Matapeli wakubwa 5 kuwahi kutokea Tanzania

Matapeli wakubwa 5 kuwahi kutokea Tanzania

Kigogo wacha Bwn, Babu kawapanga foleni, nasikia hata mkulu wa kaya alikunywa kikombe??
 
Last edited by a moderator:
Salaam wakuu,

Baada ya kuboreka vya kutosha na Bunge la katiba, hebu chukua popcorn tubadilishane mawazo.

Tangu kuumbwa kwa ulimwengu, kumekuwa na baadhi ya binadamu wachache ambao wamekuwa ni mahili sana kutumia umbumbumbu na udhaifu wa binadamu wenzao kuwadanganya na kujipatia kipato! mara nyingi watu hawa inasemekana wana kiwango kikubwa cha akili na ni wabunifu kupindukia... huwa tunawaita MATAPELI. hawa wapo kuanzia kule kijijini Namtumbo Ruvuma mpaka NYC, marekani! kwa mtazamo wangu wafuatao ni MATAPELI wakubwa zaidi kuwahi kutokea hapa nnchini ambao walitingisha na kuteka hisia za watu..

5. MANYAUNYAU
Huyu jamaa wote tunamfahamu, aliiitikisa sana miaka ya 2006,2007, na 2008! alijigamba kuwa akinywa damu ya paka anapata uwezo wa kimiujiza kufichua wachawi.! alizunguka mitaa karibia yote ya uswahilini hapa Dar, except huko udhunguni masaki n.k (sijui huko hakuna wachawi)! baada ya kuteka hisia za watu vya kutosha akaanza na ziara za mikoani... jamaa akaingiza mkwanja mrefu sana kwa kazi yake hii, nakumbuka miaka ile ya 2008 alinunua RAV 4 flani hivi kali sana, na mjengo wa maana.! sijui kwa sasa amepotelea wapi, inawezekana kazi yake ilikuwa effective wachawi .

Huyu tapeli manyaunyau , mimi alinitapeli laki Tatu na nusu mwaka 2012.
Hafai kabisa ni muongo wa waziwazi na anamtandao mkubwa sana.
Juzi juzi alikuwa na kesi ya milioni miambili kama sikosei.
Kaanae mbali sana. Hana chochote.
 
Salaam wakuu,

Baada ya kuboreka vya kutosha na Bunge la katiba, hebu chukua popcorn tubadilishane mawazo.

Tangu kuumbwa kwa ulimwengu, kumekuwa na baadhi ya binadamu wachache ambao wamekuwa ni mahili sana kutumia umbumbumbu na udhaifu wa binadamu wenzao kuwadanganya na kujipatia kipato! mara nyingi watu hawa inasemekana wana kiwango kikubwa cha akili na ni wabunifu kupindukia... huwa tunawaita MATAPELI. hawa wapo kuanzia kule kijijini Namtumbo Ruvuma mpaka NYC, marekani! kwa mtazamo wangu wafuatao ni MATAPELI wakubwa zaidi kuwahi kutokea hapa nnchini ambao walitingisha na kuteka hisia za watu..

5. MANYAUNYAU
Huyu jamaa wote tunamfahamu, aliiitikisa sana miaka ya 2006,2007, na 2008! alijigamba kuwa akinywa damu ya paka anapata uwezo wa kimiujiza kufichua wachawi.! alizunguka mitaa karibia yote ya uswahilini hapa Dar, except huko udhunguni masaki n.k (sijui huko hakuna wachawi)! baada ya kuteka hisia za watu vya kutosha akaanza na ziara za mikoani... jamaa akaingiza mkwanja mrefu sana kwa kazi yake hii, nakumbuka miaka ile ya 2008 alinunua RAV 4 flani hivi kali sana, na mjengo wa maana.! sijui kwa sasa amepotelea wapi, inawezekana kazi yake ilikuwa effective wachawi wameisha!!!!!!


4. ALEX MASSAWE
Huyu jamaa ni Tapeli "first class"!! alikuwa anatapeli kuanzia raia wenzake, serikali, mashirika mpaka matajiri wakubwa wakubwa! alitapeli sana watu nyumba, magari, mashamba na hata fedha! Serikali iliangaika sana na huyu jamaa kwa miaka kadhaa lakini hawakufua dafu, mpaka Interpol walipomkamata huko Dubai! inasemekana Jamaa alikuwa anapiga dili zake na watu wazito serikalini na bungeni!! Inasemekana kuna wabunge Watatu kutoka mkoa mmoja wa kaskazini ndio alikuwa anapiga nao sana ishu za madili ya gari za wizi na kusafisha fedha haramu.!

3. DAUDI BALALI

Binafsi nahisi huyu ni moja kati ya watanzania ma-genius zaidi kuwahi kutokea! huyu kipindi anasoma alirushwa sana madarasa kutokana na kiwango kikubwa cha akili hii ikapelekea yeye kusoma elimu ya msingi na sekondari kwa miaka 10 tu!!! akiwa na miaka 18 alijiunga na chuo kikuu cha Howard, marekani ambapo alitunukiwa shahada yake ya kwanza. Akiwa na miaka 25 alitunukiwa PHD na chuo kikuu cha John Hopkins.!! kisha akarudi nchini kuwa mchumi wa benki kuu mwaka 1967. Baadae kidogo akaajiriwa IMF ambako alifanya kazi huko kwa miaka 23 kabla ya Mzee Mkapa kumrudisha nnchini kama mshauri wake wa masuala ya uchumi na baadae kumfanya Gavana wa benki kuu.! kinachofanya kumuweka Balali kwenye list hii ni tukio alilolifanya la ukwapuaji kiasi cha Bilioni 164 za kitanzania pale benki kuu! Nafahamu kuna theories nyingi sana kuhusu UFISADI WA EPA, lakini kwa mujibu wa serikali ni kuwa Balali alikula njama yeye binafsi na wale wafanyabiashara wakwakwapua fedha pasipo serikali kujua! kwa maana hiyo BAlali alimpiga changa la macho Waziri Mighiro, raisi, na hata usalama wa taifa! hivi ni binadamu wangapi wana uwezo wa kupiga mtonyo na mchongo mkali kama huu! Balali anaweza.....


