Matapeli wa miaka ya 90's walikuwa balaa sana

Matapeli wa miaka ya 90's walikuwa balaa sana

Hiyo Issue naikumbuka wakamuambia zile nguzo atakuwa anafungia ng'ombe zake na walimpa risiti (Cash sale imeandikwa Matapeli)

Kama wewe ni mzaliwa wa Moro hii stori ipo ya zamani sana na matepeli walikuwa wanajulikana ingawa kwa ss wanekuwa wazee na wengine swala tano hv sasa
 
Hiyo Issue naikumbuka wakamuambia zile nguzo atakuwa anafungia ng'ombe zake na walimpa risiti (Cash sale imeandikwa Matapeli)
Na pale JUWATA stendi ya Vibajaji zamani ilikuwa stand ya Coaster za Dar - Moro yale maduka ya wahindi kuna mhindi mmoja walimuwekea kichwa cha mtu kwenye box wakataka awahifadhie baadae wakaja maaskari (ila sina uhakika kama ni askari kweli au feki) wakamtoa mpunga mrefu yule mhindi.
 
Duuuh hii sikuipata ilinipita labda nilikuwa shule.
 
Ila zamani bhana timu ya ligi kuu imevaa jezi za Manchester United na hawana wasiwasi wowote,halafu namuona Azim Dewji mwanzo kule,hii familia ya Dewji imeanza ujanjaujanja mapema sana kwenye club ya Simba

Huyu Azim Dewji amewabebesha wachezaji wa Simba enzi hizo vitu vya haramu vingi kwenye mipira aliyokuwa anawabebesha!!
 
Na-comment kuhusu mstari wa mwisho. Hata siku hizi watu bado wanaiba kirahisi mno. Bado kuna watu wanapigwa kirahisi mno na hata ukisimuliwa huwezi kuamini kama kuna watu wajinga kiasi hiki. Mtu anaweza kuambiwa wekeza sh milioni moja baada ya wiki zitazaa na kuwa sh milioni mbili na akakubali bila hata kutafakari. Utadhani ni bado tuko enzi za Abunuasi za sufuria kuzaa.

Si sawa tu na hao wanaopigwa kila siku kwenye KU BETI!!!
 
Kuna mmasai alikuwa anatafuta kiwanja kikubwa, ss pale msikitini kwa chini kule kuna shule ya sekondari ina eneo kubwa kuna ukoka mzuri sana. Yule mmasai walipomuuzia alimwelekeza kule kwenye ukoka ataweka ng"ombe na maji watakunywa pale mtoni kuna mto karibu sana. Sasa wakati wa Swala km kawaida watu wanaenda masjid masai anafukuza watu eeehhn nani wewe unachezea sehemu yangu anawafukuza na bakora. Basi hadi polisi wakaja pale kumtoa masai maana ilikuwa kasheshe.
Duh
 
Si sawa tu na hao wanaopigwa kila siku kwenye KU BETI!!!
Kubet kupi ndugu Bulesi . Kuna kubeti eg mpira huku siyo kupigwa japo uwezekano wa kushinda ni mdogo. Kubeti niliko na wasiwasi nako ni huku kunakofanywa na watu kama Clouds na redio nyingine. Hawa nina wasiwasi mno kama wanaweza kufanya mambo kihalali!
 
Kubet hata kwenye huo mpira pia ni KAMALI!!! Huo mchezo unaofanywa na hivyo vituo vya redio ni wizi wa mchana wanawaibia maskini wanaowapa tamaa kuwa watatajirika kumbe ndio wanawafirisi!!
 
Back
Top Bottom