Matamko ya (baadhi) waislam (Dar na Mwanza)

Matamko ya (baadhi) waislam (Dar na Mwanza)

Status
Not open for further replies.
wakiristo watz wanaona taifa mbele pale penye maslahi yao tu, penye maslahi ya dini nyengine hupinga kwa nguvu zote
 
Nimekupata kaka ila tatizo letu sisi waislam hatuwezi ku walk on our words, hao walioandika huo waraka wakipigwa mpunga na pesa kidogo wanauza maslahi yetu kwa kitu. Wachache sana wenye kuweza kusimama kidete mfano Sheikh Ali Basaleh lakini hana msaada wowote.

Mfano kwenye ilani ya chama chetu tawala ya mwaka 2005 iliyoandaliwana idara ya itikadi na uenezi ya chama na kupitishwa kwenye CC ya chama kulikuwa na kipengele cha mahakama ya kadhi. Tuache unafiki wote waliisifia ile ilani mapadre, makasisi na mashekhe wakamuita JK chaguo la Mungu. Ilipokuja mjadala wa mahaka ya kadhi kilichotokea sote tunakijua.

Silaha ya waislam ilikuwa kwenye sanduku la kura lakini kwa mgawanyo wetu na unafiki wetu yaliyojiri mnayajua sina mengi ya kusema ila ukweli utabaki pale pale. Itatuchukua miongo mingi sana kujipanga kupata solution ya matatizo ya kiislam na uislam.

My Take,

Waislam hawawezi kubadilika na hawatabadilika.

Aisee ndugu yangu, sijui nikupe zawadi gani?? ebu chagua
 
Kwa hiyo wewe peke yako ndio muislamu sio? au unayo detector ya kujua dini za wana JF?

Fatilia post utajua kwa nini nimesema hivyo, muongo, maneno/maandishi yake ndio yaliyo muumbua, you don't need any detector, just read between the lines
 
Ahsante sana Mkuu. Waislamu wengi ni wanafiki sana. Wengine wanadiriki hata kusema kwamba Kikwete anaandamwa kwa sababu ni Muislamu na hivyo wanamuoandama ni Wakristo kwa kuwa wanataka Rais awe mkristo mwenzao.

Ukiwaambia anaandamwa kwa kuwa ni kiongozi mbovu na kuna ushahidi wa kutosha kwamba kazi ya kuongoza nchi imemshinda hawakuelewi hata kidogo kwao wao Kikwete kafanya mengi sana. Sijui mengi yepi ambyo yamefanywa na Kikwete ukiondoa usanii.

Prejudices....another one so called great thinker!!
 
MSHAURI wa jopo la masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Iddi Simba, amesema nchi ipo hatarini kwa sababu amani na utulivu wa Tanzania vimeanza kutoweka.

Simba aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya Awamu ya Tatu, aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya utoaji wa vibali vya sukari, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati jopo hilo likizungumza na waandishi wa habari kuhusu mustakabali wa taifa.

Alisema kuwa ni vema amani na utulivu uliopo vikaenziwa badala ya watu kutoa kauli za kuchochea vurugu za kisiasa na kidini.

"Kila neno linalotolewa na wanasiasa au viongozi wa dini lina uzito wake, tunaonya amani na utulivu vimeanza kutuponyoka ni vema tukawa makini," alisema.

Alibainisha kuwa jopo hilo si kundi la wababishaji au lenye kutafuta madaraka katika jamii bali ni la watu makini wasiopenda kubezana, kukejeliana na vitendo vingine vyenye lengo la kuigawa jamii.

Awali kabla ya Simba kutoa kauli hiyo, mratibu wa jopo hilo, Sheikh Mohamed Idd Mohamed, alitoa tamko la kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kutomkebehi na kumkejeli Rais Jakaya Kikwete.

Sheikh Mohamed alisema kejeli na kebehi hizo hazisaidii kuimarisha amani na demokrasia bali zinavunja.
Alisema wananchi hawana budi kuzingatia utawala wa sheria na kutii amri za mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.

"Jopo la masheikh linawaasa Watanzania kuzingatia utawala wa sheria na kutii amri za mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa sheria za nchi na linatabanaisha kuwa kupinga amri za mamlaka za kisheria ni kupinga amri za Mwenyezi Mungu aliyeziweka," alisema.

Sheikh huyo aliongeza kwamba ni kosa kutoitii mamlaka hiyo, ni kusababisha uvunjifu wa amani na kupoteza roho na mali kama ilivyotokea Arusha hivi karibuni.

Katika maelezo yake, alisema wamesikitishwa na kauli ya maaskofu zilizoonyesha kuunga mkono matakwa ya chama cha siasa na kufikia kutomtambua kiongozi wa kisiasa kwa misingi ya kisiasa.

Alisema viongozi hao wanasahau wao ni viongozi wa dini yao na wala si viongozi au wasemaji wa vyama vya siasa.

Jopo hilo limewataka maaskofu kuacha mara moja mwenendo huo mbaya unaoweza kuwagawa viongozi wa vyama vya siasa, wanasiasa na watendaji wa serikali kwa misingi ya dini na kuisambaratisha nchi.

Aliwataka maaskofu kuacha mara moja mwenendo huo mbaya unaoweza kuwagawa viongozi wa kisiasa na watendaji wa serikali kwa misingi ya kidini, na kusambaratisha nchi vipande vipande.

Aidha, kwa upande mwingine linampongeza Rais Kikwete kwa kuona umuhimu wa kuunda Tume ya Katiba. Sheikh Mohamed, alisema jopo hilo linampongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuona umuhimu wa kuunda Tume ya Katiba ambayo wanaamini itafanya kazi itakayokidhi matarajio ya Watanzania.
 
Fatilia post utajua kwa nini nimesema hivyo, muongo, maneno/maandishi yake ndio yaliyo muumbua, you don't need any detector, just read between the lines

Kaka comprehension ngumu eeh? kwa hiyo mimi nikisema, mathalan, 'Watanzania wanahitaji serikali thabiti', ina maana mimi si mtz? au mpaka nikuoneshe kitambulisho cha kupiga kura ndio uamini?
 
Mimi nadhani ni upumbavu kushambuliana juu ya imani ya mtu au watu. Ni ujinga pia kutumia dini katika kuhalalisha udhaifu wako katika maisha.

Kwa ajili ya hayo ndio maana Palestina na Israel wanadundana kila kunapoitwa leo. Ishmail na Isaka are trully two individuals with a huge contrast in many avenus. Lakini historia yenye maana ni ile inayomsaidia binadamu kujisahihisha na kumwezesha aishi katika mazingira yaliyo bora zaidi. Wivu wenye maana ni ule uletao tija. Lakini utamsaidiaje mtu aliye mvivu wa kufikiri na akipenda sana majibu rahisi kwa maswali yaliyo mazito?

Haya, tuendelee kupigania madrasa, halafu tukasome katika shule za wakristo, kisha tutumie Biblia yao wakristo kuwazodoa. Baadaye vizazi vijavyo vitatuhukumu waislam kwa kuendekeza mawazo finyu. Waislam tumejikuta twaishi kama katika chama cha siasa, hatuwezi kuibua mambo yenye kuisaidia jamii na badala yake tunavizia wakristo wamesema nini kisha tunasimama kuwapinga. Hiyo ndiyo hasa historia kati ya Ishmail na Isaka.

Heri wenye akili kuanzia rohoni maana hao Mola wao atawaongoza kuelekea maisha yenye furaha.
 
Kaka comprehension ngumu eeh? kwa hiyo mimi nikisema, mathalan, 'Watanzania wanahitaji serikali thabiti', ina maana mimi si mtz? au mpaka nikuoneshe kitambulisho cha kupiga kura ndio uamini?

CRAP!! Ndio wale wale wakikamatwa wanaiba wanasema walikua wanaonja tu!! au nilikua naongea mimi kama mimi na sio waziri hahahha

Hivi nini kina kutuma kutumia jina zaidii ya moja, Mohammed Shossi ??
 
Idd Simba: Nchi ipo hatarini

na Salehe Mohamed

MSHAURI wa jopo la masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Iddi Simba, amesema nchi ipo hatarini kwa sababu amani na utulivu wa Tanzania vimeanza kutoweka.

Simba aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya Awamu ya Tatu, aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya utoaji wa vibali vya sukari, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati jopo hilo likizungumza na waandishi wa habari kuhusu mustakabali wa taifa.

Alisema kuwa ni vema amani na utulivu uliopo vikaenziwa badala ya watu kutoa kauli za kuchochea vurugu za kisiasa na kidini.

"Kila neno linalotolewa na wanasiasa au viongozi wa dini lina uzito wake, tunaonya amani na utulivu vimeanza kutuponyoka ni vema tukawa makini," alisema.

Alibainisha kuwa jopo hilo si kundi la wababishaji au lenye kutafuta madaraka katika jamii bali ni la watu makini wasiopenda kubezana, kukejeliana na vitendo vingine vyenye lengo la kuigawa jamii.

Awali kabla ya Simba kutoa kauli hiyo, mratibu wa jopo hilo, Sheikh Mohamed Idd Mohamed, alitoa tamko la kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kutomkebehi na kumkejeli Rais Jakaya Kikwete.

Sheikh Mohamed alisema kejeli na kebehi hizo hazisaidii kuimarisha amani na demokrasia bali zinavunja.

Alisema wananchi hawana budi kuzingatia utawala wa sheria na kutii amri za mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.

"Jopo la masheikh linawaasa Watanzania kuzingatia utawala wa sheria na kutii amri za mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa sheria za nchi na linatabanaisha kuwa kupinga amri za mamlaka za kisheria ni kupinga amri za Mwenyezi Mungu aliyeziweka," alisema.

Sheikh huyo aliongeza kwamba ni kosa kutoitii mamlaka hiyo, ni kusababisha uvunjifu wa amani na kupoteza roho na mali kama ilivyotokea Arusha hivi karibuni.

Katika maelezo yake, alisema wamesikitishwa na kauli ya maaskofu zilizoonyesha kuunga mkono matakwa ya chama cha siasa na kufikia kutomtambua kiongozi wa kisiasa kwa misingi ya kisiasa.

Alisema viongozi hao wanasahau wao ni viongozi wa dini yao na wala si viongozi au wasemaji wa vyama vya siasa.

Jopo hilo limewataka maaskofu kuacha mara moja mwenendo huo mbaya unaoweza kuwagawa viongozi wa vyama vya siasa, wanasiasa na watendaji wa serikali kwa misingi ya dini na kuisambaratisha nchi.

Aliwataka maaskofu kuacha mara moja mwenendo huo mbaya unaoweza kuwagawa viongozi wa kisiasa na watendaji wa serikali kwa misingi ya kidini, na kusambaratisha nchi vipande vipande.

Aidha, kwa upande mwingine linampongeza Rais Kikwete kwa kuona umuhimu wa kuunda Tume ya Katiba. Sheikh Mohamed, alisema jopo hilo linampongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuona umuhimu wa kuunda Tume ya Katiba ambayo wanaamini itafanya kazi itakayokidhi matarajio ya Watanzania.

My Take:

Ushauri mdogo tu kwa Idd Simba, "Charity begins at home"

Waislam hawana WIVU ya maendeleo walionayo wakristo. Wakristo ndio wenye WIVU wasiopenda waislam nao kuiubuka...

kama wakristo wana nguvu...Basi waambieni Wafute Misamaha ya KODI....Taasis walizonazo wameshindwa kuziendesha...na lazima wapate support ya Serikali.

Tunachotaka waislam HAKI sawa kwa wananchi wote. Mnaojenga Matabaka ktk nchi,haitowasaidia chochote.
 
Duh Kazi kwelikweli ndugu zangu Wasislamu nyie mlioandaa waraka huu...

Ngoja niseme... kama hawa ndio viongozi wetu wa Kiislamu wenye mtizamo huu duh itatuchukua muda mrefu sana kufanikisha maendeleo ya Waislamu... Maendeleo hayaletwi kwa kulalamika na majungu dhidi ya kundi lingine... huletwa na mikakati na mipango inayokusudiwa ikibainisha rasilimali hitajika na muda utakaohitajika kuyatimiza... ikiambatana na hamasa...

Ninatarajia watueleze mikakati waliyonayo kuweza kuimarisha mashule na hospitali na vyuo vya ufundi na vinginevyo na kuweza kuhamasisha Waislamu kujizatiti katika elimu ili wafuzu na kuingia kwenye mitandao na kuweza kufikia opportunitites sawa...

Dini ya kiislamu si ya kijinga hivyo ila wako wanaoitumia vibaya na kujaribu kujastify mambo yao na hushawishi sana kiasi cha kukusanya wengi kwa ujinga wao....

WAISLAMU NYIE (maana si wote ni wajinga hivyo) AMKENI CHANGISHANENI FUNGUENI MASHULE, MAHOSPITALI VYUO VYA UJUZI, ACHENI MAJUNGU... NA FITINA wivu wenu uwe kwenye jinsi mtakavyo fanya nini mtoke sio kwanini wale wamefika kule bila kusema na sisi tutafikaje...
 
