Matatizo ya sekta ya nishati ni tatizo la Serikali, kumtwisha Januari Makamba ni kutufanya watanzania mazuzu!

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,171
9,397
Imekuwa kawaida Kwa Chama Tawala, kujikita ZAIDI kwenye Siasa za Uchaguzi kuliko kuangalia utatuzi wa chaangamotto na kuondoka umaskini! Sekta ya Nishati ni mojawapo ya Eneo ambalo Vita vya Wana CCM hupigwa vizuri sana, Kila unapoekea Uchaguzi!

Leo nimemsikiliza Karibu Mkuu wa CCM ,nimebaini kuwa Agenda ya CCM kwa Sasa ni kielekea Uchaguzi wa ndani na 2025!
Katika miktadha ambao Nchi inakabiliwa ña matatizo lukuki ilitarajiwa Chama Tawala lijadili namna ya kuitoa nchi ktk mtanzuka huu! Lakini Agenda ni mnyukano wa kugombea madaraka!

Ukipitia kwenye mitandao ya kijamii utaona jinsi Waziri Makamba anavyoshambuliwa ...kuwa eti amesababisha matatizo yote haya!

Inawezekana ni kweli katika miezi michache aliyopewa dhamana hajafanya kitu Cha maana ...lakini swali la kujiuliza Je, matatizo ya Nishati ya Nchi hii kweli tunayadogoisha" kuwa ya mtu Binafsi!
Kama tunafika hapo basi Watanzania Hatujiitambui!

Hivi athari za IPTL,Richmond,...tumeyasahau!
Hivi Sera yetu ya Nishati ,tunaijua ...Je inatekelezwaje!
Mradi kama wa Bwawa la Nyerere tulijandaa!
Athari za Mabadiliko ya Tabia nchi tumejiandaa!

Kwa miaka takribani Kumi tumeshuhudia Hali ya Ukame, Je kama Taifa, tumejiandaaje na Mabwawa yettu ya Umeme?
Ile gesi ya Mtwara tuliyoaminishwa ni mkombozi Iko wapi!

Mbona Chama Cha Mapinduzi hawajadili mambo haya mazito, badala yake wanamjadili Luhaga na Makamba?
Leo hii, watu wana Hali ngumu Mtaani, nani anajali!

Huu ukame wa Disemba na Januari uliua maelfu ya mifugo mwaka huu utaua Makumi elfu ...Viongozi hamuoni?!
Bila Shaka Viongozi wa CCM Wanawaza Madaraka na sisi Wananchi tumelala!?

Siku tukiamka .....!
 
Acha abebe, hata yeye mwenyewe kaamua kubeba hayo matatizo ndiyo maana aliamua kuzima ovyo umeme akisema ukarabati huku akijua kuna maeneo haikupaswa kuzimwa leo unasema serikali ihusike kwani waziri ni mtu binafsi from no where?.
 
Kipara ni ovyo. Anamharibia sana mama. Mama anashindwa nini kumuondoa.

Mbona Aweso na Mkenda wanaweza kumaidia hiyo wizara hata kama hamtaki Kalemani?
 
Unafikiri mama anaipenda kuharibikiwa?!
km hapendi Nishati isimharibikie mikononi mbona kamtoa Kalemani na kumuweka huyo kipara, hivi kweli makato ya simu kwa Raia wote yasingeweza kuziba pengo la mafuta? Kenya na Nchi kibao wamerekebisha mafuta kwani ndio inayo stabilize maisha, huko vijijini umeme kuunga ni 329,000/ na bado Kuna mgao bila woga huoni NI kurejesha majenereta?
 
Back
Top Bottom