Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,452
Matokeo yasiyo rasmi ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Biharamulo Magharibi yameanza kutoka na kubandikwa ubaoni yakionyesha mgombea wa Chadema, Dr. Antony Mbassa, anaongoza vituo vya mijini. Taarifa zikieleza pia Chadema inaongoza na vijijini.

Turn out ni ndogo chini ya 40%. Matokeo yote yatapatikana by saa hizi baada ya saa 2 usiku zoezi la kuhesabu vituo vyote limekamilika ila data ndio hazijaletwa.
Mpaka sasa matokeo ya vituo 10 mjini, Chadema imeshinda vituo 9 na kutoka sare ma CCM kituo kimoja.
Kwa vijijini, matokeo ya vituo 7, Chadema imeongoza vituo vitano, CCM viwili.
miongoni mwa vitano vya Chedema, viwili ni ngome imara za CCM, zimesambaratishwa.
 
Last edited by a moderator:
Matokeo ya kwanza kubandikwa ni Biharamulo Shule ya Msingi aliposomea mgombea wa CCM. Kituo hiki kina vituo 4. Kati ya hivyo Chadema imeongoza viwili, CCM kimoja, na kimoja CCM na Chadema wamefungana.
Naelekea kituo cha pili hapa hapa mjini Biharamulo.
 
yani chini ya asilimia 40 ndio wanamchagua muakilishi wao? kweli watu wanahitaji kuelimishwa zaidi umuhimu wa kupiga kura.
 
Kituo cha Umoja Shule ya Msingi yenye vituo 4. Chadema imeongoza vituo 3 na CCM kimoja. Tofauti ya kura ni chache sana. CCM inaanza kuongoza baadhi ya vituo vya mijini, hivyo kwa vijijini ndio kabisa. TLP ni hoi bin taaban, kuna vituo imepata kura 0, kuna vituo imeambulia kura moja.
natafuta kituo cha tatu.
 
Ya Busanda yaelekea kujirudia Biharamulo, tena safari hii CCM yaweza kuongoza kwa tofauti ya kura nyingi zaidi.

Kazi kweli kweli.
 
Hivi tunapiga kula ili iweje.Mimi nadhani afadhali tusipige kula,afadhali enzi za mwalimu tulikuwa tunapiga kula kuchagua viongozi.Tangu nyerere atoke hadi leo, sioni kama tunapiga kula kuchagua viongozi zaidi ya kuchagua watu wa kuuza nchi.

Nchi imeuzwa kila kitu kinaondoka,wale tunaochagua nao wanaakikisha wanatunza pesa za kujitosheleza maana hakuna ambaye anauhakika kwamba hii nchi ni yake,kila mtu anatafuta pesa za kutosha na kurundika iwezekanavyo.

Tangu nyerere atoke madarakani mpaka sasa hivi, tumeshindwa angalau katika uchaguzi kubahatisha kupata kiongozi mzuri wakutasaidia.Kila baada ya miaka mitano,ni bahati mbaya,je mpaka lini?.Afadhali tukagoma kupiga kula,wajichague wenyewe angalau tusibaki tunajiraumu.
We fikiria mtu anaiba 200bilioni,eti yupo anaendelea kuishi,kwanini tusiige angalau nchi kama china.Mfano katika nchi ya china, wale waliouza maziwa yenye sumu walifanywaje? walishahukumiwa tayari. Kuna tofauti gani na mtu mmoja aliyeletea taifa hasara ya 200bilions.Hatuna haja ya kupiga kura.
 
Kituo changu cha 3 ni Ofisi ya Kata ya Biharamulo, ilikuwa na vituo 5. Vyote Chadema imeshinda kwa small margin. Pia nimepata taarifa CCM-imeshinda kituo kimoja. Sasa nachepuka kidogo vituo vya mjini kuelekea nje ya mji japo sio vijijini.
 
