Inasikitisha sana ukisoma comments za wanaJF wengine. Sehemu ambayo inategemewa kuwa kimbilio la suluhisho badala yake inageuzwa kijiwe cha kahawa na sehemu ya kuongea upepo.
Suala la matamko ya waislamu linapewa msukumo mkubwa na uongozi wa nchi. Mpaka sasa Raisi hajakemea maaskofu wala masheikh wanaotoa matamko. Hii ni weakness kubwa sana ya Raisi wetu.
Angekuwa kiongozi jasiri angetamka waziwazi bila kuficha na kuwakemea viongozi wa dini kuacha kupandikiza chuki.
Huo uonevu wa waislamu unafanywa na nani? JK, IGP, Usalama wa Taifa, Makamba? Jaji Mkuu? Waziri wa Mambo ya Ndani? Je hao hawaswali nao kuwaekeza kuhusu huo uonevu? Hao ma-ustadh na masheikh hawajui nani wa kumueleza matatizo yao?
Haya, wametoa tamko. Wat next? Chuki inayopandikizwa kwa baraka za viongozi walioko madarakani itakuja kuwa majuto. Mpango uliopo ni kuisolate CDM na waislamu ili CCM iendelee kutawala. Waislamu wanatumika. CCM wanajua kabisa CUF ikijaa waislamu wakristo watashun away. And that way CUF n CDM will not oust CCM. That is there thinking!