Matatizo matatu makubwa kwenye Dira ya Taifa 2050

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,248
Reaction score
90,318
1. Malengo yasiyo na uhalisia
Nimemsikiliza Rostam Aziz anasema tume ya kutengeneza dira walikuwa wanalenga Tanzania iwe na ukubwa wa uchumi(GDP) kati ya $bilion 500-700, wao sekta binafsi wakina Rostam wakapendekeza malengo iwe GDP $Trilion 1 ! Haya ni malengo yasiyo na uhalisia, kwa miaka 25 ijayo uchumi wa Tanzania kukua mara 12 zaidi ya sasa unahitaji miujiza au akili kama za Wazungu na Tiger economies. Uchumi wa $Trilioni 1 unazungumzia uchumi kama wa Saudi Arabia na Netherlands.

2. Kutoweka kipaumbele katika kupunguza masikini
Inaonekana walioitengeneza hii dira ni wale watu walioganda na wanaoamini zaidi katika "trickle down economics" , mkakati wa uchumi unaoamini zaidi kwamba ukuaji mkubwa wa uchumi siku zote utajitafsiri katika maisha mazuri kwa raia wengi. Huu ni mkakati ambao kwa sasa unaonekana kufeli vibaya sana katika nchi kadhaa zenye uchumi mkubwa . Ukuaji mkubwa wa uchumi hauna maana sana kama sio jumuishi na wenye kuleta nafuu ya maisha kwa raia wengi. Nchi nyingi duniani zenye uchumi mkubwa hadi za ulimwengu wa kwanza kwa sasa nyingi raia wanapoteza imani juu ya serikali zao kwa sababu uchumi unamilikiwa na watu wachache sana huku mamilioni wakiishi maisha ya kuteseka.

3. Utengenezaji wa Dira kuongozwa na mwalimu wa saikolojia na elimu.
Dira ya Taifa ilitakiwa iongozwe na mwanauchumi nguli, hili halitakiwi kuwa suala la mjadala au kubishaniwa.
 
1. Malengo yasiyo na uhalisia
Nimemsikiliza Rostam Aziz anasema tume ya kutengeneza dira walikuwa wanalenga Tanzania iwe na ukubwa wa uchumi(GDP) kati ya $bilion 500-700, wao wakina Rostam wakapendekeza malenge iwe GDP $Trilion 1 ! Haya ni malengo yasiyo na uhalisia, kwa miaka 25 ijayo uchumi wa Tanzania kukua mara 12 zaidi ya sasa unahitaji miujiza au akili kama za Wazungu na Tiger economies. Uchumi wa $Trilioni 1 unazungumzia uchumi kama wa Saudi Arabia na Netherlands.

Inaonekana walioitenegeza hii dira wanaamini zaidi katika "trickle down economics" mkakati wa uchumi unaoamini zaidi kwamba ukuaji mkubwa wa uchumi siku zote utajitafsiri katika maisha mazuri kwa raia wengi. Huu ni mkakati ambao kwa sasa unaonekana kufeli vibaya sana katika nchi kadhaa zenye uchumi mkubwa . Ukuaji mkubwa wa uchumi hauna maana sana kama sio jumuishi, nchi nyingi duniani zenye uchumi mkubwa hadi za ulimwengu wa kwanza kwa sasa nyingi raia wanapoteza imani juu ya serikali zao kwa sababu uchumi unamilikiwa na watu wachache sana huku mamilioni wakiishi maisha ya kuteseka.

Ukirudia kusoma utagundua ni mawazo ya kikundi cha watu, siyo shirikishi.
 
Jamanani mwenye soft copy ya pdf ya hii dira atuwekee humu tuone kama maoni ya wengine kweli yalizingatiwa au ni ya ccm pekee?
 
1. Malengo yasiyo na uhalisia
Nimemsikiliza Rostam Aziz anasema tume ya kutengeneza dira walikuwa wanalenga Tanzania iwe na ukubwa wa uchumi(GDP) kati ya $bilion 500-700, wao wakina Rostam wakapendekeza malenge iwe GDP $Trilion 1 ! Haya ni malengo yasiyo na uhalisia, kwa miaka 25 ijayo uchumi wa Tanzania kukua mara 12 zaidi ya sasa unahitaji miujiza au akili kama za Wazungu na Tiger economies. Uchumi wa $Trilioni 1 unazungumzia uchumi kama wa Saudi Arabia na Netherlands.

