Matapeli wa miaka ya 90's walikuwa balaa sana

Matapeli wa miaka ya 90's walikuwa balaa sana

jamaa alitapeli muhindi..
alimpelekea muhindi sampo za pesa(rupia)zile zenye tobo katikati.

"akamwambia anatafuta kama izo na kila moja atalipa donge nono sana"

muhindi tamaa ikamuwakia akaona hapa anaenda kuongeza utajiri....

baada ya siku mbili akaja mtu mwingine anauza zile hela zenye tobo katikati.

muhindi akazinunua kwa fujo zote akijua baada ya wiki mnunuzi atakuja ampige bei anayotaka..

kwani mnunuzi alitokea tena!!ndo akawa ameenda kwa mama sirudi.
 
Mimi niliwahi kutapeliwa pale moshi mjini enzi za miaka 2002 namalizia md kcmc ...nilikutana na matapeli wakanisimamisha eti wanikague kiasi cha pesa nilichonacho,kuna maduka yalivunjwa jana yake ..basi jamaa wakanishusha kule njoro eti kituo cha polisi....
 
Ukipenda shortcut lazima utapeliwe.Mimi tangu nitapeliwe pale DDC Kariakoo mwaka 1998 sijatapeliwa tena hadi leo😀
Ukiniambia sijui Almas nakuelekeza pa kwenda kuziuza.Nimemaliza
 
Ila dokta shika ni kiboko zaidi ya mamba aisee hivi alisharudi kwao Urusi au vipi?
 
Kuna jamaa alikujaga mkoani kwetu enzi za chemsha bongo ina hit eti anajifanya Nigga J, basi watu wakawa wanamshobokea ananunuliwa mihogo ya kukaanga na kachumbari bure. Nigga J gani hana hata ela ya kununua mihogo. Kakalili mistari anawashushia rhymes wana.
Looking back nacheka sana.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji23]
 
Nakumbuka mmasai mmoja aliuziwa Msikiti mkubwa wa Ijumaa wa Morogoro.Sisi tunaenda kufanya Ibada tunafukuzwa na yule masai.Mbona ilikuwa mfacane war ile .
😂😂😂😂😂 Mkuu ya Kweli ? Daaah Nimecheka Sana kwa sauti kuubwaaa
 
Watu waishaibiwa saana miaka hiyo anakuja juma nature, sura ya nature hawaijui wanaletewa mjomba tu, wanagongwa pesa, imesiha hiyo[emoji23]
 
Back
Top Bottom