2. DESI
Inawezekana hata wewe ulikuwa ni mmoja wa "waliopanda mbegu" DESI.!
Haya yalikuwa ni maumivu ya Taifa.! watu walipanda mbegu, mvua zikanyesha, lakini ghafla jua likawaka mavuno yakaingia mitini.. kuna watu wakisikia hili jina tu kichwa kinaanza kuuma.!
wanasema wajinga ndio waliwao, wenzetu huko udhunguni mfano marekani, huu mfumo wa DESI ulishapigwa marufuku toka miaka ya 1920, wenyewe wanauita PONZI SCHEME (PYRAMID SCHEME), lakini sisi kwetu ulikuwa ni mfumo mpya na watu waliona DESI nmkombozi tukakimbilia, wajanja wakatula alafu wakasepa kimya kimya! ila ilitufundisha tusipende bure bure..


1. BABU WA LOLIONDO
Mpaka leo bado sijaelewa Babu aliwezaje kutupiga changa kiasi kile! hivi ni kwamba babu alikuwa kichwa sana, au media ilisaidia! kipindi kile kuna watu walitamani Babu atangazwe kuwa nabii, au shujaa wa taifa! mpaka wakuu wa nchi walitengeneza mpaka kiwanja kidogo cha ndege wakawa wanatua, wanapanga foleni, wanapiga magoti kwa unyenyekevu kabisa na kuachama midomo kama wanakula sakramenti.! kila kona ilikuwa ni Babu, babu, babuuu..... kila mtu anapigania akanywe KIKOMBE! sijui hata ilikuwaje, maana ghafla tu, ziiiiii!! babu kimya! kila mtu kimya kimya akashtuka huu ni uzuzu.... lakini sio mbaya sana kwa jero jero tulizo mchangia babu! maana angalau sasa ana maisha yanayo eleweka na siha yake iko poa! naamini tutakuta 'thawabu' zetu huko juu..

umetisha mkuu.
hao wako ni wakubwa sana,kuna fundi mmoja wa redio pale moshi mjini alikuwa anaitwa nyange huyu alikuwa tapeli balaa mkono alikuwa anauweza ukipeleka ki 77 chako usipokaa vizuri kimeuzwa,akinunua kiwanja karibu na kwako juaumelizwa kiwanja kwani anajenga mpakani kwako kabisa anaweka matoleo ya matofali yanaelekea kwako ukiuliza anakuambia fundi kakosea tu atayavunja ukikubali jua anatafuta pakutapeli akipata pesa anakuja na malori ya matofali mchanga na simenti ndani ya siku mbili nyumba imepauliwa na kuwekwa mpangaji.
ukichelewa anakushitaki wewe kwa kusumbua wapangaji wake.alikuwa na kesi kama 20 kwa wakati mmoja.
 
Yuuuuup!
Jamaa aliyeingia ubia aliulizwa swali moja tu!
"Ina maana nilikuachia paa langu liwe kiwanja cha nyumba yako?"

HAHAHAHAHAA partner hoooii....halafu matapeli hawalogekiee maana duhh watu wanawaacha hivihivi tu??
 
Babu wa loliondo ulikuwa mpango wa gvt intelligence kutuliza fujo za chadema,balali unamsingizia tu kwakuwa yeye ndiyo anamajibu ya maswali magumu ila wezi wa bot wapo hapahapa tz, alex masawe si tapeli ni jambazi wa magari na alishirikiana na yule mbunge aliyetajwa na abdalah zombe kuwa ni jambazi wa magari. Matapeli maarufu ni papa musofe, msama na wengine wote wanaojiita mapapaa

!
!
chukua tano mwana.....babu ulikuwa mpango maalumu kwa ajili ya chadema. Kama nikikumbuka vizuri ni kwamba kulikuwa na mauaji Arusha by the time.
Matapeli au "maprofesa" yupo mmoja hapo anaitwa Lusekelo yule ni tapeli wa kutupwa.
 
Mkuu Kiranga,

Hii stori ni ya kweli? Kama ni kweli huyu jamaa anakamata namba moja. Julius huyu aliyekuwa anaogopwa bado kidume kikamuingiza mjini.

Hapana, nimemkubali.

Watu wa Musoma na Wahaya ni watani, hakuna kitu hapa. Kilichotumika hapa ni guts siyo akili. Mimi Babu wa Loliondo na jopo lake namgwaya sana, watu wanaotumia akili ni hao!
 
...Uzi umetulia mkuu ila hapo namba 2 ni DECI na sio DESI! Cheki hizo C na S. Lastborn wangu hapa amekununia mbaya...anasema kama vipi umpoze asikufikishe kwa pilato kwa kumsingizia utapeli na kumuharibia jina!! teh teh teh...
 
...Uzi umetulia mkuu ila hapo namba 2 ni DECI na sio DESI! Cheki hizo C na S. Lastborn wangu hapa amekununia mbaya...anasema kama vipi umpoze asikufikishe kwa pilato kwa kumsingizia utapeli na kumuharibia jina!! teh teh teh...

Hahahahah! Nimekusoma mkuu, ila Daah kama umempa hlo jina miaka ya karibuni baada ya hawa jamaa kutupiga hela zetu inabidi akufikishe kwa pilato aisee..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom