Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 14,326
- 40,593
Orodha hii sio rasmi, ni utafiti wangu binafsi. Unapingika, unajadilika na unarekebishika.
10.Mohamad.
Huyu ni muasisi wa dini ya kiislamu. Alikua mwanamapinduzi, askari na mwanasiasa. Kulingana na imani ya waislamu ndie mjumbe wa mwisho wa Mungu. Jina lake ni maarufu sana duniani. Changamoto umaarufu wake unaishia kwenye nchi za kiislamu au ambazo angalao dini ya kiislamu imeenea. Katika nchi ambazo hakuna kabisa uislamu sio ajabu kumkuta mtu mzima kabisa hajui chochote kuhusu Mohamad.
9.Bob Marley.
Mwanamziki wa muziki aina ya reggae. Huyu jamaa ndio taswira ya huu mziki. Nyimbo zake aliamasisha zaidi masuala ya ukombozi na kujenga umoja, upendo na mshikamano.
8.Pele na Maradona.
Nimeshindwa kuwatenganisha hawa jamaa wawili maana umaarufu wao ni kama upo kwenye mzani sawa. Ni wachezaji mahiri ambao waliu-define mchezo wa mpira wa miguu. Pele ni mzaliwa wa Brazil na Maradona ni mzaliwa wa Argentina. Pele alianza kucheza mpira miaka mingi kidogo kumzidi Maradona. Pamoja na kuwepo kwa wachezaji wengine mahiri hapa duniani lakini Pele na Maradona ni kama wameshajijengea daraja lao ambalo hakuna mchezaji mwingine anaweza kuvuka.
7.Bruce Lee.
Alitambulika kwa umahiri wake wa upiganaji wa mtindo wa karate na kong fu. Kumekua na mjadala watu wakihoji kama Bruce Lee ndie mpiganaji mahiri zaidi kutokea. Wanaipinga hilo suala hoja wanayoitumia ni kwamba jamaa hakuwahi kushiriki na kushinda mashindano rasmi. Ngumi zake ni za kwenye movie na sanaa za maonyesho tu. Lakini pamoja na hayo bado haiondoi ukweli Bruce ni moja ya watu maarufu zaidi kuwahi kutokea dunian na amekua kioo na role model kwa watu wote wanaopenda kong fu.
6.Tupac.
Alitambulika kwa umahiri wake katika mziki wa rap au hip hop. Nini kilimpa umaarufu Tupac kuzidi wasanii wengine?
Je ni umahiri wa kurap? Sina uhakika kama anawazidi Nas, lil wayne n.k
Je ni ile style yake ya kurap fasta ambayo inahitaji pumzi nyingi? Sina uhakika kama anamzidi Eminem.
Je ni ile ngoma yake ya dear mama? Binafsi nafikiri ile ndio hit song kali ya muda wote ya kumsifia mama( Lucas Mwashambwa, choice variable na machawa wengine nieleweni vizuri hapa. Simaanishi huyo mama yenu mnaomfikiria nyie)
Au ilitokea tu zali mziki wa hip hop ukatengenezewa taswira ya huyu jamaa?
5.Adolf Hitler.
Mwamba huyu hapa. Harakati zake za kutaka kuitawala dunia zilisababisha awe center ya vita ya pili ya dunia. Wayahudi ndio hawataki hata kumsikia huyu muhuni
4. Lionel Messi.
Sina mengi ya kumuongelea huyu jamaa. Kwa kifupi tu inasemekana ndie mchezaji mpira wa miguu mahiri zaidi kuwahi kutokkea duniani. Mashabiki wa soka wa kizazi chake tuna bahati sana ya kumwona huyu jamaa akicheza maana habari zake zitakuwepo juu kabisa kwenye kumbukumbu za kidunia mpaka mwisho wa dohari
3.Cristiano Ronaldo.
Mchezaji wa mpira wa miguu ambaye kwa miaka mingi amekua mshindani wa Messi huku wakiwagawa mashabiki. Umaarufu wake ulianza kupanda kwa kasi baada ya kusajiriwa na manchester united kwa mara ya kwanza akitokea timu ya sporting lisbon ya nyumbani kwake Ureno.
Namba hazidanganyi. Ndie binadamu mwenye wafuasi wengi zaidi katika mitandao yote ambayo yupo active. Style yake ya ushangiliaji inayotambulika kwa jina la siuuu ndio style maarufu zaidi ya ushangiliaji. Ndie mchezaji ambae ni role model wa wachezaji wengi sana mahiri wanaotamba sasa mfano mbappe, vinicious, kravatkhelia, dembele n.k. Ndie mchezaji ambae ni kipenzi zaidi cha watoto.
Tofauti yake na Messi ni kwamba Messi anaonekana kupendwa na wanaopenda mpira pamoja na mashabiki wa timu alizocheza tofauti na Ronaldo anapendwa na hata wasiokua na mapenzi na mpira wa miguu pamoja na mashabiki wa timu ambazo hajacheza.
2.Michael Jackson.
Madogo wa GenZ wanaweza kushangaa kidogo hapa maana hawakuwepo nyakati ambazo huyu jamaa alikua ameiweka dunia chini ya nyayo za miguu yake.
Ndie msanii wa kwanza mweusi wimbo wake kupigwa mtv. Aliibuka katika nyakati ambazo ubaguzi wa rangi umeshamiri kiasi cha kuwepo na sheria ya kuzuia nyimbo za watu weusi kupigwa kwenye baadhi ya station. Wimbo wake wa billie jean ulifanya mtv waondoe huo utaratibu.
Katika prime yake alishawahi kupanda jukwaani na kusimama tu kwa takribani dakika 2. Ukumbi ukalipuka kwa shangwe mpaka watu wakazimia kwa sababu ya furaha isiyo kifani. Just imagine hali hiyo inatokea wakati mtu kasimama tu bila kuimba chochote.
Nyakati zake ilifika hatua super market zikawa zinamtengea muda wa kufanya shopping, yaani akitaka kufanya manunuzi anawasiliana na uongozi wa super market watu wote watoke kwanza ili yeye aingie kufanya manunuzi akiwa peke yake. Maana kila anapoingia shughuli zilikua zinasimama.
Kumbuka hayo yote yalitokea kwenye nyakati ambazo hakuna mitandao ya kijamii
1.Yesu.
Anatambulika katika dini ya ukristo kama masiha. Sidhani kama kuna pembe ya dunia unaweza kwenda leo hii ukakutana na jamii ya watu wanaoishi katika mtindo huu wa modern civilization na hawamjui kabisa Yesu. Najua hapa utaibuka mjadala wa kuhoji. Je, huyu Yesu alishawahi kuwepo duniani au ni fictional character tu?
Wanahistoria nguli wanakubaliana kwamba Yesu ni binadamu halisi alikuwepo. Aliishi uko Bethlehemu, Nazareti na Misri. Alikua fundi selemala na mtabibu wa tiba za jadi(kibongo bongo ni kama hawa wakina dr.mwaka). Pia alikua mwanaharakati anaepingana na mienendo ya watawala(mfano Tundu Lissu kwa sasa). Mafundisho yake yalimsababishia kuwa na mikwaruzano na watawala kiasi cha kufikia kukamatwa na kuhukumiwa kifo.
Madai ya kwamba ni mtoto wa Mungu, alifanya miujiza, alifufuka hayo ni ya kiimani zaidi. Hayana uthibitisho wa kihistoria wala sayansi.
NB: Adam na Hawa hawapo kwenye list kwa sababu hakuna uthibitisho kwamba walikuwepo hapa duniani. Wanahistoria nguli wanasema habari yao ni myth tu za wayahudi.