Matapeli wa miaka ya 90's walikuwa balaa sana

Matapeli wa miaka ya 90's walikuwa balaa sana

Enzi hizo nikatinga mkoa flani nikajifanya mimi Prof J,enzi zile za zama za mawe,nikalamba advance payment,siku ya show kuna mwana akastukia chezo maana nilichokuwa nafanya kwa Stage hakifanani na mzee wa mitulinga,nikajifanya naenda chooni mazee hizo mbio nilizotimua Subaru haikamati,mbele kwa mbele nikadandia fuso la viazi ndiyo kimojaaa.
Dah una bahat mkuu wangekukamata wangekulawiti ukumbi mzima
 
Mtu naweza kuugua kwa muda mrefu na katika kuhangaika kutafuta tiba akajikuta amekubali kununua dawa kutoka kwa matapeli ambayo haitibu. Au akatapeliwa na mganga au hawa wachungaji feki.
Kweli na kundi hilo hua wanatapeliwa sana kwa ajili ya shida zao.
Ila vitu vingine ni kujitaftia tu laana zisizo na msingi, mtu anapambania maisha inakuja tena unamtapeli
 
Kipind niko primary walikuja watu wawili kwa jirani wakamkuta housegal na mtoto wa mwenye nyumba wakawaambia mama yenu katuagiza vitenge anataka akashone.

Na yule mama alikua anapenda vitenge so alikua navyo vingii sasa kuuliza kitenge kipi wakasema tupe tu vyote ataenda kuchagua mwenyew vingine atarud navyo basi dada wa watu akakusanya vyote na begi akawapa kwa ajili ya kubebea.

Jioni maza house anarudi katika story dada akamwambia kuhusu wale wageni, mama akajua ashatapeliwa. Akampeleka yule h/girl polisi kutoa maelezo ila ikagundulika hahusiki dada akaachiwa na vitenge vikaenda.

Zamani watu walikua wanaiba kirahisi sio kama saivi
Hahaha
 
Mkuu nenda kwenye uzi wa kula tunda kimasihara ndiyo utajua mapenz ni nyookoo
Daaah hatariiii Sana binadamu utashi umetuishia yaan tumekua kama bata kuku mbuzi kondooo yaan tunapandana ovyo ovyo no ustaarabu kabsaaa
Natembeleaga ule Uzi mkuu,
Watu Wana stress sana na haya maisha
 
Ahsante kwa UPDATES basi mie nikijua amefariki zamani daaah
Nakumbuka1984 niko Morogoro, nilikuwa nimejifungua. Kumbuka ni baada yavita ya Kagera. Kila kitu ni foleni na ukiwa na bahati utapata bila bahati basi.
Nilibahatika kupata sukari kilo 5 za mchongo na ndani nilikuwa na vitenge pair 2 na khanga vile vile. Walikuja watu kesho yake wakamwambia ndugu yangu aliyekuwa ananisaidia kuangalia mwanangu awape vutu vyote nilivyonunua jana yake. Walisema ni polisi. Basi niliporudi nikakuta ndugu yangu analia alikuwa mdogo miaka 10 alikuwa anasubiri aende shule. Nilikaa kimya ila nilihisi ni watu wangu wa karibu. Hiyo miaka kuanzia mwaka 80 mpaka mwishoni mwa tisini watu tulilizwa sana. Mimi nililizwa sana.

Tusisahau Bijampola walivyovuna wasikopanda kwa kutapeli wasafiri wa kwenda bukoba at the end basi halikupatikana wala wahusika.
 
[emoji3][emoji3] umenikumbusha enzi zile miaka ya 1908 enzi zile tunajenga reli ya kati kwenda tabora... Nilikua naenda Dodoma nakujifanya Mimi ndo Mkwawa toka Iringa basi napewa mpka mke wa kulala nae bure
 
Nilitumwa nikanunue chumvi ya mawe halafu chenji nichukue maduka matatu ya kijiji yote hamna nkasema leo itapatikan tu. Chumvi nilikosa na kurudi nakuta wamelamba Radio ya mkulima band3 asee.
 
Kweli na kundi hilo hua wanatapeliwa sana kwa ajili ya shida zao.
Ila vitu vingine ni kujitaftia tu laana zisizo na msingi, mtu anapambania maisha inakuja tena unamtapeli
Mkuu hii dunia kuna watu wenye roho mbaya kuliko wanyama. Mnyama anaweza kuua binadamu kwa sababu anajihami lakini binadamu anaweza kuua ili tu apate starehe. Hili la dawa za utapeli ni laana. Watu kama hawa kina ''dr' Mwaka ni matapeli per se. Halafu wasivyo na huruma ''dawa'' zao wanauza ghali mno. Hawana huruma yoyote na wagonjwa ambao wengine wamekopa ili kutafuta kupona.
 
Wanauza bei sababu si wanajua mtu atafanya lolote ili anunue, ubinadamu hakuna
 
Nakumbuka1984 niko Morogoro, nilikuwa nimejifungua. Kumbuka ni baada yavita ya Kagera. Kila kitu ni foleni

Tusisahau Bijampola walivyovuna wasikopanda kwa kutapeli wasafiri wa kwenda bukoba at the end basi halikupatikana wala wahusika.

Shikamoo mkuu
 
Advance niko na mwanangu ye anasoma Sangu mi Meta, tulikuwa geto, kuna ticha mmoja wa hivi vi-Education center moja hivi mitaa ya karibu na Meta Sec achana na (Mbalepo ya Mbalizi Road).

Huyu ticha alikuwa anataka F-991 Calcukator, sasa tulikuwaga na "gaka" letu lipo kwenye box jipya na menu yake na "Og" mbili ambazo tulikuwa tunatumia. Tulivosikia mteja tukaenda na mwanangu asubuhi asubuhi, mwanangu kavaa kawaida mimi niko na Uniform, kufika pale Ticha akaitwa ,alikuwa anapiga pindi class hapo tuko na lile gaka kwenye box na menyu yake na Og kwenye box lake na menyu yake. Ticha alivokuja mwamba akaanza kumwambia tunauza caluculator, Akaomba aione mi nikampa Og(Ile feki mwamba ndo alikuwa nayo).

Jamaa kaiangalia pale akauliza bei, tukamwambia elf 30, akaomba atupe 25 tukamwambia hela haitoshi atupe elf 28, akawa anajivuta ,akasema ana 27, tukajifanya tunaondoka yeye akawa anarudi class, tulivofika getini ,mwanangu akanipasia gaka nikampa og, tukarudi fasta kabla hajaingia darasani tukamwambia tupe hiyo hiyo (27 elf) jamaa akatoa hela akachukua gaka tukatoweka haraka.

Haooo mpaka geto, nikatoa uniform tukaenda Kalobe kulewa ulanzi. Sikwenda shule kama siku 3, nikawa nawaza huenda Ticha alinikariri ataenda getini kwa kina Mng'ong'o kunivizia.
Aya bwana mitaa ya yetu hiyo,, Mbalepo
 
[emoji3][emoji3] umenikumbusha enzi zile miaka ya 1908 enzi zile tunajenga reli ya kati kwenda tabora... Nilikua naenda Dodoma nakujifanya Mimi ndo Mkwawa toka Iringa basi napewa mpka mke wa kulala nae bure
Ww umetisha,, unamiaka mingapi sasa
 
Neno "kanyaboya" lilitokana na bondia flani wa Burundi alikuja Tanzania kuzichapa alikuwa ba mikwara saana unaambiwa kabla ya pambano alikuwa anakimbia akiwa na gloves na mikwara kibao pale kariakoo.

Siku ya pambano yule bwana aitwae kanyaboya kilimkuta Kama bwana Mandonga.

Ndo watu wakaanza kusema kanyaboya kwa kitu Cha ubabaishaji au utapeli.

Kanyaboya
Stori za wahenga hizi
 
Kuna mwalimu alikuwa mkali balaa shuleni kwetu, anapiga kwa sifa sana!, Tukamkomoa kumtapeli deli Zima la aicream
 
Advance niko na mwanangu ye anasoma Sangu mi Meta, tulikuwa geto, kuna ticha mmoja wa hivi vi-Education center moja hivi mitaa ya karibu na Meta Sec achana na (Mbalepo ya Mbalizi Road).

Huyu ticha alikuwa anataka F-991 Calcukator, sasa tulikuwaga na "gaka" letu lipo kwenye box jipya na menu yake na "Og" mbili ambazo tulikuwa tunatumia. Tulivosikia mteja tukaenda na mwanangu asubuhi asubuhi, mwanangu kavaa kawaida mimi niko na Uniform, kufika pale Ticha akaitwa ,alikuwa anapiga pindi class hapo tuko na lile gaka kwenye box na menyu yake na Og kwenye box lake na menyu yake. Ticha alivokuja mwamba akaanza kumwambia tunauza caluculator, Akaomba aione mi nikampa Og(Ile feki mwamba ndo alikuwa nayo).

Jamaa kaiangalia pale akauliza bei, tukamwambia elf 30, akaomba atupe 25 tukamwambia hela haitoshi atupe elf 28, akawa anajivuta ,akasema ana 27, tukajifanya tunaondoka yeye akawa anarudi class, tulivofika getini ,mwanangu akanipasia gaka nikampa og, tukarudi fasta kabla hajaingia darasani tukamwambia tupe hiyo hiyo (27 elf) jamaa akatoa hela akachukua gaka tukatoweka haraka.

Haooo mpaka geto, nikatoa uniform tukaenda Kalobe kulewa ulanzi. Sikwenda shule kama siku 3, nikawa nawaza huenda Ticha alinikariri ataenda getini kwa kina Mng'ong'o kunivizia.

[emoji23][emoji23][emoji23] huu utapeli umenichekesha sana hasa iyo conclusion.
 
Back
Top Bottom