Advance niko na mwanangu ye anasoma Sangu mi Meta, tulikuwa geto, kuna ticha mmoja wa hivi vi-Education center moja hivi mitaa ya karibu na Meta Sec achana na (Mbalepo ya Mbalizi Road).
Huyu ticha alikuwa anataka F-991 Calcukator, sasa tulikuwaga na "gaka" letu lipo kwenye box jipya na menu yake na "Og" mbili ambazo tulikuwa tunatumia. Tulivosikia mteja tukaenda na mwanangu asubuhi asubuhi, mwanangu kavaa kawaida mimi niko na Uniform, kufika pale Ticha akaitwa ,alikuwa anapiga pindi class hapo tuko na lile gaka kwenye box na menyu yake na Og kwenye box lake na menyu yake. Ticha alivokuja mwamba akaanza kumwambia tunauza caluculator, Akaomba aione mi nikampa Og(Ile feki mwamba ndo alikuwa nayo).
Jamaa kaiangalia pale akauliza bei, tukamwambia elf 30, akaomba atupe 25 tukamwambia hela haitoshi atupe elf 28, akawa anajivuta ,akasema ana 27, tukajifanya tunaondoka yeye akawa anarudi class, tulivofika getini ,mwanangu akanipasia gaka nikampa og, tukarudi fasta kabla hajaingia darasani tukamwambia tupe hiyo hiyo (27 elf) jamaa akatoa hela akachukua gaka tukatoweka haraka.
Haooo mpaka geto, nikatoa uniform tukaenda Kalobe kulewa ulanzi. Sikwenda shule kama siku 3, nikawa nawaza huenda Ticha alinikariri ataenda getini kwa kina Mng'ong'o kunivizia.