2. Kutoweka kipaumbele katika kupunguza masikini
Inaonekana walioitenegeza hii dira wanaamini zaidi katika "trickle down economics" mkakati wa uchumi unaoamini zaidi kwamba ukuaji mkubwa wa uchumi siku zote utajitafsiri katika maisha mazuri kwa raia wengi. Huu ni mkakati ambao kwa sasa unaonekana kufeli vibaya sana katika nchi kadhaa zenye uchumi mkubwa . Ukuaji mkubwa wa uchumi hauna maana sana kama sio jumuishi, nchi nyingi duniani zenye uchumi mkubwa hadi za ulimwengu wa kwanza kwa sasa nyingi raia wanapoteza imani juu ya serikali zao kwa sababu uchumi unamilikiwa na watu wachache sana huku mamilioni wakiishi maisha ya kuteseka.

3. Utengenezaji wa Dira kuongozwa na mwalimu wa saikolojia na elimu.
Dira ya Taifa ilitakiwa iongozwe na mwanauchumi nguli, hili halitakiwi kuwa suala la mjadala au kubishaniwa.
1.Nadhani wamefanya uchambuzi wa kina ,wamepitia Nchi kadhaa zilizofanikiwa na wakaangalia potential ya Tanzania.

Ni muhimu kukiwekea lengo kubwa Ili kujitathmini.

Changamoto ya hii namba Moja zinazoweza kukwamisha utekelezaji ni
-Kufanya miradi na mipango kisasa bila kuwa na vipaombele
-Itikadi za Viongozi wa kisiasa,.Dira imejikita kwenye Uchumi utakaoongozwa na soko.lakini hii itategemeana na Kiongozi wa siasa za kipindi hicho ,usitegemee watu kama kina Mwendazake kufanikisha Dira.

2.Hoja ya pili Ina msingi lakini hakuna Nchi imeendelea bila kukuza GDP kwanza.

Nadhani kwenye utekelezaji unaweza weka sera za bottom up na kupata economic growth ambayo ita trifle down maana hapa ni kuangalia sekta zipi zitakuwa za kipaombele.

Ulisema sekta ya viwanda iwe Kiongozi hapo ni lazima viwe vile vya kuongoze value chain ya bidhaa za Kilimo,Mifugo na uvuvi ambako ndiko watu wengi wapo.

3.Hili Sina hakika Kwa sababu yeye ni Msemaji tuu wa Wizara ila input zimetoka Kwa Wachumi kina Dr Mpango na wengineo.
 
Uko sahihi kusema kuwa kufikia uchumi wa dola trilioni 1 kutoka takribani dola bilioni 75 (2024) ni ongezeko la zaidi ya mara 12 katika miaka 25. Ili hili litokee, Tanzania itahitaji kiwango cha ukuaji wa uchumi wa takribani 10% hadi 12% kwa mwaka kwa mfululizo, bila kurudi nyuma.Ni ngumu sana kutekelezeka
 
Angeitwa Lipumba hawa kwa hili ni wasanii halafu 2050 karibu wengi hawatakuwepo wangelenga ilani ya miaka 5 juu ya matatizo ya uchumi na ajira kwa vijana lakini huu ni usanii wa ajabu
Hivi dira ni fixed haifanyiwi review?
 
Hivi dira ni fixed haifanyiwi review?
Hili nalo ni mjadala mwingine, nafikiri zama za kupanga maendeleo ya sekta zote kwa miaka 10, 15, 20, 25 n.k ni kama zimepitwa na wakati. Nafikiri mipango miji na suala la nishati ndio vina mashiko ya kuwekewa mipango ya miaka 25 au hata 50, mambo mengine yalitakiwa kupangwa kwa miaka mitano mitano tu.
 
