Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

...Mpaka sasa hivi zimebaki dakika kama 17 tu ili matokeo yatangazwe.
Hapana, nadhani hizo dakika 17 ulimaanisha matokeo yatatangazwa saa 4 asubuhi right?

Ngumu kwa sasa, yani wameanza upya, kuhesabu kura moja moja, kituo baada ya kituo ili kila mmoja aridhike.

Kazi ipo!
 
Hapana, nadhani hizo dakika 17 ulimaanisha matokeo yatatangazwa saa 4 asubuhi right?

Ngumu kwa sasa, yani wameanza upya, kuhesabu kura moja moja, kituo baada ya kituo ili kila mmoja aridhike.

Kazi ipo!
Mkuu Invisible,

Tunashukuru sana kwa kutupasha yatokeayo huko Biharamulo. Mimi hii thread sikuifuatilia kabisa shauri ya kukosa muda (huku Kyela mawasiliano shida) ila baada ya kuona matokeo yanaingia nikaamua kuchungulia na kukuta eti mzee mzima CCM kagaragazwa.

Mimi nashauri tu kwasasa ambapo inaelekea mambo yako katikati mungetusaidia zaidi kwa kutupatia maoni pia ya pande zingine ambapo kwenye hili ni CCM na NEC. Ni vizuri sana kujua na pande zingine za shilingi zinasemaje (mimi siamini kwamba shilingi ina pande mbili).

Unajua mkitangaza ushindi mapema halafu matokeo yakaja tofauti ndio unakuwa mwanzo wa vurugu.

All in all tunashukuru sana kwa kutuhabarisha ipasavyo.
 
Ambao hawaamini kuwa mwisho wa ccm umefika imekula kwao!!!!!
Wamezoea kuiba kura dawa yao tushaijua ni kulinda kura zetu kwa namna yoyote ile.
nadhani nimesomeka.............
 
CCM nayo yadai imeshinda, wawakilishi wa vyama wako ndani ya ofisi za Halmashauri yanapofanyiwa majumuisho. Ni ukweli usiopingika kutangaza matokeo based on data za chama ni hatari, japo kurelease mapema, kunaziba mianya yoyote ya kuyafanyia madudu matokeo halisi.

Hali ni tete mjini Biharamulo, watu kwa makundi wametanda jirani na ofisi ya msimamizi na wanaonyesha hawako tayari kusikia lolote kinyume cha matumaini waliyokuwa nayo. Matokeo rasmi yakitangazwa CCM imeshinda, nadhani kuanzia hapo kwa msimamizi, patakuwa hapatoshi.FFU nao wamekaa mkao wa kula!.

Inapoelekea Saa 4:30 bila matokeo, Muda wangu BiMulo ndio umeniishia. Natamani kukaa mpaka mwisho, ila kesho ni 77 niking'ang'ana na Bi'Mulo, nitakula polisi. Ziko mtu 7 za JF Bi'Mulo, natumaini update zitaendelea, Mimi naitafuta Busisi.
 
Hapana, nadhani hizo dakika 17 ulimaanisha matokeo yatatangazwa saa 4 asubuhi right?

Ngumu kwa sasa, yani wameanza upya, kuhesabu kura moja moja, kituo baada ya kituo ili kila mmoja aridhike.

Kazi ipo!

Yani kura zinahesabiwa tena kwa mara nyingine tena kwa sababu CCM wameshindwa. Mhh Tanzania kuwa na Demokrasia ya kweli bado ni safari ndefu sana.

Kazi ipo kweli kweli.

TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Thanks mzee Invisible, kwa hii taarifa endelea kutupatia yanayojiri huko. Nina swali moja zile asilimia zinazotajwa kwenye vyombo vya habari vya hapa nyumbani zinatokana na majumuisho ya kula kutoka vituoni? na kama ndivyo wanavuyoendelea kuhesabu kura mojamoja kunaweza kuzibadili? manake hapa ninashangilia ushindi wa CHADEMA, sitaki baadaye kuumizwa roho yangu kama kule Busanda.

kazi njema wakuu.
 
CCM nayo yadai imeshinda, wawakilishi wa vyama wako ndani ya ofisi za Halmashauri yanapofanyiwa majumuisho. Ni ukweli usiopingika kutangaza matokeo based on data za chama ni hatari, japo kurelease mapema, kunaziba mianya yoyote ya kuyafanyia madudu matokeo halisi.

Hali ni tete mjini Biharamulo, watu kwa makundi wametanda jirani na ofisi ya msimamizi na wanaonyesha hawako tayari kusikia lolote kinyume cha matumaini waliyokuwa nayo. Matokeo rasmi yakitangazwa CCM imeshinda, nadhani kuanzia hapo kwa msimamizi, patakuwa hapatoshi.FFU nao wamekaa mkao wa kula!.

Inapoelekea Saa 4:30 bila matokeo, Muda wangu BiMulo ndio umeniishia. Natamani kukaa mpaka mwisho, ila kesho ni 77 niking'ang'ana na Bi'Mulo, nitakula polisi. Ziko mtu 7 za JF Bi'Mulo, natumaini update zitaendelea, Mimi naitafuta Busisi.

Nashukuru mkuu kwa kazi nzuri na Mungu akubariki ufike salama. Pita Tinde mkuu nikupe hi kama unaenda Dar.
 
Hapana, nadhani hizo dakika 17 ulimaanisha matokeo yatatangazwa saa 4 asubuhi right?

Ngumu kwa sasa, yani wameanza upya, kuhesabu kura moja moja, kituo baada ya kituo ili kila mmoja aridhike.

Kazi ipo!

Mhh sasa hayo masanduku yaliyokwama njiani yameshaletwa??? Hizi ni dalili za UFISADI. Leo hizo kura zinaweza kurudiwa mpaka jioni kwa sababu CCM wameshindwa.

Kazi ipo.
 
Asante kwa wale wote wanaoleta habari hizi...

Hapa Mtwara ni saa nne unusu ... kuna habari yoyote mpya?
 
hizo habari ni za muda huu au za usiku.Hongereni CHADEMA,Ila muwe makini wakati wa mwishomwisho huu.Achekae mwanzoni siku zote hununa mwishoni.Hao jamaa waangalieni kwa makini.tarakim zitawekwa kinyume msipochangamka
 
Nimeambatanisha nakala kwenye 1st post ambayo niliipata ikionyesha hali halisi.

Naambatanisha (kwenye 1st post) pia na matokeo ya kituo kwa kituo ambayo walihesabu mara mbili na kukuta yanajirudia, endapo kutakuwa na mabadiliko tutafahamishana!
 
Last edited:
kama ndivyo hivyo demokrasia imekua katika nchi yetu

sisiemu wanatakiwa kukaza buti

hali itakuwa tiofauti uchaguzi mkuu 2010
 
Nimeambatanisha nakala kwenye 1st post ambayo niliipata ikionyesha hali halisi.

Naambatanisha (kwenye 1st post) pia na matokeo ya kituo kwa kituo ambayo walihesabu mara mbili na kukuta yanajirudia, endapo kutakuwa na mabadiliko tutafahamishana!

Mkuu sorry, umenichanganya. Hizi ni kata au vituo ndani ya kata? Ulichohold ni kituo (ile ya 394) au kata.
 
[ame=http://www.youtube.com/watch?v=RZY4dIJlmaQ&feature=related]YouTube - General Idi Amin Dada - An Autoportrait part2/17[/ame]

huyu jamaa ukiclick hapo ana ujumbe kwa wapinzani wa TZ
 
Kinachoendelea sasa ni kuwa ndani ya hiki chumba cha kujumlishia kura ccm wanasema kuwa tuanze kuhesabu matokeo ya kituo kwa kituo na walipotakiwa kutoa fomu za matokeo wanasema kuwa hawana kwani mawakala wao walitekwa na kunyanganywa fomu hizo .

Na wanataka yahesabiwe masanduku ya kata ya Kalenge ambayo yamefikishwa mjini asubuhi hii baada ya kutokufikishwa jana kama inavyotakiwa huku tume ikisema kuwa gari hilo liliharibika njiani, wasiwasi ni kuwa huenda mabox yalibadilishwa, malumbano yanaendelea .
 
Back
Top Bottom