Hivi tunapiga kula ili iweje.Mimi nadhani afadhali tusipige kula,afadhali enzi za mwalimu tulikuwa tunapiga kula kuchagua viongozi.Tangu nyerere atoke hadi leo, sioni kama tunapiga kula kuchagua viongozi zaidi ya kuchagua watu wa kuuza nchi.
Nchi imeuzwa kila kitu kinaondoka,wale tunaochagua nao wanaakikisha wanatunza pesa za kujitosheleza maana hakuna ambaye anauhakika kwamba hii nchi ni yake,kila mtu anatafuta pesa za kutosha na kurundika iwezekanavyo.
Tangu nyerere atoke madarakani mpaka sasa hivi, tumeshindwa angalau katika uchaguzi kubahatisha kupata kiongozi mzuri wakutasaidia.Kila baada ya miaka mitano,ni bahati mbaya,je mpaka lini?.Afadhali tukagoma kupiga kula,wajichague wenyewe angalau tusibaki tunajiraumu.
We fikiria mtu anaiba 200bilioni,eti yupo anaendelea kuishi,kwanini tusiige angalau nchi kama china.Mfano katika nchi ya china, wale waliouza maziwa yenye sumu walifanywaje?walshahukumiwa tayari.Kunatofauti gani na mtu mmoja aliyeletea taifa hasara ya 200bilions.Hatuna haja ya kupiga kura.

Mkuu,

Hiyo enzi ya Mwalimu ndio ilikuwa ovyo kabisa huwezi ita uchaguzi NDIO na HAPANA, mtu na kivuli!
 
Ya Busanda yaelekea kujirudia Biharamulo, tena safari hii CCM yaweza kuongoza kwa tofauti ya kura nyingi zaidi.

Kazi kweli kweli.
Huu ni ukweli uliowazi, CCM itashinda kwa kishindo kikuu kuliko Busanda, kama Chadema inaongoza mijini kwa slim margin, huko vijijini itakuwaje?.
 
Chadema,

Mkitoka Biharamulo endeleeni na "Operesheni Sangara" vijijini Mkoa wote wa Kagera. Halafu mikoa mingine yote Tz bara. Hakuna kulala, mpaka mafisadi na chama chao wang'oke. Dhuluma, ubadhirifu ziiiiiiii 2010.
 
Umesahau kuwaambia "wagomee" kusaini fomu za matokeo mpaka kieleweke!

Teh teh!
 
Chadema,

Mkitoka Biharamulo endeleeni na "Operesheni Sangara" vijijini Mkoa wote wa Kagera. Halafu mikoa mingine yote Tz bara. Hakuna kulala, mpaka mafisadi na chama chao wang'oke. Dhuluma, ubadhirifu ziiiiiiii 2010.

Huko vijiji huwezi kuwabadilisha kwa mikutano ya jukwaani mara moja kwa miaka 2...

CCM wana "base" imara huko vijijini ambayo hata kama haifanyi kazi yoyote ya maana katika kuboresha huduma za jamaii. Kwa wananchi wa kule wanaiona bendera na kuwatambua viongozi wa ccm kwa majina na wako nao kila siku wakiwa mashambani mwao kwenye sherehe au misiba.

Hicho ndio chadema na wapinzani wengine wanatakiwa kukifanya...kama wana nia ya kushinda vijijini.
 
Kituo-cha Shule ya Msingi ya Nyakatuntu, yenye vituo viwili- Chadema imeongoza. Sasa natoka kabisa town naingia kijijini, no network.
 
CCM inaanza kuongoza baadhi ya vituo vya mijini, hivyo kwa vijijini ndio kabisa. natafuta kituo cha tatu.
Mbona matokeo yako yanakuwa kama hayako kati, naona lugha kama ipo biased, wanapoongoza CCM sema wameongoza vingapi na wanapoongoza CHADEMA vile vile tuambie ili tujue nani anakunja jamvi huko. Lugha yako haiko straight. Hata hivyo asante kwa kutupasha yanayojiri
 
Nimepitia vituo vingine vitatu vya vijijini upande wa kabila la Wasubi, Chadema ni fumika bovu!, imeigaragaza CCMM kwa marjin kubwa.
 
Back
Top Bottom