Matokeo Ni saa 8 ya Mchana au Saa 8 ya Usiku?

Status
Not open for further replies.
Walisema saa 8. Ukiuliza kwa nini hawatoi matokeo watajibu walikusudia saa za kidhungu, yaani saa 2 usiku. Ikifika saa 2 usiku watasemawalikusudia kusema saa za kiswahili, yaani saa 8 usiku. Ikifika hapo watasema bora warejee wakati ule ule wa kidhungu yaaani saa 2 asubuhi ya kesho. Hivyo hivyo mpaka wamalize mapishi.

NYONGEZA TU: Toka jikoni nimeambiwa kompyuta NEC zimeshambuliwa na hackers na zimeingia kirusi, kwa hivyo data zote zimepotea na wanaanza kujumlisha upya kwa chaki ubaoni. Tanzania bana, raha tele!
 
Nchi ya Zambia ni kubwa kuliko Igunga lakini iliwachukua siku moja kutangaza matokeo! Hata kama CCM wakishinda lakini naona watakua wameshikwa sehemu nyeti!
 
Yule kinaja wenu anayejichubua alitoa nini asubuhi kwenye facebook? Au alitaga mayai pale!
Mfundisheni uongozi yule kijana.
kwani hujui CDM ni chama chakihuni? Kila mtu anatoa taarifa anavyojisikia


Tumeshashinda! Kubali tu yaishe... CCM ni kila kitu
 
Samahani wakuu, saa 8 igunga ni saa ngapi huku bongo-land?
 
Redio Uhuru wao wanapiga nyimbo za Rap na wao ni mabingwa wa kupiga nyimbo za Taarabu! TBC1 wametupeleka China kweli nahisi Igunga kuna hali mbaya.
 
kuweni wavumilivu tutatangaza saa 8 za ucku wakati ucngizi umewapitia mana mchana mtaleta fujo nyingi
 
Wakuu naomba msaada wenu, nilitegemea kama wanajumlisha kwa njia ya kisasa basi matokeo yangewahi kutoka! hii results management system ikoje? Wataalamu wa IT msaada wenu tafadhali ili tuweze kuelewa inavyofanya kazi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom