungu huyo! hatuna muda nae na wala hatufanyii kitu! na kamwe haji! Na Bao tunapiga mwanzo mwisho!

Kuwa mpole kwanza usaidiwe uache hizo!! huenda utakuwa MD mwenye mafanikio vinginevyo utazungusha sana mkuu! mpaka... kuwa dharau COs wenye mafanikio ni bure! tena wale madogo wengi wao ni waelewa sana ujue! ndo maana wana kimbiza!

Ajabu sasa mwenye pesa hanaga mdomo sanaaa! km COs hata humu wako wachache mie nafanya hivi kuwasaidia nyie muachane na mdomo wkt wenzenu hao wanaweza kuwa hata zaidi hata ya nyie ila ni wadogo zenu!! muwaheshimu tunajali sana michango yao!

OPP. ya kwanza alinisimamia CO, Nawaheshimu sana hawa jamaa.........
unaelewa unachoandika lakini ? mi sikuelewi bwana mganga
 
I'm an Engineer, siijui vema kada ya Afya.. ila Ninachojua CO ni Mganga sio Daktari!

Ni miongoni mwa elimu zinazotakiwa kufutwa.
Unachoandika ni sawa na kusema technicians wanatakiwa kufutwa ili engineers wabaki peke yao. Je, hiyo ni sawa?
 
Ni sawa na kusema bruda aitwe padre kwa sababu anachapa kazi vizuri. Au mchanganya zege aitwe engineer kwa sababu anachapa kazi sana. Wengi wanaomfananisha CO na MD, mara nyingi ni CO wenyewe kwa sababu hawajui MD kasoma nini.
Unatoa maelezo ya kueleweka ila naona ma CO wanakaza shingo.
 
Mada ilikuwa kufutwa kwa matokeo lakini hoja zilizojadiliwa ni Nani ni Nani Kati ya afisa tabibu na daktari dah! Nchi ngumu hii hatari...
 
Utaratibu umeshatangazwa na lini mtihani utarudiwa ....
 

Attachments

  • 4_5771526749707831972.pdf
    872.4 KB · Views: 8
Taarifa rasmi ni kwamba matokeo ya mwaka wa pili ya udaktari CO yameshikiliwa NACTE kwa vyuo vyote vya afya baada ya kusemekana paper kuvuja Tanzania nzima pamoja na marking scheme kupelekea GPA kuwa juu mnoo!
Yaaan madogo wangekuwa washachomoka!
Maoni yangu serikali KWANZA ibaini chuo kilichovujisha mitihani itakuwa poa sana na kukifungia kabisaa!
Mitihani haijavujishwa na vyuo kwakuwa kwa level 5&6 mitihani na marking scheme hailetwi vyuoni isipokuwa level 4.
Tayari Wizara kwa maelekezo ya Nacte wameshakaa vikao vyao na wametoa taarifa ya kurudiwa kwa mitihani kuanzia January 2022 wakati wa mitihani ya supplementaries ikiendelea.
 
Vilaza bila kuiba paper hawatoboi, hawa ndo wanakuja kutusumbua wanaprescribe ampiclox asubuhi mpaka jioni hamna dawa nyingine wanajua
 
Hii kada ilikuwa inaheshimika sana zamani lakini siku hizi magumashi anajipenyeza kabisa na kumaliza tena MD kabisa wakati zamani ukisoma PCB tu usipokaa vizuri unakuwa mwehu.
Mimi ni mhenga. Tukiwa pale KHS mwenzetu mmoja alitaka kuhifadhi kile kitabu cha Biology kilichoandikwa na Vines and Reeds. Matokeo yake akili zilifyatuka akawa chizi kabisa. Hili ni kweli tupu na Mungu anisaidie.
 
Mimi ni mhenga. Tukiwa pale KHS mwenzetu mmoja alitaka kuhifadhi kile kitabu cha Biology kilichoandikwa na Vines and Reeds. Matokeo yake akili zilifyatuka akawa chizi kabisa. Hili ni kweli tupu na Mungu anisaidie.
Mkate volume 1 and two sii mchezo. Siku hizi vijana wa madesa na biological science, too simplified wanaenda muhimbili na wanatoboa😀😀😀
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom