BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Chuo cha Kampala University hiki ambacho kipo Gongo la Mboto kina shida kubwa sana, najua wengi mnajua kimewahi kufungiwa siku za nyuma kutokana na magumashi mengi ambayo kimekuwa kikifanya.
Serikali iingilie kati kuangalia hiki chuo, sisi wanafunzi ambao tupo chuoni hapo tunapitia wakati mgumu.
Mfano sasa hivi wanafunzi wa Diploma ya Udaktari wa mwaka wa kwanza na mwaka wa pili matokeo yetu yote yameonesha ni incomplete wakati sisi tumeshafanya kila kitu, chuo kinatulazimisha tuendelee na mwaka wa tatu wakati wanatambua wazi kuwa kufanya hivyo lazima huko mbele ya safari tudunde.
Tumeshaenda hadi Wizara ya Afya ambao ndio wanaosimamia mitihani yetu, wao wanasema tatizo lipo upande wa chuo.
Wanachojua wao kuna vitu havijakamilika na kama tumeambiwa tulipe ada ya mwaka wa tatu wakati matokeo ni incomplete maana yake wanataka wale ada zetu huku wakitambua hakuna uwezekano wa Kwenda mbele.
============
SERIKALI YATOA UFAFANUZI YADAI CHUO KIMEFANYA UDANGANYIFU
Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara Afya, Dk Saitore Laizer amesema:
“Hao wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wapili hawakufundishwa, chuo hakikuwafundisha, huwa tunakuwa na utaratibu wa kuhakiki wakati au baada ya mitihani.
“Baada ya mtihani tukabaini kuwa hao wanafunzi kuna masomo hawajafundishwa hata nusu ya syllabus, na chuo kimefanya udanganyifu mkubwa sana
Tusipokuwa makini tutauana huku duniani, kilifanyika kikao cha pande zote, chuo wakari makosa na kuandika barua jinsi ya kuziba hizo nafasi ili wanafunzi waweze kufundishwa vizuri ili mambo yao yaendelee.”
Kuhusu madai ya wanafunzi kusema kuwa wamekamilisha kila kitu na ndiyo maana wakaruhusiwa kufanya mitihani, Mkurugenzi anasema: “Hawakukamilisha, hapo wenye tatizo ni chuo.”
Kuhusu malalamiko ya wanafunzi kuwa wameshalipa ada na wanatakiwa kulipa tena amesema: “Hicho ni chuo binafsi, hatuingilii masuala ya ada. Hayo malalamiko yanaweza kwenda NACTE.”
Alipoulizwa kwa nini waliruhusu wanafunzi kufanya mitihani wakati wanatambua chuo hakikukamlisha taratibu ambazo zinatakiwa, anasema: “Udanganyifu kwenye mitihani unaweza kugundulika wakati wowote.”
“Tulichoamua ni lazima wanafunzi wafundishwe kile ambacho hawakufundishwa kisha watafanya mitihani tena, lakini hapohapo na sisi tutafanya uhakiki wetu kwa njia tunazozijua.”
Tukiwauliza nini kinachoendelea wanatuzungusha tun a kutupiga danadana, wanataka tulipe ada tu.
Serikali iingilie kati na kutusaidia, kuna mambo mengi hayapo sawa katika hiki chuo.
Kuna baadhi ya wanafunzi wameshakata tamaa ya kuendelea na masomo ukizingatia tunalipa ada kubwa, wengine tunatoka familia dun, hivi inakuwaje unafika mwisho wa masomo na hauwezi ku graduate, unamueleza nini yule ambaye amekuwa akikupa fedha ya ada
Kuna watu wanaishia kulia tu hatuna msaada.