1. Malengo yasiyo na uhalisia
Nimemsikiliza Rostam Aziz anasema tume ya kutengeneza dira walikuwa wanalenga Tanzania iwe na ukubwa wa uchumi(GDP) kati ya $bilion 500-700, wao sekta binafsi wakina Rostam wakapendekeza malengo iwe GDP $Trilion 1 ! Haya ni malengo yasiyo na uhalisia, kwa miaka 25 ijayo uchumi wa Tanzania kukua mara 12 zaidi ya sasa unahitaji miujiza au akili kama za Wazungu na Tiger economies. Uchumi wa $Trilioni 1 unazungumzia uchumi kama wa Saudi Arabia na Netherlands.

2. Kutoweka kipaumbele katika kupunguza masikini
Inaonekana walioitengeneza hii dira ni wale watu walioganda na wanaoamini zaidi katika "trickle down economics" , mkakati wa uchumi unaoamini zaidi kwamba ukuaji mkubwa wa uchumi siku zote utajitafsiri katika maisha mazuri kwa raia wengi. Huu ni mkakati ambao kwa sasa unaonekana kufeli vibaya sana katika nchi kadhaa zenye uchumi mkubwa . Ukuaji mkubwa wa uchumi hauna maana sana kama sio jumuishi na wenye kuleta nafuu ya maisha kwa raia wengi. Nchi nyingi duniani zenye uchumi mkubwa hadi za ulimwengu wa kwanza kwa sasa nyingi raia wanapoteza imani juu ya serikali zao kwa sababu uchumi unamilikiwa na watu wachache sana huku mamilioni wakiishi maisha ya kuteseka.

3. Utengenezaji wa Dira kuongozwa na mwalimu wa saikolojia na elimu.
Dira ya Taifa ilitakiwa iongozwe na mwanauchumi nguli, hili halitakiwi kuwa suala la mjadala au kubishaniwa.
Kuanzia Dira iliopita mwaka 99/2000 mpaka sasa hivi uchumi umekuwa mara 7 yake, so at minimum 500B mpaka 700B ni reasonable figure kabisa, na 1T pia inawezekana. Ulichosahau kwenye Estimation zako ni Population yetu unavyokua kwa kasi kuliko hayo mataifa uliyotaja. Kwa rate ya sasa ya 6-7% tutadondokea humo humo kwenye around 500-600B.

Kinachodrive uchumi sasa ni Kilimo, so si kweli kwamba Masikini hawamo kwenye hio Dira, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni wakulima wapo vizuri sasa hivi kuanzia bajeti ya Kilimo hadi value inayopatikana kwenye kilimo, kama kilimo Kinapita Madini , Utalii na na sekta nyengine ambazo watanzania wengi hawafaidiki ni obvious kitafaidisha watu wengi.

Pia Uchumi ni moja tu ya Dira ya Taifa kuna mambo mengi kwenye hio Dira kama mazingira, Ukuaji wa kiswahili etc hivyo sioni tabu kukiwa na mwalimu.

Watu wanadharau sana na wengi hawaongelei mazingira ila sisi as of now tusipodhibiti hilo Tutakua nchi ya kipuuzi sana.
 
1.Nadhani wamefanya uchambuzi wa kina ,wamepitia Nchi kadhaa zilizofanikiwa na wakaangalia potential ya Tanzania.

Ni muhimu kukiwekea lengo kubwa Ili kujitathmini.

Changamoto ya hii namba Moja zinazoweza kukwamisha utekelezaji ni
-Kufanya miradi na mipango kisasa bila kuwa na vipaombele
-Itikadi za Viongozi wa kisiasa,.Dira imejikita kwenye Uchumi utakaoongozwa na soko.lakini hii itategemeana na Kiongozi wa siasa za kipindi hicho ,usitegemee watu kama kina Mwendazake kufanikisha Dira.

2.Hoja ya pili Ina msingi lakini hakuna Nchi imeendelea bila kukuza GDP kwanza.

Nadhani kwenye utekelezaji unaweza weka sera za bottom up na kupata economic growth ambayo ita trifle down maana hapa ni kuangalia sekta zipi zitakuwa za kipaombele.

Ulisema sekta ya viwanda iwe Kiongozi hapo ni lazima viwe vile vya kuongoze value chain ya bidhaa za Kilimo,Mifugo na uvuvi ambako ndiko watu wengi wapo.