CRAP!! Ndio wale wale wakikamatwa wanaiba wanasema walikua wanaonja tu!! au nilikua naongea mimi kama mimi na sio waziri hahahha

Hivi nini kina kutuma kutumia jina zaidii ya moja, Mohammed Shossi ??

Sums up all.

Eti Mapambano, pambana na UJINGA KWANZA.
 
Kinachonishangaza ni kimoja tu, matamko haya ynatolewa baada ya maaskofu kutoa matamko yao hali inayoonyesha kama vile mnatumiwa kuwajibu.

nadhani masheikh walitakiwa kuwa wabunifu na kutokusubiri mpaka maaskofu watoe kauli zao ndipo wadese in opposite way.
 
Nauliza tena:

1) Ulipokuja waraka wa wakatoliki hamkuona tatizo ???

2) Maaskofu walipoanza kufanya kampeni za siasa, hamkuona tatizo??

3) Maaskofu, waliyofanya Rukwa, hamkuona tatizo??

4) Maaskofu, kutomtambua Meya Arusha (Sheria na siasa), hamkuona tatizo ???

Wanafiki wakubwa nyie, kama matatizo ya serikali rushwa, ufisadi wote tunapinga. Lakini nafsi zenu zinawasuta kwa sababu mmejaa udini na chama chenu chadema hamtaki watu wawakosoe.

Hao masheikh, Maaskofu ni watu, na watu wanakosea na kufanya makosa. Lakini kwa sababu ya udini wenu mlishindwa kuona hilo...
 
Huo ndio udanganyifu wenu kama kwamba munacheza na watoto wadogo.Hizo resource za kanisa ni zipi?.
Hayo mambo mungeyafanya bila MOU na kulazimisha misamaha ya kodi tungewaelewa.Kinyume cha hapo ni kutaka kuchukua majukumu ya serikali kupitia mlango wa nyuma na kukuza dini yenu kupitia mabezo kwa waislamu.Hapa ndipo ambapo waislamu wamewashtukia.

Nadani misamaha ya kodi wanapata taasisi zote za dini, taasisi za kislamu na kikristo sasa kwa nini waislamuu hawatake advantage ya misamaha ya kodi, na misamaha hiyo inatolewa kwa taasisi za dini kwa sababu hazifanyi biashara zinapoingiza madawa kwa ajili ya hospitali na zahanati, vifaa vya ujenzi wa shule, misikiti, au makanisa etc, which is a good thing and both side of the isle benefit from misaaha ya kodi sasa mbona tunaoneana gere,

MOU-Je waislamu wamejaribu kuiomba serikari kuingia nayo ubia kutoa huduma za afya au elimu kwenye vituo vya kislamu wakakataliwa, kwanini msiwe creative and convince the government you can do something kwa jamii na serikari can cooperate with you.

kuhusu MOU, mashirika ya dini ya kikristo yanajenga shule na zahanati na serikari inasaidia uendeshaji kwa kuwalipa wataalamu na utoaji wa baadhi ya vifaa, so this is a partnership between mashirika ya dini na serikari and every single cent is counted for, hivyo pesa hizo haziwezi kutumiwa kwa mambo mengine kwani hazitolewi ki holela kama mnavyofikiri, kila senti ipo kwenye bugdeti, hivi hakuna watu wa maana wanaweza kufatilia na kujua kuwa mashirika ya dini ya kikristo ndo yanayoisadia serikari na jamii yetu kwa ujumla, na project zote zilizo kwenye MOU ni kwa manufaa ya watanzania wote
 
Executive Kandamiza Ng'wana... Big Up hiyo imekaa vizuri...
 
Duuuuuuuuuuuuu!

Kama hao walioandika waraka huo ni ile cream ya waislam basi waislam bado mtaendelea kudhulumiwa. Lakini mimi sikubaliani kwamba hayo ni mawazo ya waislam wote. Leo tuna waislam waeledi tena wengi sana tofauti na waraka unavyosema eti wasomi waislama ni wachache. Sasa mawazo ya wasomi waislam kwenye waraka huo yako wapi?

Ukitaka kujua mwandishi wa waraka huo ni Mwalimu wa Madrassa angalia suggestion yake ya kugawa nchi kwa misingi eti maeneo yenye waislam wengi ndio iwe nchi ya waislam na yenye wakatoliki wengi iwe ya wakristo, sasa kwa Tanzania ya leo, maeneo hayo yako wapi?

Naona tujadili matatizo yanayotugusa kama watanzania bila kujali itikadi za dini, maana ufisadi unatuumiza wote wakristo na waislam
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom