Matapeli wakubwa 5 kuwahi kutokea Tanzania

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
May 7, 2013
6,557
25,671
Salaam wakuu,

Baada ya kuboreka vya kutosha na Bunge la katiba, hebu chukua popcorn tubadilishane mawazo.

Tangu kuumbwa kwa ulimwengu, kumekuwa na baadhi ya binadamu wachache ambao wamekuwa ni mahili sana kutumia umbumbumbu na udhaifu wa binadamu wenzao kuwadanganya na kujipatia kipato! mara nyingi watu hawa inasemekana wana kiwango kikubwa cha akili na ni wabunifu kupindukia... huwa tunawaita MATAPELI.

Hawa wapo kuanzia kule kijijini Namtumbo Ruvuma mpaka NYC, marekani! kwa mtazamo wangu wafuatao ni MATAPELI wakubwa zaidi kuwahi kutokea hapa nnchini ambao walitingisha na kuteka hisia za watu..

5. MANYAUNYAU
Huyu jamaa wote tunamfahamu, aliiitikisa sana miaka ya 2006,2007, na 2008! alijigamba kuwa akinywa damu ya paka anapata uwezo wa kimiujiza kufichua wachawi.! alizunguka mitaa karibia yote ya uswahilini hapa Dar, except huko udhunguni masaki n.k (sijui huko hakuna wachawi)! baada ya kuteka hisia za watu vya kutosha akaanza na ziara za mikoani...

Jamaa akaingiza mkwanja mrefu sana kwa kazi yake hii, nakumbuka miaka ile ya 2008 alinunua RAV 4 flani hivi kali sana, na mjengo wa maana.! sijui kwa sasa amepotelea wapi, inawezekana kazi yake ilikuwa effective wachawi wameisha!!!!!!

4. ALEX MASSAWE
Huyu jamaa ni Tapeli "first class"!! alikuwa anatapeli kuanzia raia wenzake, serikali, mashirika mpaka matajiri wakubwa wakubwa! alitapeli sana watu nyumba, magari, mashamba na hata fedha! Serikali iliangaika sana na huyu jamaa kwa miaka kadhaa lakini hawakufua dafu, mpaka Interpol walipomkamata huko Dubai!

Inasemekana Jamaa alikuwa anapiga dili zake na watu wazito serikalini na bungeni!! Inasemekana kuna wabunge Watatu kutoka mkoa mmoja wa kaskazini ndio alikuwa anapiga nao sana ishu za madili ya gari za wizi na kusafisha fedha haramu.!

3. DAUDI BALALI

Binafsi nahisi huyu ni moja kati ya watanzania ma-genius zaidi kuwahi kutokea! huyu kipindi anasoma alirushwa sana madarasa kutokana na kiwango kikubwa cha akili hii ikapelekea yeye kusoma elimu ya msingi na sekondari kwa miaka 10 tu!!! akiwa na miaka 18 alijiunga na chuo kikuu cha Howard, marekani ambapo alitunukiwa shahada yake ya kwanza.

Akiwa na miaka 25 alitunukiwa PHD na chuo kikuu cha John Hopkins.!! kisha akarudi nchini kuwa mchumi wa benki kuu mwaka 1967. Baadae kidogo akaajiriwa IMF ambako alifanya kazi huko kwa miaka 23 kabla ya Mzee Mkapa kumrudisha nnchini kama mshauri wake wa masuala ya uchumi na baadae kumfanya Gavana wa benki kuu.! kinachofanya kumuweka Balali kwenye list hii ni tukio alilolifanya la ukwapuaji kiasi cha Bilioni 164 za kitanzania pale benki kuu!

Nafahamu kuna theories nyingi sana kuhusu UFISADI WA EPA, lakini kwa mujibu wa serikali ni kuwa Balali alikula njama yeye binafsi na wale wafanyabiashara wakwakwapua fedha pasipo serikali kujua! kwa maana hiyo BAlali alimpiga changa la macho Waziri Mighiro, raisi, na hata usalama wa taifa! hivi ni binadamu wangapi wana uwezo wa kupiga mtonyo na mchongo mkali kama huu! Balali anaweza.....

2. DECI
Inawezekana hata wewe ulikuwa ni mmoja wa "waliopanda mbegu" DECI.!
Haya yalikuwa ni maumivu ya Taifa.! watu walipanda mbegu, mvua zikanyesha, lakini ghafla jua likawaka mavuno yakaingia mitini.. kuna watu wakisikia hili jina tu kichwa kinaanza kuuma.!

wanasema wajinga ndio waliwao, wenzetu huko uzunguni mfano Marekani, huu mfumo wa DECI ulishapigwa marufuku toka miaka ya 1920, wenyewe wanauita PONZI SCHEME (PYRAMID SCHEME), lakini sisi kwetu ulikuwa ni mfumo mpya na watu waliona DESI nmkombozi tukakimbilia, wajanja wakatula alafu wakasepa kimya kimya! ila ilitufundisha tusipende bure bure..

1. BABU WA LOLIONDO
Mpaka leo bado sijaelewa Babu aliwezaje kutupiga changa kiasi kile! hivi ni kwamba babu alikuwa kichwa sana, au media ilisaidia! kipindi kile kuna watu walitamani Babu atangazwe kuwa nabii, au shujaa wa taifa! mpaka wakuu wa nchi walitengeneza mpaka kiwanja kidogo cha ndege wakawa wanatua, wanapanga foleni, wanapiga magoti kwa unyenyekevu kabisa na kuachama midomo kama wanakula sakramenti.! kila kona ilikuwa ni Babu, babu, babuuu.....

Kila mtu anapigania akanywe KIKOMBE! sijui hata ilikuwaje, maana ghafla tu, ziiiiii!! babu kimya! kila mtu kimya kimya akashtuka huu ni uzuzu.... lakini sio mbaya sana kwa jero jero tulizo mchangia babu! maana angalau sasa ana maisha yanayo eleweka na siha yake iko poa! naamini tutakuta 'thawabu' zetu huko juu..
 
TAFADHALI: Mods naomba tuheshimiane, acheni huu uzi maana naona siku hizi mmenicharukia sana..


3. DAUDI BALALI
Binafsi nahisi huyu ni moja kati ya watanzania ma-genius zaidi kuwahi kutokea! huyu kipindi anasoma alirushwa sana madarasa kutokana na kiwango kikubwa cha akili hii ikapelekea yeye kusoma elimu ya msingi na sekondari kwa miaka 10 tu!!! akiwa na miaka 18 alijiunga na chuo kikuu cha Howard, marekani ambapo alitunukiwa shahada yake ya kwanza. Akiwa na miaka 25 alitunukiwa PHD na chuo kikuu cha John Hopkins.!! kisha akarudi nchini kuwa mchumi wa benki kuu mwaka 1967. Baadae kidogo akaajiriwa IFM ambako alifanya kazi huko kwa miaka 23 kabla ya Mzee Mkapa kumrudisha nnchini kama mshauri wake wa masuala ya uchumi na baadae kumfanya Gavana wa benki kuu.! kinachofanya kumuweka Balali kwenye list hii ni tukio alilolifanya la ukwapuaji kiasi cha Bilioni 164 za kitanzania pale benki kuu! Nafahamu kuna theories nyingi sana kuhusu UFISADI WA EPA, lakini kwa mujibu wa serikali ni kuwa Balali alikula njama yeye binafsi na wale wafanyabiashara wakwakwapua fedha pasipo serikali kujua! kwa maana hiyo BAlali alimpiga changa la macho Waziri Mighiro, raisi, na hata usalama wa taifa! hivi ni binadamu wangapi wana uwezo wa kupiga mtonyo na mchongo mkali kama huu! Balali anaweza.....

..

Mkuu una kithethe cha vidole eeh? hivi ni IFM au IMF?
 
list yako ni fake.kuna matapeli sijawaona.
papa msofe,ndama mtoto wa ng'ombe,ostaz juma na musoma,cheif kiumbe nk.

Hahaha, Ndama mtoto ya ng'ombe I will personally vouch for his mischief.

Alinifanya mpaka nimfungulie kesi polisi Magomeni, enzi hizoooooo.

Kuna mchizi mmoja anaitwa Batenga, alikuwa tapeli kabla neno la tapeli halijajulikana.

Jamaa alienda kwa Nyerere akamkuta Nyerere anafyatua matofali kibao, akawa anapiga naye story huku ananyoosha mikono kwenye matofali.

Kesho yake Nyerere akasafiri, jamaa akaja na malori, akaanza kusomba matofali, alipoulizwa akawa mkali, nyie hamkuniona nakubaliana na mzee jana hapa?

Walinzi wa Nyerere wakaogopa kuuliza, Nyerere akazidiwa na kazi, kuja kushtuka kaibiwa matofali kibao hakuwa hata na muda wa kufuatilia.

Batenga akajenga nyumba ya nyuma ya Karibu Hotel.

Or so goes the legend.
 
Hahaha, Ndama mtoto ya ng'ombe I will personally vouch for his mischief.

Alinifanya mpaka nimfungulie kesi polisi Magomeni, enzi hizoooooo.

Kuna mchizi mmoja anaitwa Batenga, alikuwa tapeli kabla neno la tapeli halijajulikana.

Jamaa alienda kwa Nyerere akamkuta Nyerere anafyatua matofali kibao, akawa anapiga naye story huku ananyoosha mikono kwenye matofali.

Kesho yake Nyerere akasafiri, jamaa akaja na malori, akaanza kusomba matofali, alipoulizwa akawa mkali, nyie hamkuniona nakubaliana na mzee jana hapa?

Walinzi wa Nyerere wakaogopa kuuliza, Nyerere akazidiwa na kazi, kuja kushtuka kaibiwa matofali kibao hakuwa hata na muda wa kufuatilia.

Batenga akajenga nyumba ya nyuma ya Karibu Hotel.

Or so goes the legend.

Duh!! Huyo naye kiboko! Yaani alimtapeli baba wa taifa hivihivi na kwa wakati ule tuliamini hakuna mtu aliyekuwa na akili duniani kama nyerere.
 
Back
Top Bottom