3.Hili Sina hakika Kwa sababu yeye ni Msemaji tuu wa Wizara ila input zimetoka Kwa Wachumi kina Dr Mpango na wengineo.
Nchi gani zilizofanikiwa kufanya hivyo? Ziweke hapa tuzilinganishe na Tanzania.
 
Kuanzia Dira iliopita mwaka 99/2000 mpaka sasa hivi uchumi umekuwa mara 7 yake, so at minimum 500B mpaka 700B ni reasonable figure kabisa, na 1T pia inawezekana. Ulichosahau kwenye Estimation zako ni Population yetu unavyokua kwa kasi kuliko hayo mataifa uliyotaja. Kwa rate ya sasa ya 6-7% tutadondokea humo humo kwenye around 500-600B.

Kinachodrive uchumi sasa ni Kilimo, so si kweli kwamba Masikini hawamo kwenye hio Dira, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni wakulima wapo vizuri sasa hivi kuanzia bajeti ya Kilimo hadi value inayopatikana kwenye kilimo, kama kilimo Kinapita Madini , Utalii na na sekta nyengine ambazo watanzania wengi hawafaidiki ni obvious kitafaidisha watu wengi.

Pia Uchumi ni moja tu ya Dira ya Taifa kuna mambo mengi kwenye hio Dira kama mazingira, Ukuaji wa kiswahili etc hivyo sioni tabu kukiwa na mwalimu.

Watu wanadharau sana na wengi hawaongelei mazingira ila sisi as of now tusipodhibiti hilo Tutakua nchi ya kipuuzi sana.
Kama kwa miaka 25 iliyopita uchumi umekuwa mara 6 maajabu gani unafikiria yatafanyika ukue mara 12 kwa miaka 25 ijayo??
Kilimo kinachangia robo tu(25%) kwenye GDP ya Tanzania.
 
Kwa GDP PPP inawezekana. Sema nchi yetu inapotential sana. Hata kukuza Nominal GDP kwa ukubwa huo kwa watu wenye akili inawezekana.
 
1. Malengo yasiyo na uhalisia
Nimemsikiliza Rostam Aziz anasema tume ya kutengeneza dira walikuwa wanalenga Tanzania iwe na ukubwa wa uchumi(GDP) kati ya $bilion 500-700, wao sekta binafsi wakina Rostam wakapendekeza malengo iwe GDP $Trilion 1 ! Haya ni malengo yasiyo na uhalisia, kwa miaka 25 ijayo uchumi wa Tanzania kukua mara 12 zaidi ya sasa unahitaji miujiza au akili kama za Wazungu na Tiger economies. Uchumi wa $Trilioni 1 unazungumzia uchumi kama wa Saudi Arabia na Netherlands.

2. Kutoweka kipaumbele katika kupunguza masikini
Inaonekana walioitengeneza hii dira ni wale watu walioganda na wanaoamini zaidi katika "trickle down economics" , mkakati wa uchumi unaoamini zaidi kwamba ukuaji mkubwa wa uchumi siku zote utajitafsiri katika maisha mazuri kwa raia wengi. Huu ni mkakati ambao kwa sasa unaonekana kufeli vibaya sana katika nchi kadhaa zenye uchumi mkubwa . Ukuaji mkubwa wa uchumi hauna maana sana kama sio jumuishi na wenye kuleta nafuu ya maisha kwa raia wengi. Nchi nyingi duniani zenye uchumi mkubwa hadi za ulimwengu wa kwanza kwa sasa nyingi raia wanapoteza imani juu ya serikali zao kwa sababu uchumi unamilikiwa na watu wachache sana huku mamilioni wakiishi maisha ya kuteseka.

3. Utengenezaji wa Dira kuongozwa na mwalimu wa saikolojia na elimu.
Dira ya Taifa ilitakiwa iongozwe na mwanauchumi nguli, hili halitakiwi kuwa suala la mjadala au kubishaniwa.
Ingawa niko na itikadi tofauti ila nakupongeza sana kwa kutoa maoni yako kuhusu dira ya Taifa tofauti na wengi wanaomjadili Mbowe aliyehudhuria uzinduzi.
 
Back
Top Bottom